Pages

Saturday, June 30, 2012

"Kipigo kililenga kumnyamazisha Ulimboka"-CWT

Na Pamela Chilongola,Issa Lazaro (SJMC) CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema tukio la kutekwa nyara na baadaye kujeruhiwa kwa Dk Steven Ulimboka, linalenga katika kuwanyamazisha wanyonge wanaodai haki zao. Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatano. Katika tukio hilo watu wasiojulikana, walimteka nyara kiongozi huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, akiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni na baadaye kupelekwa katika Msitu wa Pande.www.mjengwa.blogspot.com

Friday, June 29, 2012

Mnyika na mgomo wa madaktari

Sababu ya hali tete ya nchi na maisha ya wananchi kwenye sekta ya afya ni udhaifu wa serikali na uzembe wa bunge. Rais Jakaya Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka Steven na kutoa ahadi ya kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kushughulikia chanzo cha mgogoro. Spika Anna Makinda aruhusu bunge litumie mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha.( Chanzo Mjengwa blog).www.mjengwa.blogspot.com