Pages

Thursday, February 21, 2013

Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

 
Nilitaka kuandika makala ndefu lakini nimeona niende moja kwa moja na kusema ombi/pendekezo langu kama litampendeza Rais Kikwete.

KWA KUWA, matokeo ya kidato cha nne ambayo yametoka hivi karibuni yameonesha kufeli kwa kutisha kwa watoto wetu katika mtihani wao;

KWA KUWA
, kufeli huko kuna matokeo ya moja kwa moja katika maisha ya wanafunzi hawa, familia zao na kwa taifa kwa u jumla;

KWA KUWA
, matokeo hayo ni hasara kubwa kwa wazazi waliowekeza kwa miaka minne ya elimu ya watoto hawa na kwa taifa katika kuwekeza vifaa, walimu na miundo mbalimbali;

KWA KUWA, kuacha kundi kubwa la watoto hawa kurudi katika maisha ya uraiani kutaongeza jamii ya watu ambao hawana elimu ya kutosha na wasioweza kuajiriwa hata katika mifumo isiyo rasmi (pamoja na kushindwa kujiajiri wenyewe);

KWA KUWA, kufeli kwa watoto hawa ninaamini siyo kosa lao peke yao bali pia ni kosa la utawala na uongozi wetu, wazazi na jamii kwa ujumla;

NINAAMINI KUWA, kutokuchukua uamuzi wa makusudi na wa lazima kuwasaidia watoto hawa kuwapa nafasi nyingine ni kuwahukumu katika maisha duni na kuwanyima kimsingi nafasi ya kuinuka wakati tayari wameshaanguka

NINAAMINI KUWA, matokeo haya ni dhambi na aibu ya taifa letu hasa katika nchi ambayo inajivunia kuwa ina 'shule nyingi, vyuo vingi, walimu wengi, na teknolojia ya kisasa katika elimu;

NINAAMINI KUWA, Ni jukumu la uongozi wa kisiasa wa taifa kuchukua hatua za haraka na za lazima kuwapa nafasi nyingine watoto hawa kuweza kutengeneza waliposhindwa.

NINAAMINI KUWA, Taifa lina deni kwa watoto hawa, lina deni kwa historia, lina deni kwa familia zao na kwa hakika kabisa lina deni kwa maisha ya watoto hawa. Deni hili tusiliache likue lije kushindwa kulipika. Naamini tunaweza kulilipa kabla halijaanza kuwa na riba isiyokamatika!

Kutokana na mambo yote hayo juu na mengine ambayo nimeyaadhania, ninaamini Utawala wa Rais Kikwete unaitwa na historia, unadaiwa na haki, na unalazimishwa na wajibu kuwapa watoto hawa nafasi nyingine ya kurudia mitihani ya kidato cha nne ili kuweza kuinua alama zao za kufaulu, kusahihisha makosa yao na kuwapa nafasi ya kuweza kuendelea na elimu ya kidato cha tano na cha sita. Kutokana na hili:

HIVYO BASI, Baraza la Mawaziri lifanye kikao cha dharura kuhusiana na matokeo haya ya mitihani ambapo uamuzi wa kutengua matokeo yote ya mtihani uchukuliwe na kuyafuta kabisa matokeo hayo;

NA HIVYO BASI
, Baada ya kufuta matokeo hayo serikali iamue kuwa watoto wote waliofanya mtihani huu uliopita watarudia mitihani yote ya kidato cha nne ndani ya mwaka mmoja pamoja na watoto watakaokaa katika mtihani wa mwaka huu au katika mtihani mwingine tofauti

NA HIVYO BASI
, Watoto wote ambao katika mtihani huu wamepata daraja la I na II watakuwa na uhuru wa ama kurudia mtihani wao ili kuthibitisha kufaulu kwao au kuendelea na matokeo waliyonayo. Wakiamua kurudia basi kama watafaulu alama za juu zaidi ya sasa watashika alama hizo kama watapata alama za chini watashika alama zao za sasa;

NA HIVYO BASI
, Wanafunzi waliopata daraja III na 0 nao itakuwa hivyo hivyo, watapewa nafasi moja ya kurudia mitihani yote kuiinua viwango vyao na wale watakaopata viwango vya juu kuliko vya sasa basi watasika viwango hivyo na wale ambao watapata viwango vya chini kuliko sasa watashika viwango vya sasa.

NA HIVYO BASI, Wanafunzi ambao sasa wamepata daraja la III na 0 endapo watarudia mitihani ijayo na wakainua viwango vyao na kuwa kati ya daraja la I na II basi SERIKALI itawapa nafasi ya kusoma bore kidato cha tano na cha sita katika shule za Sekondari za Serikali. Hii iwe 'AHADI YA TAIFA' (National Promise)

NA HIVYO BASI, ili kutoa motisha kwa shule na walimu ambao wanawafundisha wanafunzi hawa na wengine basi serikali ianze kutoa motisha kwa shule zote (zenye watahiniwa wengi) ambazo zitafaulisha watoto wengi kwenye madaraja ya I na II. Motisha huu utakuwa kwa shule na kwa jopo la walimu wa kidato cha nne.

- Shule ambayo haitatoa daraja 0 kuanzia sasa itapata zawadi ya shilingi milioni 50 kwa matumizi ya sule
- Shule ambayo haitatoa daraja IV kuanzia sasa itapata zawadi ya silingi milioni 75 kwa matumizi yake
- Walimu wanaofundisha shule hizo zikiwa na matokeo hayo watagawana zawadi ya nusu ya tuzo hizo (Milioni 25 kama hakuna 0, milioni 37.5 kama hakuna daraja la IV)

Tuzo hizo zinaweza kurudiwa kila mwaka endapo viwango hivyo vitaendelea.

NA HIVYO BASI, Mwalimu Mkuu wa shule ambazo zinafanya vibaya zaidi watafukuzwa kazi, Afisa Elimu wa Wilaya yenye shule nyingi zilizofanya vibaya nao watafukuzwa kazi.

NA HIVYO BASI, kuanzia sasa wanafunzi wote wanaopata daraja la IV na 0 watakuwa wanapata automatic resit ya mtihani katika mwaka unaofuatia. Na katika hili napendekeza wanafunzi wote waliopata madaraja hayo katika miaka mitano iliyopita na ambao wangependa kurudia mitihani wapewe nafasi hiyo na wao wakifaulu kama hapo juu serikali iwagharimie kidato cha TANO na cha SITA.

