Pages

Saturday, September 29, 2012

Maige sasa ahojiwa na Takukuru

Fidelis Butahe
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemvaa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na kumhoji kuhusu tuhuma kadhaa zinazomkabili, ikiwamo kumiliki ghorofa la mamilioni ya fedha, jijini Dar es Salaam.

Katika siku za hivi karibuni, Maige amekumbwa na kashfa kadhaa kubwa ikiwamo ya kumiliki nyumba yenye thamani ya Dola 410,000 za Marekani (sawa na Sh700 milioni), nyumba ambayo ilizua mjadala mkubwa huku baadhi ya watu wakihoji namna alivyopata fedha hizo wakati akiwa mtumishi wa umma.

Kashfa nyingine dhidi ya Maige ni ile ya kujimilikisha vitalu na kufanya biashara ya wanyama hai, akiwa waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii.

Habari zilizopatikana jana zilisema mbali na kuhojiwa kuhusu nyumba hiyo, pia alihojiwa kuhusu tuhuma mbalimbali ikiwamo ile iliyomfanya Rais Jakaya Kikwete amwondoe katika Baraza la mawaziri.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu suala hilo, Maige alisema asingependa kulizungumzia na kwamba hajahojiwa na Takukuru.

"Sipendi kuzungumzia hilo, hata hivyo mimi sijahojiwa na Takukuru, niko Mwanza katika shughuli zangu binafsi," alisema.
Tuhuma nyingine zinazomkabili zinatokana na Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa wakati Maige akiwa waziri, ikieleza kuwa ofisi yake ilipoteza Sh874,853,564 baada ya kufanya uamuzi wa upendeleo wa kutoa kiwango cha chini cha mrabaha katika mauzo ya misitu.

Katika kipindi cha ukaguzi wa hesabu za Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (Tanapa), ilibainika kuwa shirika liliingia mkataba na Kampuni ya CATS Tanzania LTD , kuhusu matengenezo ya kawaida, ufungaji wa vifaa vya mawasiliano na vifaa vingine katika mkataba wa jumla ya Dola milioni moja za Marekani.

Maige pia anakabiliwa na tuhuma za kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, ugawaji ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwamo kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha vitalu walivyopewa.

Pia, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo, hazikuomba na kwamba vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili.

Habari zaidi zilisema kuwa Takukuru pia imepanga kufuatilia mali zake katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ili kubaini kama alichokiorodhesha ni sahihi.

“Takukuru wamesema hiyo ni moja ya kazi zao za kila siku, kuchunguza tuhuma mbalimbali na ukipatikana ukweli, hukabidhi jalada kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)” zilieleza habari hizo.

Habari hizo zilisema Takukuru imeanza uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na hadi jana, Maige alikuwa amehojiwa mara tatu.

"Usiku wa kuamkia leo (jana), alihojiwa Makao Makuu ya Takukuru tangu saa 2 usiku hadi usiku wa manane. Alienda Takukuru akiwa na mwanasheria wake," ilisema moja ya chanzo cha habari.

Chanzo hicho kimeendelea kueleza kuwa mbali na kumhoji, Takukuru imewasiliana na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuchunguza tamko la Maige kuhusu mali zake.

Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alipotakiwa kuzungumzia suala hilo hakutaka kuthibitisha wala kukanusha.

Alisema “Siwezi kulizungumzia jambo hilo kwa kuwa sheria zinanibana.”

Mwanzoni wa wiki hii wakati anajibu maswali ya washiriki wa kongamano la kujadili utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kupambana na rushwa nchini na mapendekezo yanayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu wa 2012-2016, Dk Hoseah alisema uchunguzi wowote ukikamilika jalada hupelekwa kwa DPP.


Nyumba ambayo Maige anadaiwa kuimiliki ipo katika eneo la Mbezi Beach jijini Dares Salaam ambayo hivi karibuni alidaiwa kutafuta wanunuzi kwa Dola za Marekani 800,000 (takriban Sh700 milioni).

Watu wa karibu na Maige walilidokeza gazeti hili kuwa waziri huyo wa zamani, amefikia uamuzi wa kuuza nyumba hiyo, kwa kile alichoeleza kuwa ni kama mkosi kwake kwa kuwa ni moja ya sababu za mambo yake kuwa mabaya kisiasa.

Habari za awali zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate.

Mmoja wa madalali wanaouza nyumba za kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman (Ustadhi) alilithibitishia gazeti hili kwamba Maige alinunua nyumba moja kati ya nne zilizokuwa sokoni kwa wakati huo.

Hata hivyo, hakutaka kueleza alinunua nyumba hiyo lini na kwa gharama gani baada ya kueleza kuwa yeye siyo msemaji wa kampuni hiyo.

Baada ya kuibuka kwa taarifa hizo mwanzoni mwa mwaka huu, Maige aliliambia gazeti hili kwamba hakununua nyumba hiyo kwa Dola 700,000 kama ilivyodaiwa, bali aliinunua kwa Dola za Marekani 410,000.

Maige alifafanua namna alivyoinunua nyumba hiyo na kuonyesha nyaraka mbalimbali, huku akieleza kuwa sehemu ya fedha alizonunulia, zilikuwa za mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Alisema 2005 alipoanza kuwa mbunge alipata mkopo ambapo yeye na wenzake watatu, waliunda kampuni ya kusafirisha mzigo ya Splendid Logistic na kuanza kununua magari matatu na baadaye magari hayo yaliongezeka na kufikia saba.

Alisema kuwa Septemba, 2010 mwenzao mmoja alijitoa katika kampuni hiyo, hivyo waliamua kugawana mali kwa kuzingatia mtaji wa kampuni ambapo alipata magari mawili na mwenzake manne akiongeza kuwa gari moja kati ya hayo saba lilipata ajali.

Source: Mwananchi

Friday, September 28, 2012

Breaking Nuz...Mtu mmoja achunwa ngozi huko Iringa


Habari Kutoka IRINGA zinadai kuwa eneo la njiapanda ya Mlolo kuelekea Tanangozi kuna mtu kauwawa na kuchunwa ngozi. Taarifa zaidi juu ya tukio hilo fuatilia blog hii ama blog ya Fracis godwin (Mzee wa Matukio)

Ubunge sasa basi-Zitto

Na: Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma, MWANANCHI.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.

“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.” Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

“Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.

“Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

“CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Thursday, September 27, 2012

Wamachinga Wazua Tafrani Arusha,Gari La CUF Lapigwa Mawe



Mahmoud Ahmad,
Arusha Hali si shwari katika jiji la Arusha na viunga vyake baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kuzua tafrani mara walipovamia eneo la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la Kilombero na kisha kuanza kugawana maeneo ya kufanyia biashara kwa kujipimia.

Vurugu hizo zimetokea jana wakati Rais Jakaya kikwete akiwa jijini Arusha kufungua mkutano mkubwa wa mapinduzi ya kijani ambao umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nchi za Afrika,Amerika,Ulaya na Asia. Hatahivyo,katika vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha wananchi(Cuf),Athuman Abrahaman alishambuliwa kwa mawe na kisha kujeruhiwa eneo la usoni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema huku gari la matangazo la Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa mawe na spika zake kuharibika vibaya. Askari wa jiji la Arusha walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita na gari lao katika maeneo mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia wamachinga wote kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara zao.

