Pages

Sunday, November 4, 2012

Familia ya Mwangosi kuishtaki Serikali

Itika Mwangosi-mjane
Familia ya aliyekuwa Mwandishi wa kituo cha televisheni cha chaneli ten, Marehemu Daudi Mwangosi, imepanga kuishtaki Serikali na jeshi la polisi kufuatia mauaji hayo ya kinyama. Mauaji hayo ya mwandishi huyo wa habari yameweka rekodi ya mwandishi kuuliwa mbele ya polisi katika taifa hili la Tanzania.
 
Familia inatumai kwamba hatua za kisheria zitaisaidia kutoa ukweli wa wazi kabisa na hivyo kumfikisha muuaji katika haki. Mjane wa Daudi Mwangosi, Ms Itika Mwangosi amesikitishwa na taarifa ya tume ya kuchunguza mauaji ya mume wake iliyoundwa na Waziri wa mambo ya Ndani Dr. Emannuel Nchimbi. Itika mwangosi amesema srekali haina nia ya thabiti ya kuelezea kile kilichotokea na hana imani na jinsi kesi iliyoko mahakamani jinsi inavyoendeshwa.
 
Itika Mwangosi ameshangazwa na hatua ya tume hiyo ya kutotaja muuaji wa mume wake na kuona ni kama vile imepoteza fedha za walipa kodi katika kuchunguza tukio hilo. "Tunajua kuna baadhi ya watu wanataka kuficha ukweli juu ya suala hili na sisi tutaipeleka serikali mahakamani ili haki itendeke" alisema Mjane wa Mwangosi. Hakuna kitu kitakachonipa faraja kama muuaji wa mume wangu kuhukumiwa kwa kile alichotenda" alimalizia Ms Itika Mwangosi.....
 
Kwa taarifa zaidi fuatilia link hii....The Citzens
 
 

No comments:

Post a Comment