Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, na kiongozi wa upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe amesema sababu kuu ya watanzania wengi kupenda kulalamika kuwa ni uoga.Mh mbowe aliyasema hayo jana usiku, wakati wa hafla iliyoondaliwa na Wanadar es salaam wa CHADEMA iliyorushwa moja kwa moja na kitu cha Star TV, ya kuchangia mchakato wa vugu vugu la mabadiliko linalofanywa na chama hicho maarufu kama"Movement for Change".
Mh Mbowe ambaye alikaribishwa ili kuongeza nguvu ya hamasa ya kuchangia mchakato huo, amesema yeye ndiye muasisi mdogo kuliko wote wa CHADEMA, na ameishi takribani miaka 21 katika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi bila kuogopa ya kupigania mabadiliko katika nchi ya Tanzania.
Mh amewaomba watanzania kuwa waogope kutokuogopa na kuacha kunung'unika na sasa ni muda wa vitendo katika kupigania mabadiliko ya katika Taifa la Tanzania. Mh alienda mbali zaidi na kuwalaumu wasomi wengi Tanzania wamejitajirisha na kuepuka kusidia Taifa bila kuondoa mfumo mbovu uliopo hapa Nchini, na kuwapongeza wale wachache ambao wamejiunga katika mchakato wa kuleta mabadiliko.
Mheshimiwa aligeukia suala la elimu na kusema kuwa CHADEMA inathamini sana elimu kwa kuwa elimu ni msingi wa kila jambo, na kusema umaskini uliopo hapa nchini unasababishwa na elimu kudharauliwa, na kuongeza kuwa umaskini wa akili ni mkubwa kuliko ule wa rasilimali hapa Nchini. Mbowe alisema endapo CHADEMA kitashika hatamu kipaumbele cha kwanza kitakuwa elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu pia.
Rasmali zetu haziwezi kusimamiwa ipasavyo endapo watanzania wengi wa sasa hawana elimu mahsusi zinazohusiana na suala fulani mfano Gesi. Kuthibitisha hilo mheshimiwa Mbowe alisema 95% ya wasimamizi na watafiti wa rasmali zetu zinafanywa na wageni. Hii sio sahihi, na imefika hapa kwa kuwa elimu ambayo ndio msingi imedharauliwa. Mheshimiwa mbowe alisema elimu ni "Primary Contradiction na kama ukitatua primary contradiction then secondary contradiction will take care itself".
Mheshimiwa Mbowe alizungumzia pia kuwa CHADEMA haipo kwa ajili ya kupigania vyeo, bali kuunganisha nguvu za Watanzania kuleta mabadiliko hapa nchini. "CHADEMA kipo salama, na kitakuwa salama na sasa si wakati wa kuzungumza Uraisi ila wa kupambana" alisema Mh Mbowe.
Katika kuonesha kuipiga kijembe Serikali inayoongozwa na CCM , Mbowe alisema uongozi uliopo hauna uwezo wa kutawala kwa kuwa umeshindwa kusimamia masuala ya msingi, na kuwataka wananchi kutoogopa siasa kwani gharama ya kufanya hivyo ni kubwa. Mh mowe alimnukuu mwanafilosofia mmoja aliyesema" Gharama ambayo analipa mjanja,kwa kuogopa siasa ni kutawaliwa na dhaifu".
Mheshimiwa Mbowe aliomba makundi mbali mbali katika jamii ikiwamo walimu na madaktari wajiunge na chama hicho, kwa kuwa kinawajali.
No comments:
Post a Comment