Askari hao walikuwa wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo wakikahidi watachukua bidhaa zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za kisheria. Hatahivyo,baada ya muda mfupi ndipo askari hao wali anza kutekeleza majukumu yao ya kusomba bidhaa hizo na kisha kuzipakia ndani ya gari lao huku wakivipeleka katika ofisi za manispaa ya Arusha.

Hatua hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya kwa pamoja na kisha kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa mabati uliokuwepo na kisha kuanza kujigawia maeneo kwa kuyapima kwa kamba. Wamachinga hao zaidi ya 200 walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo kupora mali mbalimbali zilizopo ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na saruji zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo. Katika heka heka za kugawana viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao walikata miti iliyokuwemo ndani na kisha kuanza kuichoma kwa moto hali ambayo ilisababisha wingu zito la moshi kutanda hewani.

Hatahivyo,wakati tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa wamesheheni kwenye magari yao walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo hilo lakini hawakuonekana wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia wamachinga hao. Kitendo cha askari wa jeshi la polisi mkoni hapa kushindwa kuwadhibiti wamachinga hao kimetajwa kimetokana na uhaba wa askari kutokana na ugeni wa mkutano wa jana pamoja na kuhofia hali ya amani kuharibika jijini Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba wamachinga hao wamevamia eneo hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku akikitupia lawama chama kimoja cha siasa hapa nchini kwamba kimehusika katika kuhamasisha vurugu hizo. Alisema kwamba kwa sasa watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa kuwa wana ugeni mkubwa lakini alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kupiga mawe gari la Cuf na mfuasi wake si cha kiungwana.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole alisema kwamba kitendo cha wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja sheria na wataondolewa hapo hivi karibuni. Mkombole,mbali na kulaani tukio hilo alisema kwamba uongozi wa jiji umepanga maeneo mbalimbali ya kufanyia biashara na eneo hilo ni mali ya mtu binafsi ambapo alikuwa ameanza jitihada za kuliendeleza.
 

Mwalimu Mkuu ILboru asimamishwa kazi

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Kassim Majaliwa, amemsimamisha kazi Mkuu wa Sekondari ya Wenye Vipaji Maalumu ya Ilboru mjini hapa, Jovinas Mutabuzi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Miongoni mwa tuhuma hizo zilizotolewa na wanafunzi katika maandamano yao yaliyowafikisha hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Malongo ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, ikiwa ni pamoja na kujianzishia Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) kutokana na michango isiyo rasmi.

Vyanzo vingine vya Saccos hiyo inayokadiriwa kuwa na zaidi ya Sh milioni 800 vinadaiwa kuwa faini ambazo wanafunzi wamekuwa wakitozwa kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kuripoti shuleni, ingawa hazikuwa na stakabadhi.
Kutokana na tuhuma hiyo na nyingine, Majaliwa amemtea Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Lorna Nteles kukaimu kwa muda, huku akimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Khalifa Hidda kuteua mkaguzi wa ndani kuchunguza tuhuma zinazomkabili Mkuu huyo wa shule.

Majaliwa alifikia uamuzi huo jana mjini hapa, baada ya kusikiliza madai ya wanafunzi hao katika mkutano wa hadhara na kubaini kuwa hoja zao zina msingi. Moja ya hoja hizo ni madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma zikiwamo hizo Sh milioni 800 za Saccos kwa kuzikopesha kwa riba kwa walimu na watumishi wa shule hiyo.

Septemba 24 wanafunzi hao waliandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa, wakitoa shinikizo la kung’olewa kwa Mkuu huyo, ambapo pamoja na mambo mengine, walidai amechangia kudorora kwa taaluma, kuwadhalilisha kwa matusi akiwaita mashoga.

Mkuu wa Mkoa aliwasihi wanafunzi hao kurejea shuleni na kuendelea na masomo wakati suala lao likishughulikiwa, hata hivyo baada ya kurudi shuleni, walianzisha mgomo wa kuingia darasani ikiwamo kutokula chakula cha shule hiyo.

Hatua hiyo ilimlazimu Naibu Waziri, kufika shuleni hapo kuwasikiliza wanafunzi hao, ambapo kabla ya kufanya mkutano alitembelea maeneo yote yanayolalamikiwa na wanafunzi hao ikiwamo, jiko, mabweni na choo cha matundu mawili kinachodaiwa kujengwa kwa Sh milioni 25.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara shuleni hapo, Majaliwa aliwasihi wanafunzi hao kutovunja sheria kwa kuitisha migomo na maandamano yasiyo rasmi huku akimtaka Makamu Mkuu wa Shule kusimamia nidhamu kwa wanafunzi hao.
Naibu Waziri akiwa amefuatana na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wenye mabomu na silaha za moto, alitumia zaidi ya saa tano kutoa ufafanuzi wa madai ya wanafunzi hao ambao muda wote walionesha kumsikiliza kwa makini huku hoja yao kubwa ikiwa ni kumkataa Mkuu wao.

Hata hivyo, Majaliwa alikerwa na mabango aliyoyakuta yakiwa yamesambazwa katika majengo yote ya shule yakibeba ujumbe mbalimbali wa kumpinga Mutabuzi huku baadhi yao yakiwa yamechorwa vikaragosi vinavyomfananisha na marehemu Nduli Idd Amini wa Uganda.

Pamoja na kuwasihi kuwa wavumilivu wakati hatua zikichukuliwa, walipaza sauti wakidai kuwa hawako tayari kuingia madarasani bila kuondolewa kwa Mkuu huyo, hali iliyomlazimu Naibu Waziri kutoa tamko hilo na kuamsha shangwe na nderemo kwa wanafunzi hao.

Naibu Waziri pia alipiga marufuku michango isiyo na tija shuleni, matumizi ya simu za mkononi kwa wanafunzi, adhabu za malipo ya fedha, matumizi ya M-Pesa shuleni na kuagiza bodi za shule nchini kutatua matatizo ya wanafunzi mara yanapoibuka kabla ya kuleta madhara.

Source:  www.wavuti.com
 

Wednesday, September 26, 2012

Mtuhumiwa wa Mwangosi Mahakamani tena

Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.

Akisomewa shitaka lake na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian ngilangwa , amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 10 Oktoba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.

Kila wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuvaa miwani meusi kuhakikisha kuwa sura yake haionekani na waandishi hao.

Katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili DFP 2175 Toyota Land cruiser tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.
Source:Francis Godwin

Monday, September 24, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 
TAARIFA- KUSIMAMIA HAKI NA UWAJIBIKAJI, CHADEMA YAKATAA KUKUTANA NA KAMATI YA NCHIMBI

by ChademaTz on Monday, September 24, 2012 at 7:47pm ·
 
KATIKA kusimamia uongozi unaozingatia misingi muhimu ya haki za binadamu, sheria na utawala bora, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza msimamo wake wa kutotoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuchunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel ten, Daudi Mwangosi, kilichotokea Septemba 2, 2012, Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.
 
Msisitizo huo umekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo kukiandikia barua (isiyokuwa na Kumbukumbu Namba) CHADEMA, akiomba kamati yake ikutane na viongozi wa chama Septemba 25, ili kutafakari tukio hilo na matukio ya aina hiyo yaliyowahi kutokea hapa nchini.
 
