Swali 1. Nini tofauti ya Mfumo wa utangazaji wa Dijitali na mfumo wa utangazaji wa analojia ambao unatumika kwa sasa?
Jibu.
Tofauti ya mifumo hii miwili,(analojia na dijitali) iko kwenye usafirishaji wa mawimbi ya sauti na picha. Kwa asilia mawimbi ya sauti au ya picha yako kwenye mfumo wa analojia. Mawimbi yaliyo kwenye mfumo wa analojia yanaposafirishwa mbali kwa msikilizaji/mtazamaji yameonyesha kupoteza ubora wa sauti na picha. Mawimbi yanapobadilishwa kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali yanaposafirishwa kwenda mbali yameonyesha kuwa na ubora wa sauti na picha. Dijitali ni mfumo mpya ambao unatumia paketi kusafirisha data.
SWALI. Kwa nini tunahama kutoka mfumo wa utangazaji kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo wa utangazaji kwa kutumia teknolojia ya dijitali?
JIBU.
Sababu kubwa ni faida zilizoko kwenye matumizi ya mfumo wa dijitali kulinganisha na mfumo wa analojia. Faida hizo ni kama ifuatavyo:
i. Ubora wa sauti na picha;
ii. Vifaa vya kuhifadhi habari (CD, VCD, DVD) ni vidogo na huifadhi habari
nyingi ukilinganisha na tape recorder na santuri ambazo ziko kwenye
mfumo wa analojia;
iii. Matumizi bora ya masafa. Kwa mfano chaneli moja ya analojia hutumiwa
na kituo kimoja cha utangazaji wakati kwa mfumo wa dijitali chaneli moja
hutmiwa na vituo zaidi ya kumi;
iv. Mitambo ya kurusha matangazo kutumia nguvu ndogo ya nishati;
v. Kuwepo kwa luninga za mkononi (Mobile TV) kwenye mfumo wa dijitali na
faida nyinine nyingi;
SWALI. Nini Tofauti kati ya Utangazaji wa Televisheni kwa kutumia miundo mbinu ya ardhini (Terrestrial) na utangazaji wa kutumia satelite
Jibu. Tofauti kati ya utangazaji unaotumia mitambo ya ardhini (Terrestrial) na utangazaji wa kutumia satellite ni kwamba Utangazaji kwa kutumia miundo mbinu ya ardhini unatumia minara na mitambo ya kurushia matangazo (Transmmitters) iliyosimikwa ardhini. Kwa kupokea matangazo ya mitambo hii mtazamaji na msikilizaji hupokea matangazo kwa njia ya antenna zinazofungwa juu ya nyumba au ndani.
Utangazaji wa satelaiti hutumia mitambo ya kurushia matangazo amabayohusimikiwa angani na kurusha matangazo ambayo humfikia mtumiaji kwa njia ya madishi au nyungo zinazofungwa mahali ambapo hakuna kizuizi kwa mawimbi (Masafa) yatokayo kwenye satelaiti. Ukubwa wa madishi haya hutegemeana na teknojia ya mawimbi yanayotumika.
Source: TCRA website
No comments:
Post a Comment