PAMOJA NA HAYO, Baraza la Mawaziri liangalie kwa kina haja ya kuufumua mfumo wetu wa elimu kukidhi changamoto ambazo tumeziona sasa. Baadhi ya mabadiliko hayo:

- Kuondoa Elimu kutoka kuwa suala la mfumo wa kitaifa (decentralization of the education system)
- Kuweka miaka mitatu ya kwanza ya elimu kuwa ni ya lazima katika 3R (Hisabati, Kuandika, na Kusoma)
- Kuweka mwaka wa kwanza kwenye O'Level kuwa Wa Kiingereza na Hisabati na Lugha (Pre-Secondary) - miaka mitatu ya mwiso kufanya elimu ya O'level
- Serikali ikutanishe wadau wa elimu kutoka Shule zinazofanya vizuri zaidi kushirikisha mawazo yao na wadau wa shule nyingine (KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU ELIMU - NATIONAL EDUCATION REFORM CONFERENCE)
- Makampuni na taasisi binafsi na za umma zitakiwe kuadopt shule za msingi na za sekondari na yashiriki katika uendeshaji na uboreshaji wake. Mtindo wa sasa wa makampuni makubwa kutoa madawati, mabati halafu wanakimbia haujasaidia kuinua elimu; makampuni yahamasishwe (ikiwemo motisha wa aina fulani katika kodi -tax incentive) kulea shule za sekondari. Tax breaks makampuni yatapata endapo shule wanazozilea hazitakuwa na madaraja ya IV na 0


* Kwa kweli nimeandika kwa haraka bila kufikiria mengi zaidi na implication yake na hivyo ni mchango wangu kidogo tu wa mawazo ya nini tufanye sasa hivi na baadaye. NIna uhakika watu wengine wana mawazo bora zaidi. Jambo moja ambalo hatupaswi kukubali na kuliachilia ni matokeo haya kusimama. Ni LAZIMA yatenguliwe kama tunaamini katika utu, usawa na haki kwa watoto wetu.
 
Source :MMM - BGM

Tuesday, February 19, 2013

Asilimia 60 chali matokeo ya kidato cha nne

 
MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.

Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
 
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.

Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.
 
Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.

Ufaulu kwa madaraja
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.
 
Waliopata daraja la tatu ni 15,426, wavulana 10,813 na wasichana 4,613, waliopata wa daraja la nne 103,327, wavulana 64,344 na wasichana 38,983 huku waliopata sifuri wakiwa 240,903, wavulana 120,664 na wasichana 120,239.
 
Shule 20 bora
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wizara ilitaja shule 20 zilizofanya vizuri badala ya 10 kama ilivyozoeleka, kati yake 18 zilikuwa za watu binafsi na mashirika ya dini na mbili za Serikali.

Shule hizo ni pamoja na St.Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Boys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Rosmini ya Tanga, Canossa ya Dar es Salaam, Jude Moshono ya Arusha, St. Mar’s Mazinde Juu ya Tanga, Anwarite Girls ya Kilimanjaro na Kifungilo Girls ya Tanga.
 
Nyingine ni Feza Girls ya Dar es Salaam, Kandoro Sayansi Girls ya Kilimanjaro, Don Bosco Seminary ya Iringa, St. Joseph Millenium ya Dar es Salaam, St. Iterambogo ya Kigoma, St. James Seminary ya Kilimanjaro, Mzumbe ya Morogoro, Kibaha ya Pwani, Nyegezi Seminary ya Mwanza na Tengeru Boys ya Arusha.
Shule 10 za Mwisho
Kwa upande wa shule 10 za mwisho, iliyofanya vibaya zaidi ni Mibuyuni ya Lindi, Ndame ya Unguja, Namndimkongo ya Pwani, Chitekete ya Mtwara, Maendeleo ya Dar es Salaam, Kwamndolwa Tanga, Ungulu Morogoro, Kikale ya Pwani, Mkumba na Tongoni za Tanga.

Matokeo yaliyofutwa
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu na kuandika matusi.
 
Baadhi ya udanganyifu huo ni karatasi za majibu kuwa na mfanano usio wa kawaida, kukamatwa na simu za mkononi kwenye chumba cha mtihani, kukutwa na karatasi au madaftari pamoja na kubadilishana karatasi za majibu.

Dk Kawambwa alisema matokeo ya watahiniwa 28,582 yamezuiwa kwa sababu ya kutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja.
 
Matokeo ya QT
Dk Kawambwa alisema waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) walikuwa 21,310, wasichana 13,134 na wavulana 8,176 na waliofanya ni 17,137 sawa na asilimia 80.42... “Watahiniwa 5,984 kati ya 17,132 waliofanya mtihani huo wamefaulu
 
Waziri akwepa
Kabla ya kutangaza matokeo hayo, Waziri Kawambwa alitumia muda mwingi kuzungumza sababu za yeye mwenyewe kuamua kutangaza matokeo hayo badala ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mirihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako kama ilivyozoeleka
 
“Najua kila mtu ana shauku ya kusikia matokeo leo, naona mkimwangalia Katibu (Dk Ndalichako) hapa, lakini mimi kwa kujua jambo hili, nimeona kwa nini nimbebeshe jukumu hilo zito wakati waziri mwenyewe mwenye dhamana hiyo nipo! Ndiyo nimekuja niwape matokeo haya,” alisema Dk Kawambwa
 
Baadaye Dk Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na haraka hivyo asingekuwa na muda wa kujibu maswali, huku akitumia muda mwingi kuzungumza mambo yaliyokuwa nje ya matokeo aliyotarajiwa kuyasoma.
 
Pia alikwepa kujibu maswali ya msingi likiwamo kutaja majina ya wanafunzi bora pamoja na majina ya shule 10 bora zenye wanafunzi chini ya 40 akisema anajua umuhimu wa kueleza mambo hayo, lakini wataalamu wake wamekwepa kuandika kila kitu katika taarifa hiyo kwa kile alichoeleza kukwepa kuwa na taarifa ndefu. Taarifa iliyosomwa na waziri kwa waandishi ilikuwa na karatasi nne.
 
Ufaulu mwaka 2011
Kwa mujibu wa matokeo ya mwaka 2011, ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule ulionyesha kuwa watahiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 walifaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu. Wasichana waliofaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 10,313 sawa na asilimia 7.13 na wavulana 23,267, sawa na asilimia 12.13.
 
Waliopata daraja la nne mwaka huo walikuwa 146,639 sawa na asilimia 43.60. Wavulana 87,039 sawa na asilimia 45.40 na wasichana 59,600, sawa na asilimia 41.22 huku waliofeli wakiwa 156,089 sawa na asilimia 46.41, kati yao wavulana wakiwa 81,418 sawa na asilimia 42.47 na wasichana 74,667, sawa na asilimia 51.64.
Source: Mwananchi

Sunday, February 17, 2013

Vita ya Lissu, Ndugai yakolea


 
MOTO wa kuwashtaki kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai uliowashwa na Chadema, jijini Dar es Salaam Februari 10 mwaka huu, unaendelea huku chama hicho kikieleza kuwa kitawabana viongozi hao hadi wajiuzulu.

Mbali na hilo, chama hicho kimesema Bunge, halina uwezo wa kuanzisha chombo cha habari kitakachokuwa chanzo cha habari kwa vyombo vingine vya habari.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema kwamba Spika wa Bunge naye hana uwezo wa kuunda Kamati za Bunge na kwamba wanachokifanya viongozi hao ni kudhoofisha mamlaka ya mhimili huo wa taifa.

Katika mkakati wa kumbana Spika na naibu wake ili wajiuzulu, Dk Slaa alisisitiza kuwa watatumia nguvu ya umma pamoja na mikutano inayoendelea nchi nzima ili kuwashtaki na mikutano hiyo inaanzia mkoani Arusha.

“Tunaanzia Arusha mjini na mkutano wetu utafanyika kesho, atakuwepo Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama” alisema Dk Slaa na kuongeza:

“Kila kanda itakuwa na ratiba zake, lengo letu ni kufanya mikutano na kuwaeleza wananchi ukweli na tutakwenda hadi vijijini.”

Alisema mikutano hiyo kwa kila kanda inaweza kuchukua hadi mwezi mzima, huku akisisitiza kuwa kauli zinazotolewa na Makinda na Ndugai ni udikteta na kutaka kuirudisha Tanzania miaka 50 iliyopita.