Itakumbukwa kuwa Marehemu Mwangosi aliuwawa na Jeshi la Polisi akiwajibika kwa jamii katika shughuli za uandishi wa habari, wakati askari wa jeshi hilo walipovamia ofisi za CHADEMA Kata ya Nyololo na kuanzisha vurugu wakati wanachama walipokuwa wakiendelea na shughuli halali za ndani za chama.
 
Katika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CHADEMA kimesema wazi kuwa hakiko tayari kukaa na kutafakari juu ya kifo cha Mwangosi kama ilivyopendekezwa na kamati hiyo, kwani imeundwa kinyume cha sheria, huku pia ikiwa imeundwa na mtu ambaye kanuni za msingi za utawala bora, zinamtaka awe amejiuzulu au kufukuzwa kazi, kupisha uchunguzi huru juu ya mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la polisi, linalowajibika kwake kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Kamati hiyo pia inawahusisha polisi ambao katika tukio hilo ni watuhumiwa namba moja.
 
Mbali ya kusisitiza kuwa haiwezi kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haipo kwa mujibu wa sheria, CHADEMA kimeshangazwa na kusudio hilo la Kamati ya Nchimbi kutoa mwaliko wa kutaka kukutana na viongozi wa CHADEMA, huku ikitambua wazi msimamo wa chama hiki juu ya uwepo wa kamati hiyo mara tu ilipoundwa.
 
Kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haina mamlaka ya kisheria ya kuhakikisha ukweli mtupu unajulikana na haki ionekane ikitendeka kutokana na kifo hicho na vingine vingi ambavyo vimefanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, kwa masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa, ni kuhalalisha uvunjivu wa haki za binadamu, Katiba na sheria za nchi. CHADEMA haiko tayari kuona hali hiyo ikifanyika.
 
Katika kuonesha msisitizo wa kutokubali mwaliko wa Kamati ya Nchimbi inayotaka kutafakari matukio ya vifo ambapo Jeshi la Polisi limewanyang’anya watu wasio na hatia haki ya kuishi, katika barua yake ya majibu, CHADEMA pia kimeambatanisha nakala ya barua ya tarehe 10/09/2012 iliyowasilishwa kwa Rais, ili kamati hiyo iweze kuelewa msimamo mpana wa chama kuhusu mauaji ya kisiasa yanayofanyika nchini.
 
Kwa taarifa hii, CHADEMA kinaendelea kusisitiza maazimio ya Kamati Kuu ya Chama, ambayo pamoja na mambo mengine, iliazimia kuwa kutokana na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kisiasa yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli halali za chama, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu au Rais awawajibishe kwa kuwafukuza kazi ili wapishe uchunguzi huru na wa haki.
 
Pia Kamanda wa Polisi Iringa, Michael Kamuhanda, Kamanda wa FFU Mkoa wa Morogoro, na askari wote wanaoonekana kwenye picha wakiwa wamemzunguka Mwangosi muda mfupi kabla hajalipuliwa na kuuwawa, wakamatwe haraka na kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Mwangosi. Kinyume na hapo ni kuchezea akili za wapenda haki na uwajibikaji, ikiwa moja ya misingi ya amani Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.
 
CHADEMA inapenda kusisitiza kuwa itatoa ushirikiano kwa chombo kitachoundwa kwa mujibu wa Sheria huku ikitilia msisitizo wito kwa Rais kuunda Tume ya Kimahakama/Kijaji kuchunguza vifo vyote vyenye utata na vinavyohusishwa na masuala ya kisiasa kama tulivyopendekeza kwake hapo kabla.

Imetolewa leo Septemba 24, 2012 Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Habari wa CHADEMA
 

Wamasai na Waarusha watwangana Arusha...


Chanzo kimoja cha habari kinaarifu kuwa wamasai na waarusha wanapigana kugombea eneo huko oldonyasambo, ambapo ndani ya eneo hilo kuna shule, hivyo wanafunzi wameshindwa kutoka madarasani kutokana na mapigano hayo.

Habari zinaendelea kusema kuwa shule hiyo ndiyo chanzo cha ugomvi huo baada ya kila upande kusema ndiyo wamiliki halali wa shule hiyo hiyo.

Chanzo hicho kimesema kuwa,Polisi na FFU wameshindwa kuwaamulia,mapigano bado yanaendelea mpaka sasa.

Source: Jamii forum

Sunday, September 23, 2012


WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kuwa chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM zimevurugika kwa kuwa mafisadi wameingilia na kupachika watu wao kwa lengo la kulinda masilahi yao.

Sitta alisema hayo jana mjini hapa katika mahafali ya 11 ya Shule ya Msingi Kwema yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Shule ya Sekondari Kwema. Alisema watu waliojitokeza kugombea ni mapandikizi na vibaraka wa mafisadi hao. "Hivi karibuni tumepata aibu kubwa ndani ya chama chetu, wakati chaguzi zetu zikiendelea viongozi wamepitisha vipaza sauti vya mafisadi, kazi yao kubwa ni kulinda masilahi ya mabwana zao na kuwafurahisha," alisema na kuongeza: "Wameajiriwa kwa lengo la kupiga kelele, kupiga vijembe, kuwapamba wafalme wao ambao wamefanikisha kuwa wanapata madaraka hayo, lakini kubwa zaidi ni kuwa vibaraka."

Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema lengo kubwa la mafisadi hao ni kuhakikisha wanashika kila sehemu ya nchi ili iwe rahisi kwao kuendelea kutafuna rasilimali za nchi kwa kupitia watu wao. Alienda mbali zaidi na kutoa mfano wa miaka ya zamani ambapo nchi za Uingereza na Ufaransa kulikuwa na wafalme ambao walikuwa wakiwaajiri watu ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kumchekesha mfalme huyo hata kama atakuwa amekosea.

"Wachekeshaji wa mfalme wao wanawajibika kwa mfalme, kumsifia, kuremba kupiga vijembe, kuwa vibaraka, kujipendekeza, kumpamba, lakini kubwa zaidi ni kumchekesha mfalme hata kama amefanya mabaya,” alisema. Sitta alisema wachekeshaji hawana aibu kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa mfalme anafurahi kwa kila kitu hata siku akitembea uchi wao wanasema mfalme umependeza na kanzu yako inang'aa dhahabu. Alisema kuwa hali inazidi kuwa mbaya zaidi pale watu hao ambao ni vibaraka wanapojivunia kuwa vibaraka wa watu fulani huku wakipita na kujisifu usiku na mchana wakiwatambia wajumbe.

Waziri huyo alisema umefika wakati wa chama hicho kuzaliwa upya vinginevyo kitaendelea kupata upinzani hata kutoka katika vyama vidogo. Hata hivyo, Waziri huyo alisema ataendelea kusema na wala hataogopa kitu chochote na atakayenuna na anune kwani yeye ni 'Chuma cha Pua' kwa kuwa anaamini anasimamia katika ukweli. "Ndiyo maana wengine
nikisema huwa wananuna, wananuna kwa sababu hawawatendei haki Watanzania. Nchi imejaa mali na rasilmali, lakini zinatumiwa na watu wachache wenye uchu badala ya kuzitumia sote," alisema na kuongeza: "Mimi ni msemakweli ndiyo maana kule kwetu Urambo wananiita 'Chuma cha Pua.' Watu wengine wanasema nailaumu Serikali wakati mimi nipo serikalini na kwamba hiyo ni aibu... Sasa aibu ipo wapi? Hapa mimi nipo ndani ya Serikali lazima niseme vitu hivi kamwe siwezi kunyamaza na kuacha mambo yakiharibika."

