Zaidi ya wafungwa 60 wametoroka gerezani Nchini Liberia, katika jiji la Zwedru lililo kusini-Mashariki mwa Nchi Hiyo.
Redio ya Taifa ya Nchi hiyo imesema wafungwa hao walikuwa wana silaha na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea katika msitu ulio mpakani na nchi ya Ivory Coast.
Mji huo unahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka Ivory Coast waliokimbia machafuko yaliyotokana na uchaguzi wa mwaka 2010.
Mashambulizi yameripotiwa kutokea Ivory coast kutoka katika Nchi jirani ya Liberia katika miezi ya hivi karibuni.
Source:BBC-Africa
No comments:
Post a Comment