Dk Slaa aliponda kitendo cha Makinda kuvunja baadhi ya Kamati za Bunge pamoja na Kashilillah kusema kwamba ofisi yake itazuia kuonyesha moja kwa moja vipindi vya Bunge, kabla ya juzi kuifuta kauli hiyo kwa maelezo kuwa sasa Bunge litaanzisha televisheni yake na vituo vingine vitakuwa vikichukua matangazo ya Bunge kupitia Televisheni hiyo.

“Anachokifanya Kashilillah ni kinyume na Katiba Ibara ya 18, Katibu wa Bunge. Hana uwezo wa kutoa tamko la kuzuia jambo fulani bila Bunge zima kuridhia mabadiliko hayo” alisema Dk Slaa na kuongeza;

“Hata Makinda naye hana mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge, kifupi ni kwamba wanachokifanya ni kinyume na Kanuni ya Bunge ya 151(1) na 152(2).”

Chadema ambacho ni chama kikuu cha upinzani, mara kwa mara kimekuwa kikilalamikia utendaji kazi wa Spika na naibu wake.

Wakati huohuo, mabishano ya kurushiana maneno ya kashfa, ubabe na kutupiana lawama juu ya matumizi ya Kanuni za Bunge, viliibuka juzi kati ya Naibu Spika, Job Ndugai na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu walipohamishia malumbano yao nje ya Bunge.

Ndugai na Lissu walipambanishwa katika Kipindi cha Kipima Joto kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV.

Mwongozaji wa kipindi hicho, Rainfred Masako, alila zimika kufanya kazi ya ziada ili kupunguza jazba za Ndugai na Lissu, ambao kila mmoja alikuwa akimtupia lawama mwe nzake kuhusu masuala ya Bunge.

Awali wakati kipindi hicho kilipoanza, Masako alisema kuwa amewaalika viongozi hao ili kuzungumzia kanuni mbalimbali za kuendesha shughuli za Bunge.

Wakiwa wenye ghadhabu na kurushiana maneno ya uhasama, kila mmoja alionekana kumpania mwenzake na mara kadhaa mwongozaji alilazimisha kuwarudisha kwenye mstari, baada ya wawili hao kutoka nje ya mada.

Akianza kumtuhumu mwe nzake, Lissu alisema: “Mimi sina tatizo na kanuni…nasema kwa kiasi kikubwa ziko sawa, lakini tatizo ni hawa wanaozitafsiri. Spika wa Bunge amekuwa akionyesha upendeleo kwa chama chake na kushindwa kuzitafsiri Kanuni za Bunge.”

Lissu alimtuhumu moja kwa moja Naibu Spika na Ndugai kuwa wameshindwa kuliongoza Bunge kwa kufuata kanuni na kwamba inavyoonyesha, wanafanya hivyo kwa kutokuelewa kanuni au kwa makusudi.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, alisema kuwa tangu kuanza kwa Bunge la 10, Spika Anne Makinda na Ndugai wamekuwa wakiendesha Bunge kwa ubabe na kukandamiza hoja za upinzani, bila sababu.

“Mimi ninachofahamu, Spika anatakiwa kuendesha Bunge kwa kufuata kanuni, haki bila chuki wala upendeleo,” alisema.

Alisema kuwa hadi sasa wa pinzani wamewasilisha rufani tisa mbele ya Kamati ya Kanuni za Bunge, lakini mpaka sasa ha zijafanyiwa kazi. Hata hivyo, Ndugai alimjibu akisema kuwa Bunge li naendeshwa kwa kanuni na kila kinacholalamikiwa na wapinzani walishirikishwa kikamilifu.

“Kinacholalamikiwa na watu ni utovu wa nidhamu wa baadhi ya wabunge ama kwa kuzikiuka kanuni au kufanya makusudi.

Kambi ya upinzani, inatumika kama wabunge wengine, kupa nga taratibu za mkutano na hata vikao bungeni. Hapa kuna Mnadhimu wa Serikali, kuna Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu,” alisema na kuongeza:

“Upande wa pili kuna Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, wote tunashirikiana na hawa ndiyo wanamshauri Spika kwa pamoja kama kuna jambo.”

Kauli hiyo ya Ndugai ilisababisha kuibuka kwa malumbano yaliyojaa jazba na vijembe kutoka katika pande zote mbili, huku Lissu akisisitiza kuwa pamoja na hayo, Spika anapindisha kanuni.

Sehemu ya malumbano yao yalikuwa hivi:

Lissu: Tatizo linaweza kuwa siyo Kanuni za Bunge, bali tatizo ni tafsiri ya kanuni mbele ya Spika, sijaelewa anafanya hivyo ama kwa kutokujua kanuni, au kufanya uamuzi kwa makusudi?

Ndugai: Kinacholalamikiwa na watu ni utovu wa nidhamu, kuna matumizi ya kanuni kama vile mwongozo, taarifa na kuhusu utaratibu, yaani vipengele hivi mbunge anaweza kuzungumza ovyo tu na Lissu ndiyo amekuwa kinara wa vurugu hizo.

Lissu: Ngoja nitoe mfano, Tangu kuanza kwa Bunge la 10, Spika Makinda na Naibu wake, tumeshawasilisha rufani tisa mbele ya Kamati ya Kanuni za Bunge, hoja binafsi kukandamizwa na uamuzi wa ubabe kwa wabunge wa kambi ya upinzani.

Ndugai: Kama kuna rufani hizo, taratibu zipo na zitafuatwa, ila mimi mpaka sasa sijapata nakala yoyote hata hiyo inayonitaka kujiuzulu. Lakini, mbona wewe Lissu tumekufikisha mbele ya Kamati ya Maadili na bado hujashughulikiwa?

Lissu: Unaona sasa, nikisema Spika hajui Kanuni za Bunge au anatumia makusudi naonekana mtovu wa nidhamu na hivi ndivyo siku zote Bunge linavyokuwa.

Ndugai: Tatizo ndiyo hilo kwa ndugu yangu, rafiki yangu Lissu, yaani anapenda kulaumu tu uongozi, staha ni pamoja na mavazi na mazungumzo, halafu hatua ya kutoa namba zetu za simu kule Mwembeyanga kwa kweli hayapendezi, labda aiombe radhi jamii.

Lissu: Hapa tuko kwenye mjadala wa Kanuni za Bunge, mambo ya Mwembeyanga si mahala pake, hilo pia ni tatizo ninalolifananisha na ukiukwaji wa kanuni. Nafikiri ingekuwa bora zaidi tukazingatia mjadala wetu.

Ndugai: Yaani ukashinikize kwa wananchi Mwembeyanga kuniondoa madarakani nisiseme, tatizo la Lissu ndiyo hilo tunatakiwa kuwa wavumilivu. Wenye mamlaka ya kuniondoa mimi ni wabunge, kama walivyonipatia nafasi hiyo.

Baada ya kuona malumbano yamezidi kuongezeka mwendeshaji kipindi alihamishia mjadala kwa watu wengine walioalikwa kwenye kipindi hicho hali iliyochangia kushusha jazba.

Ndugai apandisha munkari

Hata hivyo, katika mjadala huo, Ndugai alionekana kujaa hasira baada ya kubanwa maswali kutoka kwa wachangiaji wengine walioshiriki mjadala huo na wananchi waliokuwa wakipiga simu.