Source:www.mwananchi.co.tz


Sitta alilaani tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali wanaonyamazia maovu kwa kuwa tu wanaogopa kuonekana wabaya ndani ya jamii. Alisema viongozi wengine wamekuwa wanafiki kwa kuwa wako ndani ya Serikali na mambo yanaharibika wananyamaza hivyo nao kuwa kama wachekeshaji wa mfalme. Alisema watu wanatumia vibaya madaraka, kuna watu wazima wanafikiri kwa kutumia matumbo yao badala ya akili wakati mwingine wanajisahau na kuwa na matumbo makubwa mpaka yanawashinda. Aliwataka watu wote wanaohusika kuleta viongozi katika chaguzi hizo watumie fursa hiyo kuweka viongozi bora na si bora viongozi ambao wana masilahi yao binafsi.

Wakati hali katika chaguzi hizi zikienda ovyo, Waziri Sitta alisema pia kuwa amepata fununu mafisadi hao wanafanya kila njia kuhakikisha wanaweka vibaraka wao katika uongozi wa wilaya hiyo ili kuhakiksha wanaendelea kunufaika na migodi iliyopo katika wilaya hiyo. "Nimepata taarifa kuwa eti umeme unapatikana katika migodi ambayo inazunguka wilaya hii saa 24, lakini cha ajabu wananchi hawafaidiki na umeme huu. Hii inamaanisha nini hasa? Yaani wawekezaji ni bora sana kuliko wananchi? alihoji Sitta. Mahafali hayo pia yalihudhuriwa na Mbunge wa jimbo hilo, James Lembeli ambaye alisema shule hiyo imeujengea sifa mji wa Kahama kwa kuwa mwaka jana ilikuwa ya pili kitaifa na kutoa wanafunzi bora watatu katika 10 bora ambao walishika nafasi ya kwanza, tatu na ya nne.

Lembeni ambaye ndiye aliyeonyesha wazi kuanza kuchochea moto huo wa Sitta alisema kuwa wahitimu wa shule hiyo ndio wanaohitajika katika taifa la Tanzania kwa kuwa wamekuzwa katika misingi ya kutokupenda rushwa, kwani hata kujiunga na shule hiyo inahitaji uadilifu wa hali ya juu. Mkurugenzi wa Shule hiyo, Pauline Mathayo alisema hata siku moja hawezi kuruhusu vitendo vya kifisadi katika shule yake kwani anaamini elimu ikitumika vibaya inaweza kuzalisha watu hatari sana katika taifa. "Wote ni mashuhuda, sasa wizi wa benki kwa njia ya mtandao umezidi kuongezeka yote hii inatokana na kutumia elimu vibaya,"alisisitiza Mathayo.

Saturday, September 22, 2012

Mkuu wa wilaya Mbeya awatusi waalimu


Dr Norman Sigalla, Mkuu Wa Wilaya Mbeya. "Ualimu Ni Fani Ya Watu Waliofeli Hivyo Hawana
Sababu Ya Kudai Nyongeza Ya Mishahara".

Source: Jamii forum
 

Tuesday, September 18, 2012

How your shoes can tell your age...try this and see...........!!!!


1. Take your shoe size.2. Multiply it by 5.
3. Add 50.
4. Multiply by 20 ...
5. Add 1012.
6. Subtract the year you were born��

The first digit is your shoe size, while the last 2 digits are your age.

SURPRISED..................... ....................?

Before murdering Mwangosi, this is what police did.....at Nyololo.


Askari polisi Iringa wakimburuza mfuasi wa Chadema Nyololo wilaya ya Mufindi kabla ya kumuua Daudi Mwangosi kwa bomu ,huku askari kulia akikimbia na skafu ya kada wa Chadema sasa sijui walimrudishia ama lah?Hiki ndicho kikosi kilichoshiriki kuondoa uhai wa mwanahabari Daudi Mwangosi katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Sunday, September 16, 2012

Uchaguzi bububu...mabomu mtindo mmoja....

Katika kupitia site tofauti katika mtandao nimekuta habari hiyo hapo juu..kuwa mambo si shwari katika uchaguzi uliofanyika leo bububu....Zanzibar.

Thursday, September 13, 2012

Zengwe laanza kesi ya Mwangosi..Laptop yaibiwa hotelini


Habari kutoka mkoani Iringa zilizoripotiwa na mwandishi maalum wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com Kutoka mjini Iringa zinadai kuwa Kamati iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi kuja kufanya uchunguzi dhidi ya mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoani Iringa na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Iringa, Marehemu Daudi Mwangosi imeibiwa katika hoteli maarufu iliyokuwa imefikia .

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Leo ambapo mmoja Kati ya wajumbe wa tume hiyo ameamka na kujikuta mtupu Bila ya Laptop yake yenye nyaraka nyeti za kumwezesha kufanya uchunguzi huo kuibwa.

Inadaiwa kuwa Kamati hiyo pamoja na kuundwa na waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi ila bado imekuwa ikifanya kazi katika mazingira hatari zaidi baada ya kuwepo kwa habari kuwa imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu zaidi na makachero wa polisi.

Hata hivyo habari Kutoka ndani ya jeshi la polisi ambazo zinafanyiwa kazi na jeshi la polisi mkoani Iringa zinadai kuwa Kamati hiyo imeondoka asubuhi hii kuelekea Nyololo kuanza kufanya kazi yake .

Wednesday, September 12, 2012

Muuaji wa Mwangosi apandishwa kizimbani Iringa leo


Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa mahakamani.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu Michael Luena, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mtuhumiwa huyo mnamo Septemba 02 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.

Kila wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuziba uso kuhakikisha kuwa sura yake haionekanai na waandishi hao.

Katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili T 320 ARC Toyota Land cruiser GX tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.

Source: Francis Godwin Blog

Monday, September 10, 2012

Waandishi kuandamana kimyakimya nchi nzima

NI KESHO ASUBUHI, LENGO NI KULAANI MAUAJI YA DAUD MWANGOSI, KUTOA MATAMKO
Frederick Katulanda
WAANDISHI wa habari nchini kesho wataandamana nchi nzima kwa amani kulaani kuuawa kwa mwandishi mwenzao, Daud Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Iringa.
Maandamano hayo ambayo yatakuwa ya kimyakimya yatafanyika katika mikoa yote nchini kuanzia saa 2:00 asubuhi na waandishi watakaoshiriki katika maandamano hayo watavaa ama nguo nyeusi au watafunga vitambaa vyeusi mkononi ikiwa ni ishara ya kuomboleza na kulaani kuuawa kwa mwenzao.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), Theophil Makunga alisema kuwa uamuzi wa kufanyika kwa maandamano hayo ulifikiwa katika kikao cha jukwaa hilo kilichofanyika Dar es Salaam juzi.
Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, maandamano hayo yamepangwa kuanzia katika Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Mtaa wa Jamhuri ambacho Mwangosi alikuwa akikitumikia na kupita katika Mtaa wa Azikiwe, Barabara ya Bibi Titi hadi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambako maandamano hayo yatahitimishwa.

Alisema baada ya kufika katika viwanja hivyo, yatapokewa na viongozi wa TEF na kisha baadhi ya waandishi waliokuwapo katika eneo la tukio watatoa ushuhuda wa kilichotokea na kufuatiwa na mjadala kuhusiana na mauaji hayo na kutoa tamko la pamoja.

