Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!
Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:
Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?
Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.
Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:
kuzuia shughuli za Siasa (mikutano na maandamano) kipindi cha zoezi la kitaifa la Sensa kuanzia tarehe 25 Agosti 2012 hadi 08 Septemba 2012”. Uhalali wa Amri/Zuio hili ulithibitishwa pia na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika barua yake Kumb Na. DA. 112/ 123/ 01/ 34 ya tarehe 28/08/2010 na wakati wa mahojiano na Kamati ya uchunguzi tarehe 22 Septemba 2012.
Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.
Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?
Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?
Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!
Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:
Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:
Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?
Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?
Simply put, Ni ripoti ya kijinga.
Source: Jamii forum
Sawa mwanakijiji
ReplyDelete