Washiriki wengine walikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiraia ya kufuatilia Mwenendo wa Bunge, Pakozi Azaniye na Mtafiti wa Masuala ya Haki za Binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pansience Mlowe.

Akichangia mjadala huo, Azaniye alisema: “Wakati mwingine tuliona Spika alipotafsiri Kanuni na mbunge akaitumia tafsiri hiyo kwa mbunge mwingine tofauti na kanuni ilivyo.

Akitoa taarifa za Bunge lililomalizika Azaniye alisema katika hoja binafsi 30 ni hoja 18 tu ndizo zimeshajadiliwa hatua iliyosababisha hasara ya kupotea kwa saa 12 na zaidi ya 300 milioni kujitokeza.

Hata hivyo, kila mmoja alipopewa nafasi ya kuaga, Lissu alitaka kuwepo utaratibu wa Bunge zima kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni, lakini Ndugai alitumia nafasi hiyo kumshambulia Lissu kwa utovu wa nidhamu na kulidhalilisha Bunge, kabla ya Masako kumkatiza akimtaka atumie nafasi hiyo kueleza mwenendo wa Bunge na utendaji wake.





source: mwananchi

Thursday, February 14, 2013

Tundu Lissu afichua ya Spika Makinda


 
  • Akiri kushiriki pamoja na akina Lukuvi
  • Akwepa kuzungumzia meseji za matusi
MNADHIMU Mkuu wa Kambi ya Upinzani Tundu Lissu amefichua mwenendo wa mjadala wa kikao kilichofikia uamuzi wa kufuta Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA).

Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) amezungumza na Raia Mwema kujibu madai kwamba yeye aliunga mkono hoja ya kufutwa kwa kamati hiyo wakati wa kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na alifanya hivyo kusimamia msimamo wa chama chake, unaodaiwa kuungwa mkono na baadhi ya viongozi wa juu, ikiaminika ilikuwa njia ya kuzidi kumdhibiti Zitto kisiasa.

Lakini ameyapingwa madai hayo akieleza mwenendo wa mjadala kuhusu hoja hiyo na kiwango cha upinzani alioonyesha.

Mbali na Lissu, kamati ambayo ilipitisha uamuzi huo inaundwa na Mbunge wa Mbulu (CHADEMA) Mustafa Akuunay; Mbunge wa Kibondo, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi); Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF); Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF); Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani (CCM); Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM). Vikao vya kamati hiyo vinaongozwa na Spika.

Maelezo ya Lissu
Mazungumzo kati ya Lissu na mwandishi wetu baada ya utambulisho na maelezo ya awali yalikuwa hivi;

Mwandishi: Ulishiriki katika kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na unadaiwa kuunga mkono hoja ya kuvunjwa kwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Ni kweli?

Lissu: Kweli nilishiriki, lakini sikuunga mkono hiyo hoja. Nilisema sababu za kuanzishwa kwa kamati hiyo bado hazijapitwa na wakati, tena zina uzito mkubwa zaidi kwa sasa.
Kisheria Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anatoa ripoti za ukaguzi tatu. Kwanza Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, pili; Hesabu za Mashirika ya Umma na tatu; Hesabu za Serikali za Mitaa. Si sahihi kuua kamati moja na kuacha nyingine mbili.

Mwandishi: Kama si sahihi ulikuwa na mapendekezo gani mbadala?

Lissu: Nilisema ni bora ziunganishwe kamati zote tatu au kuacha kama ilivyokuwa. Mapendelezo yalikataliwa...kama unavyojua wao wapo wengi kwa idadi kwa hiyo walipitisha uamuzi.

Mwandishi: Lakini wanasema lengo la kuunganisha kamati ni kutoa fursa kwa wizara na mashirika inayosimamia kuripoti sehemu moja. Kwa mfano, kabla ya kuvunja Waziri wa Nishati aliwajibika Kamati ya Hesabu Serikali Kuu na TANESCO, shirika lililo chini yake liliwajibika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Huoni kuna mantiki?

Lissu: Hiyo hoja haikuletwa kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge, imejitokeza huku mtaani. Lakini hata hivyo, haina nguvu kwa sababu kuna wizara nyingi ambazo zinawajibika katika kamati zaidi ya moja bungeni.

Mwandishi: Uamuzi gani zaidi wa kibunge mtakaochukua?

Lissu: Hakuna uamuzi zaidi kwa sababu rufaa zote za kibunge zinakatwa kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge na chombo hicho ndicho kimeamua kuvunja kamati hizo, hapa ni kuzidi kuchukua uamuzi wa kisiasa.

Meseji matusi kwa Spika
Kuhusu ujumbe mfupi wa simu ya mkononi uliotumwa kwa Spika Anna Makinda unaodaiwa kuwa wa matusi ya nguoni, kama ilivyopotiwa na baadhi ya magazeti jana Jumanne, Lissu alisema hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.

“Bado sijaonyeshwa hizo meseji zinazoitwa za matusi. Ningeonyeshwa ningeweza kutoa maoni yangu kwa sababu wewe unaweza kudhani ni matusi kumbe si matusi. Kwa hiyo sina maoni hadi nitakapoonyeshwa,” alisema Lissu ambaye akiwa bungeni, Spika wa Bunge, Makinda alimtaja kama ndiye kinara wa vurugu ndani ya ukumbi wa Bunge.

Moto wazidi kusambaa
Uamuzi huo wa Spika kupitia Kamati ya Kanuni za Bunge ambao Lissu anasema ni ushahidi mwingine wa matumizi mabaya ya kanuni za Bunge, umezidi kuwa mwiba kwa uongozi wa Bunge licha ya kwamba ni uamuzi uliopitia hatua zote za kibunge.

Inaelezwa kwamba baadhi ya mabalozi nchini wameanza kufuatilia sababu hasa za kufikiwa kwa uamuzi huo, ikizingatiwa ya kwamba lengo la kamati hiyo pamoja na nyingine ni kudhibiti matumizi ambayo yanatokana na Bajeti inayochangiwa na baadhi ya nchi wahisani.

Taarifa zinaeleza kuwa, Zitto Kabwe anaweza kupata fursa ya kujieleza mbele ya wahisani nchini na anaweza kufanya hivyo katika kikao kilichoandaliwa Alhamisi, wiki hii jijini Dar e Salaam.
Akizungumzia uamuzi huo, mmoja wa wadau alisema; “Mapendekezo ya CAG katika taarifa ya mashirika ya umma ya mwaka 2011 yanasema Bunge linapaswa kupanua majukumu Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Uma katika kuhakikisha kamati inakuwa na nguvu ya kikanuni za Bunge katika kusimamia hesabu za mashirika na kampuni zote ambazo serikali ina hisa. Hata kama serikali inamiliki asilimia chini ya 50.”

Lakini mmoja wa wabunge ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema; “Sijui kwa nini watu wanahangaika, Bunge kupitia Kamati ya Kanuni haikufuta shughuli za iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma bali kilichofanyika ni kuhamishia majukumu hayo katika kamati nyingine ili kupata ufanisi zaidi.”

Mbali na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma kuunganishwa na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, Kamati nyingine iliyoundwa ni iliyokuwa Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje ambayo imemegwa na kuundwa kamati mbili, moja ni Ulinzi na Usalama na nyingine ni Kamati ya Mambo ya Nje.
Source:Raia Mwema

Monday, February 11, 2013

Rais Kikwete amjibu Lowassa tatizo la ajira nchini


 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete katika hali inayoashiria kumjibu rafiki yake, Edward Lowassa ameponda makada wa chama hicho ambao wamekuwa wakipanda jukwaani kuhubiri kuwa ajira ni tatizo pasipo kupendekeza suluhisho la tatizo hilo.
 