“Kutatolewa ushuhuda kutoka kwa waandishi wa habari ambao walishuhudia tukio la kuuawa kwa mwandishi mwenzao, wataeleza kwa kina hali halisi na ukweli waliouona siku ya tukio,” alisema Makunga.
Alisema tayari wamekwishawasiliana na Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ambako wamepeleka barua ya kuomba ulinzi kesho wakieleza njia watakazopitia siku hiyo.

“Tunafanya matembezi ya amani, kimyakimya kwa lengo la kulaani tukio la kusikitisha la kuuawa kwa Mwangosi. Ni mwandishi wa kwanza hapa nchini kuuawa akiwa kazini na doa kubwa kwa nchi yetu na vyombo vya dola, hivyo lazima tulilaani tukio hilo.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema, hajapokea barua hiyo na kusema kwamba inawezekana ipo kwa wasaidizi wake na hivyo kuahidi kuifanyia kazi.

“Sijaiona barua yao, inawezekana ipo kwa maofisa wangu au wameipeleka kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, nitafuatilia kujua ili kuona jeshi langu litafanya nini,” alisema.
Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji alisema kwamba lengo la maandamano hayo ni kulaani mauaji ya Mwangosi na zaidi ni kufikisha ujumbe kwa Serikali.

“Hatukupendezwa na mauaji hayo, yametuumiza na hatutopenda yatokee tena, tunayalaani na kuomba hatua kali zichukuliwe,” alisema Mihanji.

Maandamano mikoani

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan alisema, sambamba na maandamano hayo Dar es Salaam, pia waandishi wengine mikoani nao wataandamana kuungana na wenzao kulaani mauaji hayo ya mwenzao.
Maandamano ya mikoa yote nchini yatasimamiwa na klabu zote za waandishi wa mikoa husika na kwamba maandalizi yake ni pamoja na kubainisha njia watakazopitia kwa upande wa mikoani, yamekwisha kamilishwa. Alisema maandamano hayo yatapokewa na wenyeviti wa klabu ambao watatoa matamko mbalimbali kuhusiana na kifo cha Mwangosi.

“Kila mkoa hapa nchini utashiriki maandamano, wataandamana kwa amani kuungana na wenzao kulaani kifo cha mwandishi mwenzao, nao kama ilivyo kwa Dar es Salaam watavaa nguo nyeusi au vitambaa vyeusi mkononi,” alisema.

Alisisitiza kwamba kama itakavyokuwa kwa yale ya Dar es Salaam, maandamano hayo hayatahusisha kiongozi yeyote wa Serikali, chama cha siasa au wanaharakati, bali waandishi wa habari wenyewe viongozi wao.

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yamekamilika. Alisema yataanzia katika Viwanja vya Ghand Hall, kupitia Barabara za Uhuru, Mlango Mmoja, Nyerere na kuingia katika Barabara ya Miti Mirefu, Pamba, Barabara ya Kenyatta hadi Uwanja wa Nyamagana.

Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma, Habel Chidawali alisema, ofisi yake ilikuwa katika maandalizi ya kufanikisha maandamano hayo akisema kwamba hadi leo jioni watakuwa katika nafasi nzuri ya kutangaza njia watakazopitia na mahali yatakapoishia.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Christopher Nyenyembe alisema kwamba pia wako katika maandalizi ya kukamilisha maandamano hayo.
“Tunazo sababu za kuandamana kuungana na wenzetu nchi nzima, tulikwisha toa tamko letu kulaani mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kususia kuandika habari za polisi, lakini katika maandamano hayo tutatoa tena tamko,” alisema
Source: Mwananchi

Scolarship

VLIR-UOS Scholarships for Developing Countries

Saturday, September 8, 2012

SUMAYE AISHUKIA POLISI

ASEMA MATUMIZI YA SILAHA ZA MOTO HAYATATUI MIGOGORO, ASKARI WALIOKAMATWA IRINGA, KUFIKISHWA KORTINI JUMATATU

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha kutumia silaha za moto au nguvu ya ziada linapokabiliana na raia, badala yake litumie busara kutatua migogoro.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, baada ya kufunga mafunzo wa wahariri wa vyombo vya habari yaliyohusu utawala, Sumaye alisema kufa mtu katika mapambano ya polisi na raia siyo kitu kidogo.


Kauli hiyo ya Sumaye inaonekana kuwalenga polisi ambao wanadaiwa kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Televisheni ya Channel Ten mkoani Iringa, David Mwangosi.


Mwandishi huyo aliuawa Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Nyololo, Iringa kwa kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu, wakati polisi walipokuwa wakiwazuia viongozi na wanachama wa Chadema kukusanyika wakati wakifungua tawi la chama hicho kijijini hapo.


Mpaka sasa askari watano wa jeshi hilo, akiwamo anayetuhumiwa kumlipua kwa bomu marehemu Mwangosi, wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo mkoani Iringa.

 
Sumaye alisema kuwa katika siku za karibuni, polisi wamekuwa wakikimbizana na raia mara kwa mara pamoja na kutumia silaha na nguvu isiyo ya kawaida hata pale pasipostahili. Jambo ambalo alisema siyo sahihi kwa mustakabali wa jeshi hilo.

“Si lazima sana kwa polisi kutumia silaha hasa za moto kila wakati. Nimekuwa nikitazama kwenye televisheni mara kwa mara na kuona polisi wakitumia silaha, hata sehemu za kuvunja nyumba tu huko vijijini. Nawashauri watumie busara,” alisema Sumaye na kuongeza:

“Tusidhani risasi inaweza kutatua migogoro wakati wote. Risasi inaweza kuharibu kila kitu, zitumike pale inapokuwa ni lazima kwani Watanzania siku zote si watu wa fujo.”

Alisema kutokana na tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa mwandishi wa habari, Serikali, Polisi na vyombo vingine vya usalama, watakuwa wamejifunza kitu katika kutatua migogoro na migongano baina yao na wananchi wanaowaongoza.

Alisema kwamba Jeshi la Polisi nchini linapaswa kutambua kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi ikiwa ni pamoja na kutumia risasi kutawanya raia, si suluhisho la migogoro baina yake na wananchi, bali kinachohitajika ni busara zaidi, ili kuepusha maafa.

Akizungumzia suala la polisi kupambana na wanasiasa alisema, mazingira ya siasa kwa sasa yamechangamka zaidi ikilinganishwa na yale ya zamani na kwamba wakati mwingine wanasiasa wamekuwa wakichangia vurugu na hivyo kulilazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu ya ziada.

“Sisi wanasiasa tusiwe kichocheo cha kuleta vurugu na badala yake tutumie njia za kistaarabu na si kuchokoza vyombo vya usalama. Kinachotakiwa busara zitumike pande zote, vinginevyo tutaendelea kuumiza watu,” alisema.

Kuhusu uhusiano baina ya Serikali na waandishi wa habari, Sumaye alisema kinachoathiri hali hiyo katika nchi za Afrika ni kutokana na baadhi ya Serikali kutotaka mambo yake yawe wazi. Alisema katika mazingira mengi hata pale unapokuwapo uhusiano huo unakuwa wa kinafiki usioleta tija kwa pande zote.

