Walimu
hao ni Lucas Chihwalo, Mgeni Shomari pamoja na Mkali Mlanzi, Mwalimu mkude
aliambatana na walimu hao kama Mlezi. Wanafunzi walijifunza mambo mengi ikiwamo
aina ya ng’ombe wa maziwa waliopo katika kituo cha masista Narunyu.
Tulipokelewa vizuri na wageni wetu ambao ni sista Editha Mbunda na Diana
Millanzi ambao ndio walikuwa waelekezaji wakuu.
Masista
hawa walituonesha mashine inayotumika kukata kata majani yanayotumika kulishia
mifugo (chopping Machine). Mashine hiyo ina uwezo wa kukata kata majani na kuwa
madogo kabisa hivyo kumuwezesha ng’ombe kula kiurahisi.
Kwa
upande wa mifugo tumejionea aina mbili ya Ng’ombe wa maziwa ambao ni jess ambao
wana rangi aina ya dark red pamoja na fresian wenye mabaka meusi na meupe.
Katika aina hizi mbili fresian ndio hutoa maziwa kwa wingi ukilinganisha na
aina nyingine. Kuna changamoto kadhaa zinazofanya mifugo hii isitoe maziwa kwa
wingi ama zinazo zoretesha afya za mifugo hii. Mifugo hii huathiriwa kwa
kiwango kikubwa na Tsetse fly wanaosababisha ugonjwa wa Typanasimiosis, na kupe
wengine wanaosababisha ugonjwa wa ECF. Njia zinazotumika kuzuia magonjwa haya
ni njia ya kuosha mifugo hiyo mara kwa mara kwenye josho kubwa lililopo kituoni
hapo. Aidha kuna sista ambaye ana elimu ya kutibu mifugo hivyo hutibu mifugo
hiyo mara isumbuliwapo na magonjwa hayo.
Kuna
karakana kubwa iliyokuwa inatumika kuzalishia umeme kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe
(biogas) zamani. Wanafunzi walijionea jinsi kinyesi cha ng’ombe kinavyoweza
kutumika kuzalisha umeme kwa mafanikio.
Miradi
mingine inayopatikana katika kituo hiki ni kuku wa nyama pamoja na shamba kubwa
la miwa, mpunga ndizi pamoja na bustani. Wanafunzi wamejifunza mengi ambayo
hayapatikani katika chuo chetu, ni muhimu kwa safari hizi kufanyika kwani
huwaongezea ujuzi na uzoefu wanafunzi wetu ambao kwa muda mwingi huwa
wanajifunza kinadharia tu na si kivitendo.
Nawasilisha
wadau.
No comments:
Post a Comment