Rais Kikwete ambaye alikuwa akifungua semina ya siku mbili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma jana, alisema kusimama jukwaani na kusema kwamba ajira ni tatizo hakuna maana ikiwa mhusika hatoi pendekezo la jinsi ya kumaliza tatizo hilo.
 
Ingawa hakutaja majina ya wanasiasa ambao wamekuwa wakizungumzia suala hilo lakini Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la ajira kwa maneno kwamba ‘ni bomu linalosubiri kulipuka’.
 

Lowassa, ambaye ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM, aliwahi kuingia hata kwenye malumbano makali na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka.
 
Kabaka akiwa bungeni mjini Dodoma, Machi 21, 2012 alilazimika kutoa takwimu za namna Serikali ilivyokuwa inatengeneza ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa ameeleza tatizo la ajira linavyowaathiri vijana kwenye moja ya hafla.
 

Lowassa ameendelea kuzungumzia suala hilo mara kwa mara kila anapopata fursa ya kuhutubia.

“Ndiyo ajira ni tatizo, hapa mkakati ni ajira itapatikana vipi? Ni tatizo kweli, tunafanyaje na tunalitatua vipi? Tunataka mtu anayesema kwamba ni tatizo na apendekeze pia suluhu yake,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliwahi kutamka kuwa Lowassa ni rafiki yake na anafahamika kuwa alishirikiana naye katika harakati zake za kuwania urais mwaka 2005, na baadaye akamteua kuwa Waziri Mkuu
 
Lowassa, ambaye ni miongoni wa makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais mwaka 2015, alikaririwa akisema Oktoba 19, 2011 kuwa; “Sijakutana na Rais Kikwete barabarani, watu waache kunichonganisha naye.” Ilikuwa katika mkutano na waandishi wa habari jimboni kwake Monduli.
 

Suala la ajira nchini ni moja ya mada zinazotarajiwa kuwasilishwa kisha kujadiliwa katika semina hiyo ya CCM, na Rais Kikwete aliwataka wajumbe kupendekeza jinsi ya kuongeza ajira nchini wakati mjadala husika utakapowadia.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema hivi sasa ajira katika sekta ya umma ni kama hakuna, kwani zimebaki sekta za afya na elimu na kwamba hivi sasa suluhu ni kukuza sekta binafsi ili kuongeza ajira.
 

Alitoa mfano kwamba wakati yeye alipohitimu kidato cha nne, cha sita na chuo kikuu hakukuwa na tatizo la ajira kwa kuwa idadi ya wasomi ilikuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya soko hilo.
 

Kikwete alisema wakati huo Serikali ilikuwa haijajitosheleza, tofauti na sasa ambapo imefikia ukomo wa kuajiri isipokuwa kwa sekta mbili tu.
 
“Kwa sasa Serikali haina uwezo tena wa kuajiri, ilifika mahali kila kiongozi anaenda kuomba serikalini na kupeleka watu wake, unakuta anatoka Kikwete anaomba mtoto wake aajiriwe, mara Katibu Mkuu naye anapeleka watu wake, ikafika mahali mashirika yakajaa tukapata kazi ya kuwapunguza,” alisema Rais Kikwete
.

Rais Kikwete alisema sehemu kubwa ya ajira inatoka katika sekta binafsi na jambo la msingi ni kwa viongozi kushirikiana na Serikali kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuikuza.
 

“Tutaendelea kuwaita wawekezaji wezi halafu tunataka kukuza ajira? Tunazipataje nafasi zaidi, wakiwekeza wanafanyiwa fujo wasiwekeze,” aliongeza Rais Kikwete, ambaye bila kuingia kwa undani kuhusu fujo lakini wafuatiliaji wa mambo wanaweza kuoanisha kauli hiyo na vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ambako wananchi wanapinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
 
Soma zaidi: Mwananchi
 

Thursday, February 7, 2013

Rage kitanzini Dodoma


 
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema kuwa wanaandaa jalada la kuhusika kwa Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage kwa ajili ya kuliwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).


Kamanda Misime alisema jana kuwa wako mbioni kukamilisha jalada hilo ili walipeleka kwa DPP kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.“Ni kweli tumepokea malalamiko ya Chadema na tunaandaa malalamiko ili kuwasilisha kwa mwanasheria na Serikali,” alisema Misime.
 
Hayo yamekuja kutokana na vurugu zilizotokea kati ya wafuasi wa Chadema na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Rage wakati walipokuwa wakigombea mlingoti wa bendera kitendo kilichosababisha watu watatu kujeruhiwa katika tukio hilo wikiendi iliyopita mjini Dodoma.
Hata hivyo, Rage amekana kuhusika na vurugu hizo akisema anaamini uchunguzi kuhusu tukio hilo utamuweka huru kabla au baada ya kufikishwa mahakamani kwa sababu hakushiriki wala kumpiga mwanaChadema aliyetangaza kumshtaki.

“Sikumpiga. Historia yangu inaonyesha kuwa sijawahi kushiriki vitendo vya vurugu wala mapigano kwa sababu yoyote ile. Mimi siyo mhuni wa kupiga mtu. Nilichofanya ni kumlinda yule kijana asipigwe na wanaCCM waliojaa hasira kwa yeye kuingilia mkutano wetu,” alisema Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.

Alisema kada wa Chadema ndiye chanzo cha vurugu hizo zilizoishia kwa kujeruhiwa na wanaCCM baada ya kuvamia eneo la mkutano wa chama hicho.

“Baada ya kuona kitendo hicho, mimi pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Iringa, Deo Sanga, kama viongozi tulimfuata kijana yule na kumsihi asifanye hivyo baada ya kuona vijana wa CCM waliokuwapo eneo lile wanaanza kupandisha jazba ambazo tusingemudu kuzizuia, lakini hakutusikilizwa,” alisema.

Rage alisema baada ya kuona kijana huyo anaanza kushambuliwa na wanaCCM ndipo alipolazimika kuingilia kati kuwaamulia na kumkinga asipigwe na mawe na majabali yaliyokuwa yameshikwa na wanaCCM, ambapo kijana huyo alifanikiwa kuchomoka na kukimbia.

Alisema kabla ya vurugu, kundi dogo la wafuasi wa Chadema lilikuwapo eneo la mkutano wakiwa na bendera ya chama hicho bila kufanya vurugu yoyote, ambapo yeye aliwasihi kuwaacha wasikilize sera za chama hicho kwani mkutano ulikuwa wazi kwa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

Hata hivyo, picha zilizopigwa na kuchapishwa kwenye vyombo vya habari zilimwonyesha Rage na wafuasi wa CCM wengine wakiwa katikati ya vurugu hizo na juzi uongozi wa Chadema Wilaya ya Dodoma ulitangaza kumburuta mahakamani mbunge huyo kwa tuhuma za kujeruhi, kung’oa na kuharibu mali za chama hicho kikuu cha upinzani nchini
 
Kauli ya Rage imetokana na kitendo cha uongozi wa Chadema wa Wilaya ya Dodoma kutangaza nia ya kumshtaki baada ya kumpiga kada wao.
Makada wa CCM na Chadema walipigana Jumapili iliyopita wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya CCM mjini Dodoma.