Alisema iwe ni polisi na wananchi au polisi na waandishi, busara zitumike zaidi badala ya nguvu katika kutafuta suluhisho kwani siku zote mapambano hayatatui na badala yake, yanaweza kuharibu kabisa amani iliyopo.

Akifunga mafunzo hayo ya siku nne yaliyohusu utawala, Sumaye alisema vyombo vya habari ni sehemu ya maisha ya kila siku katika jamii kwa kuwa vina habarisha mambo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Alisema vinatoa taarifa ya nini Serikali zinawafanyia watu wake na nini hazifanyi ili wananchi waweze kudai haki zao na hata kuikumbusha wajibu wake pale inapojisahau. Muda mwingine vyombo vya habari vimekuwa kisu kikali kwa sababu si Serikali zote zinazopenda kukosolewa, kukumbushwa na kupewa changamoto kwa yale zilizoyafanya na zinayopaswa kuwafanyia wananchi wake.

“Vyombo vya habari ni kama kioo tunachojitazama kila asubuhi kabla kutoka nyumbani kwenda ofisini au kuhudhuria mikutano muhimu, ili kujua kama umevaa uhusika wa kile unachokwenda kukifanya au kukizungumza mbele ya jamii. Huwezi kuvunja kioo kama kitakuonyesha kitu ambacho huhitaji kukiona kwenye mwonekano wako.

Hivyo si sahihi kuvilaumu au kuviadhibu vyombo vya habari pale vinapokosoa na badala yake ni kujirekebisha,” alisema Sumaye.

Watuhumiwa wa mauaji ya IringaKatika hatua nyingine askari watano wanaoshikiliwa Iringa wanaendelea kuhojiwa, huku taarifa zikieleza kuwa wanaweza kufikishwa mahakamani Jumatatu, kutokana na kushindikana jana.

Jana, taarifa zilisambaa kwamba askari hao walikuwa wafikishwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, lakini hadi jioni, walikuwa hawajafikishwa. Pia hakukuwa na taarifa zozote za nini kilikuwa kinaendelea.

“Ni kweli walitakiwa wafikishwe leo, lakini hadi sasa hawajafika, wakifika nitawaeleza,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa mahakama hiyo jana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda hakutaka kueleza lini watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kile alichosema kwamba kwa sasa yeye siyo msemaji wa jambo hilo.

“Hapa alikuja IGP (Said Mwema), na sasa yuko DCI (Robert Manumba). Kwa mazingira haya uhuru wangu wa kuzungumza uko limited, (una kikomo),” alisema.

Alipoulizwa watuhumiwa hao wako mahabusu ipi, alihoji... “Wapi?” Aliendelea kusema, “Nashindwa kusema wapo au hawapo kwa kuwa mimi siyo msemaji wa jambo hilo, ila nawashauri m-cross-check (kuthibitisha), vizuri vyanzo vyenu vya habari.”

belgium scholarship

Belgium scholarship

Thursday, September 6, 2012

Mwanablogger akimbia mkoa kuhofia Maisha yake


Francis Godwin akitoka kituo cha Polisi alikojisalimisha

Francis Godwin ambaye aliripoti tukio la mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi ameandika haya kwenye blog yake;

Maisha ni safari ndefu yenye misukosuko mingi ila katika maisha ukichagua kuwa mkweli kifo kwako ni rafiki wa karibu sana.

Daudi Mwangosi ameuwawa kwa kusimamia ukweli na kutimiza wajibu wake kama mwanahabari ,leo mimi nalazimika kukimbia mkoa wangu wa Iringa ambao nilitokea kuupenda zaidi kutokana na kusimamia ukweli juu ya kifo cha mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ,pia kama shemeji yangu na tatu kama mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge .

Ila cha kushangaza mbali ya kuwa mimi si muuaji wa Daudi Mwangosi jeshi la polisi wameanza kuniwinda mimi kama shuhuda wa tukio badala ya kuwasaka wauwaji kweli inanishangaza sana ila ndio Tanzania yetu .

Hivyo kutokana na kuendelea kufuatwa fuatwa usiku na mchana binafsi nimechangua kuwa mkimbizi katika mkoa wangu huku nikisimamia ukweli ule ambao ninao na kamwe sitakubali kusema uongo kwa kile nilichokiona nawapenda sana wana Iringa na kuamua kuukimbia mkoa si kwa ajili ya kuwakimbia wakazi wa mkoa wangu nimeamua kwenda mafichoni kwa muda ili kupisha wenye roho mbaya kutaka kunitoa uhai wangu kabla ya kutoa ushahidi wangu.

Iwapo nitapata nafasi zaidi nitaanika kila kitu hapa ili kukuwezesha wewe mdau kujua kilichotokea hadi leo kukimbia mkoa.

Maiti saba zapatikana, Ni wale waliofunikwa na kifusi mgodini Ruangwa


Zoezi la kufukua Maiti za watu waliofunikwa na kifusi katika Machimbo ya Madini katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi jana limekamilika leo asubuhi huku wakifanikiwa kuzipata maiti zote 7.Akiongea na mtandao huu (Michuzi blog),Diwani wa Kata hiyo, Andrew Chikongwe alibainisha kuwa kazi ya kufukua kifusi hicho imechukua muda mrefu kufuatia na kuwepo kwa zana duni za kufukua Mchanga hali iliyofanya kazi hiyo kuwa Ngumu kuanzia jana saa 9 jioni hadi leo asubuhi.

Source:Michuzi blog

Kautundu kazuri Google......try


Ingia hapa Google gravity


.maneno yote na picha zitavutwa chini aka gravity


2. ukisearch matokeo nayo yanadondoka

3. pia unaweza kudrag na kurusha anything

Siri mauaji Iringa zaanza kufichuka

POLISI WALIOTEKELEZA OPERESHENI WADAIWA KUSAFIRISHWA KUTOKA MIKOA MINGINE, WAANDISHI WA HABARI IRINGA WASUSIA MKUTANO WA DCI MANUMBA

Waandishi wetu, Dar, mikoani
INADAIWA kwamba askari waliokuwa katika operesheni ya kuzuia mkutano wa Chadema katika eneo la Nyololo wilayani Mufindi, Iringa na ambayo ilisababisha kifo cha Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi walitolewa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Mbeya.

Tayari tukio hilo limeibua mjadala mzito kiasi cha kumfanya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kuunda tume huru kubaini chanzo cha tukio hilo. Marehemu Mwangosi alizikwa juzi nyumbani kwao Tukuyu, mkoani Mbeya.
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kuwa polisi hao kutoka mikoa hiyo mitatu wakiwa wamesheheni vifaa mbalimbali likiwamo gari la maji ya kuwasha, walisafiri siku moja kabla ya mkutano huo wa Chadema na baadaye kuzuka vurugu zilizosababisha kifo hicho.
Marehemu Mwangosi aliuawa kwa mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu ambao ulisambaratisha vibaya sehemu kubwa ya mwili wake.

Chanzo cha habari kutoka mkoani Dodoma kilisema: “Hapa kwetu kuna askari 10 na tunawafahamu kwa majina. Waliondoka hapa siku moja kabla ya tukio hilo wakiwa na gari la washawasha.”
Chanzo hicho kilisema kwamba awali, hawakuwa wakifahamu kama baadhi ya wenzao walichukuliwa na kupelekwa Iringa. “Tulikuja kuona kwenye gazeti picha na tulipofuatilia tukaelezwa kuwa ni kweli Dodoma ilitoa askari kwenda Iringa.”

