Mbunge wa jimbo la kawe Mh Halima Mdee amesema Genetic Modification ni sumu na haina tija kwa wakulima wa Tanzania, zaidi itaongeza umaskini. Mh Mdee ameyasema hayo wakati akichangia muswada wa sheria ya kulinda haki ya ugunduzi wa aina mpya ya mbegu leo hii jioni bungeni mjini Dodoma.
Mh Mdee amesema sheria itakayoundwa kwa kiasi kikubwa haitawatambua wakulima wa hapa nchini kama wazalishaji wa mbegu za asili za mazao mbali mbali. Akitolea mfano zao la pamba, amesema kuwa serikali imeingia mkataba na kampuni ya kigeni kutoka Zimbabwe inayofanya kazi ya kuzalisha mbegu mpya za pamba.
" Kinachofanyika kampuni hiyo hununua mbegu hizo kwa wakulima wetu wa hapa nchini kwa bei ya chini, na kuzifanyia mabadiliko kidogo na kuja kuziuza tena kwa wakulima kwa bei ya juu" alisema Mh Mdee. Kwa kitendo hicho ni kwamba kampuni hiyo inapata hakimiliki kama wazalishaji wa mbegu mpya ilhali zimenunuliwa kwa wakulima wa hapa hapa.
Mh Mdee aliendelea kuihoji serikali kuhusu kuwa na ushirika na kampuni ya MONSATO ambayo inatajwa kuwa imefunguliwa kesi nyingi na baadhi ya nchi kwa utendaji wake mbovu wa kazi. Kampuni ya MONSATO inatajwa kuwa ni mdau namba moja katika kuisadia serikali katika kutekeleza programu ya kilimo kwanza
No comments:
Post a Comment