Vurugu hizo zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kukasirishwa na kitendo cha vijana wa CCM kung’oa bendera yao wakati wakiendesha mkutano kwenye eneo la Mwanga Baa mjini Dodoma.
Wafuasi hao wa Chadema walilazimisha kurudisha bendera yao wakati mkutano ukiendelea, ndipo makada wa CCM waliojumuisha wabunge wa Jamhuri ya Muungano walipoamua kuwapiga kwa kuwarushia mawe wafuasi hao na kusababisha kuumia kichwani kwa kada wa Chadema.
 
Wabunge wa CCM waliokuwa katika tukio hilo ukiacha Rage ni pamoja na Seleman Jafo, Said Mtanda, Mary Chatanda na Nyambari Nyangwine.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumzia suala hilo alimtetea Rage, akisema alikuwa akiamua ugomvi huo na kama isingekuwa yeye mauaji yangetokea.
“Hakuhusika yeye alikuwa akiamua ugomvi na kama asingekuwepo mauaji yangetokea,” alisema Ndugai.
 
Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama alisema kwamba hajapata taarifa za kuwapo kwa tukio hilo.
 
Source: Mwananchi

Sunday, February 3, 2013

Taswira Field Practical Supervision...Lindi Rural, Masasi na Ruangwa

Safari ilianza Lindi vijjini, Masasi tukamalizia na Ruangwa...picha hizi zimekaa kwa mtiririko huo.

Njonjo-Lindi Rural 
Ruhokwe-Lindi rural 
                                                                   kitomanga-kwa ustadhi
                                             Kilangala-Obadia na wenzake....good house
                                                            Mchinga-Lindi
                                                     Narunyu-Lindi Rural
                                                              Luwale-Lindi Rural
                                                  Nyengedi-wapo kumi hapa.....
                                              Mtama- Mihogoni, Majengo A&B, Makonde
                                                 Nyangao-hawa wanaishi kama wako home
                                          Nanganga-Masasi...hawa washakuwa Ma Dr wa mifugo
                                                Ndanda Mission-Hapa ni kama uzunguni
                                                 Mwena- hawa jamaa hawana shida ya maji
                                                   Chiwata-Yasin na wenzie wapo hapa
                                                                    Mpindimbi
                                                                        Mtandi
                                                                        Lulindi
                                                                     Chiungutwa
                                                                  Nanjota
                                                                 Mumbaka
                                                                   Mlingula
                                                                  Namajani
                                                                  Namatutwe
                                                     Mpanyani- Hapa ni mbali kweli kweli..
                                                                Lukuledi-Masasi
                                                          Temeke-Uncle yupo hapa
                                                             Kitandi-Ruangwa
                                          Mandarawe na Nachinyimba-hawa wanapiga kazi kwelikweli
                                          Liuguru- hawa walikumbana na majaribu ya wachawi
                                                   Chunyu-Tego na wenzie wapo hapa
                                          Mmawa- Hawa jamaa wapo fiti kwenye mifugo
                                            Likunja-Rwegasira na wenzie wapo hapa
                                          Nkowe-Lucy Lubuva na wenzie wako hapa
                                          Chienjere- Hapa ni cone belt...mahindi kibao
                                                 Namahema na Nandagala-Ruangwa
                                                 Mtimbila-Kuboja na wenzie wapo hapa
                                                      Michenga-hapa tulifika jioni sana
                                                            Nangumbu-Ruangwa
                                             Mtakuja- na kweli tulifika...Joy yupo hapa
                                               Hapa ni Mbecha kwa kina Manjanjagara
                                          Luchelegwa-Ayoub mzee wa English yupo hapa
                                          Chinongwe-Almas., Alphonse wapo hapa


It was very interesting journey..we shared a lot with our students and their supervisors...may god bless us all...Thank you very much...we arrived home safelly.
               



















































Saturday, February 2, 2013

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA


 
Utangulizi
 
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwenye Rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuzungumza kwa mara nyingine kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na wananchi wa Tanzania kila mwisho wa mwezi. Siku ya leo nitazungumzia safari yangu ya Ufaransa, Uswizi na Ethiopia. Pia nitazungumzia ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.
 
Safari za Kikazi Nje ya Nchi
 
Ndugu Wananchi;
Safari yangu ya Ufaransa, Uswizi na Ethiopia ilikuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu. Nchini Ufaransa licha ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi zetu, tumepata wawekezaji wengi wakubwa wenye nia thabiti ya kuja kuwekeza hapa nchini. Pia tumekubaliana kuanza mazungumzo ya kuwa na mpango mwingine wa ushirikiano. Mpango wetu wa sasa ulioanza mwaka 2006 uliisha mwaka 2010. Mpango ule ulitusaidia sana kuboresha huduma za maji katika miji ya Utete mkoani Pwani na Mpwapwa mkoani Dodoma.
Katika mkutano wa Kongamano la Uchumi wa Dunia uliofanyika Davos, Uswizi, tumehakikishiwa ushirikiano katika kuendeleza juhudi zetu za kuleta mapinduzi ya kijani ili tujihakikishie usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini na kukuza uchumi wa nchi yetu. Aidha, tulipata bahati ya kushirikishwa katika mjadala wa kuanzishwa kwa programu kubwa ya kuzisaidia nchi za Afrika kutatua matatizo ya upatikanaji wa umeme. Naamini programu hiyo ikitekelezwa na wakubwa kuheshimu kauli na ahadi zao itakuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
 
Ndugu Wananchi;
Nchini Ethiopia tulishiriki katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na katika kikao cha African Peer Review Mechanism (APRM) ambapo taarifa ya tathmini ya utawala bora ya Tanzania na Zambia iliyofanywa na APRM ilijadiliwa. Kwa jumla hatuna mahali tuliponyooshewa kidole kuwa tunafanya vibaya. Tumepongezwa katika mambo mengi na tumepewa ushauri kwa baadhi ya maeneo waliyoona hatuna budi kuyaboresha. Nilipata nafasi ya kusema ambayo niliitumia kufafanua baadhi ya mambo yaliyokuwamo kwenye taarifa. Niliwashukuru na kuahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa. Tathmini ya nchi yetu ilipitishwa kwa kauli moja.
 
Vurugu za Kupinga Gesi Kusafirishwa Kutoka Mtwara
Ndugu wananchi;
Kama mtakavyokumbuka tarehe 8 Novemba, 2012 kule Kinyerezi, Wilaya ya Ilala hapa Dar es Salaam, niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara na Songosongo kuja Dar es Salaam. Karibu na mwishoni mwa Desemba, 2012 kukafanyika maandamano mjini Mtwara kupinga ujenzi wa bomba hilo. Katika maandamano yale na baadaye kwenye kauli za wanasiasa na wanaharakati yakatolewa madai kuwa gesi hiyo itumike kwa maendeleo ya Mtwara na kwamba yale yanayotakiwa kufanyika Dar es Salaam yafanyike Mtwara. Pia, zilitolewa shutuma nyingine dhidi ya Serikali eti kuwa kwa miaka mingi imewasahau na haiwajali wananchi wa Mikoa ya Kusini na ujenzi wa bomba hilo ni muendelezo wa hayo. Kauli mbalimbali za wanasiasa na wanaharakati ni kama vile ziliongeza mafuta kwenye kaa la moto na kuuchochea mpaka kukatokea matukio yaliyotusikitisha na kutshtua sote. Baadhi ya ndugu zetu wamepoteza maisha na mali za watu na Serikali kuharibiwa.
 