Askari mwingine aliyekuwa katika operesheni hiyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kitaaluma, alikiri kuwa hadi jana baadhi yao walikuwa bado wako Iringa na kwamba walikwenda kwa agizo la wakubwa wake wa kazi.
“Sisi ni Watanzania, lakini tumelazimika kuyafanya hayo kwa sababu ya mkate (malipo). Kwa kweli haikuwa haki, kuwatoa askari na silaha kutoka mikoa mitatu kana kwamba wanakwenda kupigana vita!”

Alidokeza kwamba, askari wote waliotoka Dodoma walikuwa njiani kurudi mkoani humo, jana lakini gari la maji ya kuwasha liliendelea kubaki huko Iringa likiwa na dereva wake na askari mmoja mwenye cheo cha inspekta. Askari huyo alisema kwamba gari hilo lililazimika kubaki kutokana na hitilafu.

“Wengine wamerudi lakini, kuna wengine wenye gari la kuwasha bado walikuwa Iringa, gari lao limepata hitilafu kidogo,” kilisema chanzo hicho kutoka mjini Dodoma.
Mmoja wa askari hao alidaiwa kwamba hiyo inaweza kuwa moja ya sababu ya askari hao kumshambulia marehemu Mwangosi wakati mwenzao anayemfahamu akijaribu kuwazuia. "Hii inaonyesha kuwa askari hao waliompiga walikuwa hawamjui na huyu aliyekuwa akiwazuia, alimjua.”

Makamanda watupiana mpira
Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen hakukubali wala kukanusha na badala yake alisema: “Mambo yote hayo yanatakiwa kujibiwa na Kamanda wa Iringa.”
Aidha, alisema sakata la kifo cha mwandishi huyo kwa sasa liko katika vyombo vya uchunguzi hivyo asingekuwa tayari kulizungumzia.

“Siwezi kusema kama askari wangu walikwenda huko au hawakwenda, isipokuwa ninachoweza kusema ni kwamba suala hilo lipo katika vyombo husika hivyo waachiwe wao au Kamanda wa Iringa ndiye mwenye majibu.”
Alipotajiwa jina la mmoja wa askari aliyeonekana katika picha za video na magazeti za tukio hilo kwamba anatokea katika moja ya vituo vyake, kamanda huyo alisema: “Mimi yakitokea Dodoma nitazungumza wala siyo mtu mwingine kwa hiyo, mambo ya Iringa siwezi kuyazungumza na kama tutaanza kila Kamanda kuzungumza jambo hilo hamuoni kuwa itakuwa ni kama vurugu?”
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alipopigiwa simu yake iliita tu bila kupokewa.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alisema kwa kuwa tukio hilo limefanywa na polisi, mambo mengi yatazungumzwa lakini akasisitiza kwamba hajapeleka askari Iringa.
Alisema hakukuwa na agizo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wala ombi kutoka Polisi Iringa kutaka askari wa kuongeza nguvu... “Taarifa hizo ni za uzushi kwani hazina ukweli wowote.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani alikanusha pia kuwapeleka askari wake Iringa akisema: “Hizo taarifa siyo za kweli. Hakuna askari yeyote aliyekwenda Iringa wakati wa vurugu zile.”

Mkutano wa DCI wavunjika
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema: “Hayo yote yameundiwa tume ngoja tuiachie ifanye kazi yake.”
Awali, DCI Manumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari mkoani Iringa, ambao hata hivyo, ulivunjika baada ya kutokea kutoelewana baina yao.

Manumba alitaka kueleza ripoti ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, lakini waandishi hao walikataa kumsikiliza wakisema hawauamini uchunguzi huo kwa kuwa ulifanywa na polisi peke yao.

Kabla Manumba, hajaanza kuzungumza, Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Iringa (IPC), Frank Leonard alisema kutokana na msimamo wa waandishi wa habari wa mkoa huo hakutakuwa na uhusiano wa kikazi na polisi hadi pale tume zilizoundwa kuchunguza kifo hicho zitakapotoa taarifa sahihi juu ya mauaji hayo.

“Msimamo wetu ni kusitisha uhusiano wa kikazi baina yetu na jeshi la polisi hususan Mkoa wa Iringa, tumekuja hapa kwa sababu DCI umetuita na kama unataka kutupa taarifa ya kifo cha ndugu yetu basi waambie hao maofisa wa jeshi wa Iringa watoke nje,” alisema Leonard.

Akijibu madai hayo Manumba alisema: “Nia yangu ni kutoa taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, ndiyo maana niliwasiliana na mwenzenu ili tuweze kuzungumza, Polisi Iringa wataendelea kuwepo na waandishi wa habari mtaendelea kuwepo, matukio kama haya yapo na yataendelea kuwepo.”
Licha ya maelezo hayo, hakuna mwafaka uliofikiwa na mkutano huo ukavunjika.
Akizungumza kwa simu na gazeti hili baadaye, DCI Manumba alisema: "Ni vyema wao wangenisikiliza kujua ninataka kuwaambia nini. Lakini, kwa kuwa kuna mkanganyiko, nimeona ni vyema jambo hili lisubiri tume ndipo watakuja kulizungumza.”

Waikataa Tume ya NchimbiChama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeiponda tume ya Dk Nchimbi kikieleza kuwa imeundwa ili kurudisha uhusiano kati ya Polisi na waandishi wa habari na si kutafuta chanzo cha tatizo.

Juzi, Dk Nchimbi alitangaza kamati ya kuchunguza mauaji hayo inayoongozwa na Jaji Mstaafu, Steven Ihema na wajumbe, Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga, Mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, Mtaalamu wa milipuko kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Wema Wapo na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu.
Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu alisema Dar es Salaam jana kwamba: “Hii si tume ya kuchunguza mauaji, bali ina lengo la kurudisha uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari ili kuwasahaulisha wananchi kwa sababu imeundwa na waziri ambaye naye anatakiwa kuhojiwa.” “Tunamwomba Rais Jakaya Kikwete ateue tume kama anavyoelekezwa na Sheria ya Tume za Uchunguzi ya mwaka 1992, ambayo inaruhusu kumhoji yeyote kasoro yeye Rais.”
Lissu alisema Rais Kikwete angeunda tume hiyo na Waziri Nchimbi na IGP Said Mwema wanatakiwa kujiuzulu ili kupisha uchunguzi akidai kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba walitoa amri ya mauaji hayo.
“Dk Nchimbi anatakiwa kumuiga Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye alijiuzulu akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kutokea mauaji, akijiuzulu atajijengea heshima tofauti na sasa kwani wananchi wamesikitishwa na mauaji hayo,” alisema Lissu.
Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando alidai kwamba kuna mkakati uliowekwa na Serikali wa kukidhoofisha Chadema baada ya kuonekana kwamba ni tishio kwa CCM.
Mbali na Chadema, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), pia limesema halina imani na kamati hiyo likisema imekuwa kawaida kwa Serikali kuunda tume ambazo hazileti ripoti kwa wananchi.
“Tume zimekuwa zikiundwa bila faida yoyote, huku zikipewa muda kuchunguza yaliyotokea lakini matokeo yake huwa hakuna ripoti wanayorudisha,” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya.
Kaaya alisema tume zimekuwa zikiundwa na kuigharimu Serikali fedha nyingi za walipa kodi, lakini ripoti zake zinaendelea kuwa siri.

