Wapenzi wa blog hii nimeamua kubadili mfumo wa blog hii kutoka katika kuleta taarifa mbali mbali za kijamii na kujikita zaidi na dhana nzima ya ujasirimali. Blog hii itakuwa inakuletea tips mbalimbali za ujasiriamali kwa kadiri ya uwezo utakavyokuwa unapatikana. Hivyo nategemea mafunzo mengi pia kutoka kwa wasomaji wa blog hii ili tuweze kuondoka katika mzunguko huu wa umasikini.
Lengo kuu ni kusaidia watanzania wenzangu kujua mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wafanyabiashara mbali mbali kupata mafanikio ya kibiashara, kutumia mbinu hizo kwa kuiga ama kuibua mbinu mbadala ili tuweze kuondokana na umaskini.
Huku idadi ya watu ikizidi kuongezeka duniani na Nchini kwetu kwa ujumla, changamoto kuu imekua suala la ajira. Kila mmoja wetu anataka kuajiriwa aidha serikalini ama kwenye sekta binafsi huku suala la kujiajiri likiwa la mwisho katika vipaumbele.
Ujasiriamali ni nini?
Kwa sasa ni jina maarufu sana hapa Tanzania, mtu yeyote aliyefanikiwa katika biashara hupewa jina hili. Maana ya ujasirimali inabaki katika uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wa kutumia rasilimali chache zinazokuzunguka vizuri ili uweze kupata faida.
Mathalani rasilimali zinazokuzunguka ni ardhi, watu na maji, ni vipi mchanganyiko huu utautumia vizuri ili uweze kupata zao (output) ambayo itakusaidia kujikwamua katika hali uliyonayo. Ama ni vipi utatumia mtaji mdogo ulionao kufanya biashara itakayokuletea faida ambayo utaitumia kuongeza mtaji na kuikuza biashara yako.
Fahamu kwamba lengo lolote la mjasiriamali ni kupata faida na kumridhisha mteja ambaye anatumia bidhaa ama huduma inayotolewa na mjasiriamali. Bidhaa ama huduma ndio msingi wa mjasirimali yeyote ambaye anataka kupata faida. Mathalani mkulima wa mahindi bidhaa yake ni mahindi hivyo atauza mahindi kujipatia faida, na mtabibu wa mifugo anatoa huduma ya matibabu kwa mifugo na kulipwa ujira kwa kutoa huduma hiyo.
Itaendelea....
Niandikie: mmlanzi@yahoo.com
No comments:
Post a Comment