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, tarehe 31 Desemba, 2012, nililisemea jambo hili. Leo mwezi mmoja baadae, napenda kusisitiza mambo mawili. Kwanza kwamba, si kweli kuwa Serikali inapuuza Mikoa ya Kusini. Na pili, kwamba kujenga bomba la kuipeleka gesi Dar es Salaam hakuinyimi Mikoa ya Mtwara na Lindi fursa ya kunufaika na gesi iliyopo Mtwara.
 
Ndugu Wananchi;
Serikali imefanya, inafanya na ina mipango ya kufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya kuleta maendeleo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi. Ipo mipango ya kuboresha miundombinu, huduma za kiuchumi na kijamii pamoja na kukuza uchumi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vikubwa na vidogo. Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa, ilijenga daraja katika Mto Rufiji maarufu kama Daraja la Mkapa. Hii ilikuwa ni hatua kubwa ya awali katika safari ya kutatua matatizo ya usafiri ya Mikoa ya Kusini. Serikali ninayoiongoza mie iliachiwa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara za lami kufikia darajani na kuunanisha Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa Ruvuma. Kazi hiyo, tumeitekeleza vizuri na sasa tunakaribia kuimaliza. Tulikamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Mnazi-Mmoja hadi Nangurukuru. Mwaka 2009 tukaanza ujenzi wa barabara ya kilomita 56 kutoka Somanga hadi Ndundu (darajani). Ujenzi wa kilometa 36 za mwanzo ulienda vizuri. Bahati mbaya ujenzi wa kilomieta 20 za mwisho umechelewa sana kwa sababu ya mmiliki wa kampuni iliyokabidhiwa kufanya kazi hiyo kufariki. Kwa sababu hiyo, kampuni ilipata mtikisiko kiasi na kusababisha kazi kutotekelezwa kwa kasi tuliyoitarajia. Sasa mambo yametengemaa na kazi inaendelea kwa kasi nzuri. Matumaini yetu ni kuwa ifikapo mwezi Desemba, 2013 kazi hiyo itakuwa imekamilika.
Hali kadhalika, Rais Mstaafu, Mzee Benjamin Mkapa alituachia jukumu la kumaliza ujenzi wa Daraja la Umoja katika mto Ruvuma na ujenzi wa barabara ya lami kuanzia Mikoa ya Mtwara na Ruvuma. Tumelikamilisha Daraja hilo na ujenzi wa barabara ya lami kutoka Masasi hadi Mangaka umekamilika. Mchakato wa kujenga barabara ya kwenda Songea na kwenda Darajani umefikia mahala pazuri. Tenda ya ujenzi wa barabara kutoka Tunduru hadi Mangaka mpaka Darajani imeshatangazwa. Kama mambo yataenda sawa miezi mitatu ijayo mjenzi atapatikana. Wakati huo huo ujenzi wa barabara kutoka Namtumbo hadi Songea – Mbinga na Namtumbo – Tunduru unaendelea. Hivyo basi, kwa barabara ya “Mtwara Corridor” kazi iliyobaki ni kutoka Mbinga kwenda Mbambabay ambayo tutaifanya wenyewe kama tulivyofanya kwa Mnazi Mmoja – Nangurukuru na Somanga – Ndudu na Daraja la Umoja.
 
Ndugu Wananchi;
Ipo pia mipango ya kuipanua na kuijenga upya bandari ya Mtwara ili iweze kuhudumia mahitaji ya utafutaji na uchimbaji wa gesi baharini, kuhudumia na kuvifanyia matengenezo vyombo vinavyotumika katika utafiti, uchimbaji na uendelezaji wa gesi. Pia iweze kuhudumia shughuli za kiuchumi zitakazotokana na uchumi wa gesi pamoja na zilizopo sasa. Nilipozungumza na makampuni ya utafutaji gesi pale Mtwara tarehe 25 Julai, 2011 waliomba nikubali bandari ya Mtwara iwe mahali pa kuhudumia vyombo vyote vinavyofanya shughuli ya utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta katika pwani ya Afrika ya Bahari Kuu ya Hindi. Pia waliomba kuwa sehemu hiyo ya bandari iwe bandari huru. Niliwakubalia bila ya kusita na tayari eneo la hekta 110 zimeshatengwa na kutangazwa rasmi kuwa bandari huru. Vile vile waliomba wapewe sehemu ya bandari ya sasa kuendeshea shughuli na eneo la kujenga kituo cha mitambo ya kuchakata gesi na kusafirisha nje.
 
Ndugu Wananchi;
Baada ya kuzungumza na makampuni ya utafutaji gesi na mafuta na kuelezwa mahitaji yao nilibaini kuwa bandari ya Mtwara inahitaji kupanuliwa na kujengwa upya. Bahati nzuri viongozi wa Mamlaka ya Bandari walikuwepo na walinihakikishia kuwa watafanya hivyo.
Tayari eneo la bandari limeongezwa kutoka hekta 70.68 hadi 2,693.68. Eneo la bandari huru limeshatengwa hivyo hivyo na eneo la kampuni ya Dangote na makampuni ya gesi yaliyopo. Aidha, mchakato wa kupanua bandari iliyopo, kujenga gati mpya na kuendelea na ujenzi hadi maeneo ya Msanga Mkuu ipo katika hatua mbalimbali za matayarisho na utekelezaji.
 
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Mkoa wa Lindi mipango ya kupanua na kuijenga upya bandari ya Lindi imefikia hatua nzuri. Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba alithibitisha hayo tarehe 1 Desemba, 2012 nilipotembelea bandari hiyo wakati wa ziara yangu ya Mkoa wa Lindi ya tarehe 1 mpaka 5 Desemba, 2012. Hali kadhalika mipango ya kujenga bandari ya Kilwa iko mbioni. Tena kwa upande wa Mkoa wa Lindi moja ya makampuni yaliyogundua gesi baharini wameamua kujenga bandari na kituo cha kuchakata na kusarifisha gesi nje ya mkoa huo kama ilivyo kwa Mtwara. Naambiwa wametambua maeneo matatu, kilichobakia ni kuamua mojawapo ili ujenzi uanze.
 
Ndugu Wananchi;
Nilipotoka bandari ya Mtwara, siku ile nilitembelea Chuo cha VETA na kuzungumza na viongozi wa VETA taifa na wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu kuwa na mitaala ya kutoa mafunzo mahsusi yanayohitajika na sekta ya gesi na mafuta. Nilisisitiza kwamba tuwapatie vijana wetu mafunzo yatakayowawezsha kuajiriwa na makampuni ya gesi na yale yatakayokuwa yanatoa huduma kwa makampuni hayo. Nilisema tusipofanya hivyo, makampuni hayo yataajiri watu kutoka nje na hatutakuwa na sababu ya kuwalaumu wala kulalamika.
Nafurahi kwamba agizo langu hilo limefanyiwa kazi ipasavyo. Hivi sasa katika chuo cha VETA Mtwara mafunzo hayo yanatolewa. Kampuni ya PetroBrass ya Brazil inaendesha mafunzo ya sekta ya gesi kwa vijana 25 kutoka mkoani Mtwara. Aidha, chuo cha VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya Gesi ya Uingereza (British Gas) na Volunteers Service Overseas ya Uingereza, kinatekeleza programu ya miaka mitatu iitwayo Enhancing Employerbility Through Vocational Training. Programu hii inalenga kutoa kozi zitakazowafanya wahitimu kuweza kuajiriwa katika sekta ya gesi. Programu hii ilifunguliwa na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, tarehe 26 Novemba, 2012.
 