Imeandikwa na Habiel Chidawali, Dodoma, Hamida Sharrif Morogoro, na Tumaini Msowoya, Iringa na
Lasteck Alfred na Juliana Malondo
Source:Mwananchi

Tendwa atamani kuifuta CHADEMA


Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

 
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Monday, September 3, 2012

Mwandishi wa Channel Ten auawa katika mvutano kati ya CHADEMA na Polisi

Daudi Mwangosi
Hii hapa ni taarifa kutoka kwa Francis Godwin,


Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo



Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .



Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.



Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .



Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .



Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.



Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari



JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.



Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.



Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.



" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza



Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.



"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.



Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.



Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.

Majibu ya Dkt Slaa

Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .



Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.



"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.



Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .  
Chanzo: Francisgodwinblog ( Iringa)

Sunday, September 2, 2012

Mechi za jumapili.......


 PROBABLE LINE-UPS

BARCELONA
Valdes,Montoya, Pique, Mascherano, Alba,Xavi, Busquets, Iniesta,Tello, Messi, Sanchez

VALENCIA
Alves,Pereira, Rami, Ruiz, Mathieu ,Albelda, T Costa,Feghouli, Jonas, Guardado,Soldado

Barcelona captain Carles Puyol remains doubtful for Sunday's Primera Division encounter against Valencia with a cheekbone injury.

The Catalans, who will have coach Tito Vilanova barred from the dugout, could also be without right-back Dani Alves, after the Brazilian picked up a knock prior to Wednesday's Supercopa defeat at Real Madrid.

However, young midfielder Thiago has finally overcome a tibia injury that kept him out of the Olympics and is fit to play.

Valencia summer signing Fernando Gago faces a late fitness test, so David Albelda may make his first appearance of the season.

Also set for a start is French defender Adil Rami, who will deputise for the suspended Ricardo Costa.



PROBABLE LINE-UPS
LIVERPOOL
Reina,Johnson, Skrtel, Agger, Enrique,Sahin, Gerrard, Allen ,Downing, Suarez, Sterling

ARSENAL
Mannone,Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs,Cazorla, Arteta, Diaby,Gervinho, Giroud, Podolski

Nuri Sahin is set to make his Liverpool debut in the heart of midfield after Lucas (thigh) was ruled out for up to three months after hobbling off in the opening stages of the 2-2 draw with Manchester City.

Daniel Agger is likely to return from suspension to replace Sebastian Coates in defence but youngster Raheem Sterling is poised to make another start having impressed against Roberto Mancini's side last time out.

For Arsenal, Vito Mannone could continue to deputise in goal with Wojciech Szczesny and Lukas Fabianski both still struggling for match fitness.

Bacary Sagna's long-term leg injury means Carl Jenkinson will again step in at right-back, with the France defender set to return to training after the upcoming international break. Fellow international team-mate Laurent Koscielny (calf) faces a late fitness test.

The continuing transfer speculation surrounding Theo Walcott could mean that Gervinho will again feature from the start, in support of Olivier Giroud and Lukas Podolski, while Alex Oxlaide-Chamberlain should appear from the bench.

Jack Wilshere (ankle), Emmanuel Frimpong (knee) and Tomas Rosicky (thigh) all remain long-term absentees.

 

PROBABLE LINE-UPS


SOUTHAMPTON Davis,Clyne, Hooiveld, Fonte, Fox,Davis, Schneiderlin, Lallana,Rodriguez, Lambert, Lee

MANCHESTER UNITED
De Gea,Rafael, Evans, Vidic, Evra,Cleverley, Carrick,Valencia, Kagawa, Nani,Van Persie

Southampton could well revert to the 4-3-3 system which served them so well against champions Manchester City on the opening day, with Championship Player of the Year Rickie Lambert expected to lead the line supported by Jay Rodriguez and Tadanari Lee out wide.

Guly Do Prado is expected to be left out of the squad following his off-the-field indiscretions, while new signings Maya Yoshida and Gaston Ramirez are unlikely to start, but could well feature in the Saints squad.

Manchester United are expected to name the same side which beat Fulham 3-2 last Saturday. Jonny Evans made a full comeback in the reserves mid-week but is unlikely to be fit enough to return to first-team duties, meaning Michael Carrick will continue alongside Nemanja Vidic at centre-back.

With Wayne Rooney sidelined for the next month, Robin van Persie will almost certainly start at the head of a four-pronged forward line, with Antonio Valencia, Ashley Young and Shinji Kagawa forming the attacking fulcrum of the midfield.

Source: Goal.com

Saturday, September 1, 2012

Mechi za leo....

MANCHESTER CITY

Hart
Zabaleta, Lescott, Kompany, Clichy
Nasri, Yaya Toure, Milner, Silva Balotelli, Tevez

QPR

GreenFabio, Ferdinand, Onuoha, Traore
Taarabt, Diakite, Granero, Park, Hoilett
Cisse


Manchester City boss Roberto Mancini will once again be without Sergio Aguero (knee) after his injury in the opening game of the season, so Mario Balotelli is expected to feature in his absence.
Meanwhile, Micah Richards (foot) also remains sidelined but we could see Joleon Lescott back in the side after he sat out City's draw against Liverpool.

With Gareth Barry also set to miss out again (hernia), James Milner and Jack Rodwell are vying to partner Yaya Toure in the centre of City's midfield.

Mark Hughes has no injury concerns heading to the Etihad Stadium.
Bobby Zamora is expected to overcome a head injury to partner Djibril Cisse up front, with former Inter goalkeeper Julio Cesar being handed QPR debut after completing his move earlier in the week.
Fellow new signing Estaban Granero could also be handed a starting berth after arriving from Real Madrid on Thursday, with Mark Hughes revealing he has received international clearance for the player to take part in Manchester.





TOTTENHAM

Friedel
Walker, Gallas, Vertonghen, Assou-Ekotto Sandro, Dembele Lennon, Sigurdsson, Bale
Adebayor
NORWICH

RuddyMartin, Barnett, Bassong, Garrido
Snodgrass, Howson, Johnson, Pilkington
Hoolahan
Holt

Younes Kaboul faces up to four months on the sidelines after undergoing surgery on a knee injury sustained at the end of last season, so William Gallas and Jan Vertonghen are likely to continue their partnership in defence.
New signing Mousa Dembele could start in place of Jake Livermore in central midfield, while Scott Parker (Achilles) is still a couple of weeks away from a return to training. Giovani dos Santos (calf) remains unavailable.

Emmanuel Adebayor looks set to make his first start for Tottenham since returning to the club, and Gylfi Sigurdsson may be selected ahead of Rafael van der Vaart, with the Dutchman flirting with a return to Hamburg.

Chris Hughton rested a number of key players for the Canaries’ clash with Scunthorpe United in the League Cup on Tuesday night, while Elliot Ward (ankle), Steven Whittaker (ankle) and Elliot Bennett (knee) are all doubts.

Wes Hoolahan could be handed his first start in the league this season behind Grant Holt, though a spot on the bench will have to suffice for new signing Mark Bunn.

Sebastien Bassong should start in central defence for Norwich, marking an almost immediate return to the club he left just weeks ago. Leon Barnett is likely partner the Cameroonian, with Michael Turner on the bench.





Source: Goal.com