Pages

Wednesday, August 1, 2012

Profesa Mwandosya atinga bungeni na kushauri wabunge wapime afya zao.


Waziri wa ofisi ya raisi asiye na wizara maalum Profesa Mark James Mwandosya amehudhuria kikao cha bunge leo baada ya kuwa nje kwa muda mrefu. Mh mwandosya alikuwa akitibiwa kwa muda mrefu nchini India alionekana bukheri wa afya aliyejaa tabasamu usoni.

Alikuwa kaimu Waziri wa Afrika Mashariki Mh Sitta aliyeomba utaratibu kwa mwenyekiti wa bunge Mh Mhagama kuwa Mh Mwandosya apewe japo dakika kadhaa awasalimu waheshimiwa wabunge.

Mh Mhagama aliridhia ombi hilo na kumpa dakika tano ili aweze kutoa shukrani kwa wabunge. Mh Mwandosya alianza kwa kumshukuru Mwenyezimungu kwa kumpa ahueni katika maradhi yaliyokuwa yanamsibu, na kisha akaendelea kuwashukuru waheshimiwa wabunge kwa maombi yao kwake kipindi chote alichokuwa anaumwa.

Mheshimiwa Mwandosya aliwashauri wabunge wawe na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kujua matatizo yanayowasibu, kwa kuwa yeye amekaa takribani miaka 45 bila kuugua. Aliendelea kusema afya ni muhimu kuliko jambo lolote lile na akatania kwa kuomba muongozo kwamba kama kilimo ni muhimu kuliko afya.

No comments:

Post a Comment