Ndugu Wananchi;
Chini ya programu hii, walimu wa masomo yanayohusiana na gesi wanaongezewa ujuzi ili waweze kufikia viwango vya kimataifa. Vile vile, Wizara ya Nishati na Madini imetoa upendeleo maalum wa kudhamini wanafunzi 50 kutoka mkoa wa Mtwara kusoma chuoni hapo ambao tayari wameshahitimu mafunzo ya msingi ya uunganishaji vyuma viwandani. Mchakato wa kuwapata wanafunzi 50 kwa ajili ya mafunzo kama hayo kutoka mkoa wa Lindi unaendelea. Nimeambiwa mpaka wameshawapata vijana 25 bado 25.
Hali kadhalika, Wizara ya Nishati na Madini inadhamini wanafunzi 10 kupata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako kozi za mafuta na gesi zinatolewa. Kipaumbele kwa udhamini huu unatolewa kwa wanafunzi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wenye sifa za kudahiliwa katika mafunzo haya. Wamepatikana watatu. Wataalamu hawa na wengine wa fani mbalimbali za gesi na mafuta watafundishwa kwa kiwango cha shahada ya kwanza na baadae uzamili na uzamivu ili nchi yetu ijitosheleze kwa wataalamu wa sekta hii.
 
Kupanga Mji wa Mtwara
Ndugu Wananchi;
Baada ya kutembelea bandari ya Mtwara na Chuo cha VETA, nilikaa na kuzungumza na viongozi wa Serikali na Manispaa ya Mtwara. Katika mazungumzo yangu nao niliwasisitizia umuhimu wa kuwa na mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Mtwara – (Mtwara Masterplan) Mpango ambao utawezesha kujengwa mji mkubwa wa kisasa unaokidhi mahitaji ya mji wa uchumi wa gesi. Niliwataka wahakikishe kuwa kuna maeneo ya viwanda, biashara, makazi, mahoteli, huduma za afya, elimu, mapumziko na burudani, viwanja vya michezo na kadhalika. Kazi ya kutayarisha Masterplan hiyo imeanza na Manispaa ya Mtwara inashirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi.
Kwa upande wa uwekezaji nafahamu kuwa mpaka sasa makampuni 51 yameonyesha nia ya kuwekeza Mtwara katika viwanda, hoteli, shughuli za uchukuzi na huduma hasa kwa sekta ya gesi. Wanachosubiri ni kutengewa maeneo ya kujenga, waanze. Hivyo kukamilika mapema kwa Masterplan ya mji wa Mtwara kutasaidia kuongeza kasi ya uwekezaji huu kufanyika. Viwanda hivi vyote vitasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Mtwara na Watanzania kwa jumla. Nimeambiwa kwa mfano, wakati wa ujenzi wa kiwanda cha saruji watu zaidi ya 7,000 wataajiriwa. 
 
Ndugu Wananchi;
Kabla hata ya ugunduzi wa gesi iliyoko baharini, tulikuwa na mipango ya kutumia gesi ya Msimbati (Mnazi Bay) kwa ajili ya kuzalisha umeme, kuzalisha mbolea na kutumika katika kiwanda cha saruji. Kwa upande wa umeme kulikuwa na mpango wa kujenga mtambo wa kuzalisha Megawati 300 kwa kushirikiana na mwekezaji binafsi. Bahati mbaya wakati wa matatizo ya kifedha ya dunia mwaka 2009 mwekezaji huyo akashindwa kupata mkopo, hivyo mradi ukasimama kutekelezwa. Haukufa wala haukuhamishiwa Dar es Salaam au Bagamoyo kama ambavyo imekuwa inapotoshwa kwa makusudi. Mradi huo bado upo, tena mpango wa sasa ni kujenga Megawati 600 zitumike Mtwara na zingine kuziingiza kwenye gridi ya taifa kupitia Songea.
 
NduguWananchi;
Kwa upande wa kiwanda cha mbolea, wawekezaji wengi wameshajitokeza tangu mwaka 2008 mpaka sasa. Mchakato umefanyika wa kuchambua wawekezaji wenye sifa na kutambuliwa. Mambo mawili yamechelewesha utekelezaji kuanza. Jambo la kwanza ni wawekezaji na kampuni ya Artumas iliyokuwa mbia na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (T.P.D.C) wakati ule, kushindwa kukubaliana nao juu ya bei ya kuwauzia gesi. Wawekezaji walitaka bei ya gesi ipunguzwe, lakini kampuni ya Artumas na T.P.D.C. hawakuwa tayari kupunguza zaidi ya kiasi walichopunguza, ambacho wawekezaji bado waliona hailipi kwa kuzalisha mbolea.
Sababu ya pili ni matatizo ya kifedha yaliyoikumba kampuni ya Artumas katika kipindi hicho. Kufuatia machafuko ya masoko ya fedha na mdororo wa uchumi wa dunia mwaka 2008/2009 kampuni ya Artumas iliathirika na kulazimika kuuza hisa zake kwa wawekezaji wengine. Katika kipindi hicho ilichopitia kampuni, mazungumzo na uwekezaji wa kiwanda cha mbolea hayakuweza kupewa kipaumbele. Mtazamo wa sasa wa wabia wapya na T.P.D.C. ni kuwa wao wenyewe sasa wawekeze katika ujenzi wa kiwanda cha mbolea. Serikali imekubali rai yao hiyo na wanaendelea na matayarisho.
 
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa kiwanda cha Saruji kitakachojengwa na kampuni ya Dangote ucheleweshaji ulikuwa kwa sababu mbili. Kwanza, kampuni ya Dangote iliomba eneo zaidi ya ililokuwa imeomba na kupewa. Hoja yao ilikuwa kwamba eneo la ziada walilokuwa wanaliomba ndilo lenye malighafi nyingi na bora kwa utengenezaji wa saruji. Hivyo, waliamua kusubiri mpaka watakapopewa eneo hilo.
Bahati mbaya eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na mtu mwingine na alikuwa na hati miliki nalo. Halmashauri ya Mtwara iliomba Serikali eneo hilo litwaliwe na baadaye ipewe kampuni ya Dangote. Serikali ilikubali. Hata hivyo, mchakato ulichukua muda na hata pale ulipokamilika mwenye eneo aliupinga uamuzi wa Serikali Mahakamani. Kesi ilichukua muda kusikilizwa na kumalizika. Bahati nzuri Serikali ikashinda na mara baada ya uamuzi wa Mahakama ndipo kampuni ya Dangote ikamilikishwa eneo hilo.
Kampuni nayo ilichukua muda kuanza. Hivi sasa, timu yake ipo kwenye eneo na mradi uko tayari kuanza kutekelezwa. Niliambiwa kuwa katika magari yaliyopigwa mawe katika fujo za Mtwara ni pamoja na lile la mradi huu. Huo ndiyo ukweli kuhusu ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote. Madai kuwa kiwanda hicho kimehamishiwa Bagamoyo si ya kweli. Ni uzushi wa makusudi wa watu wenye nia mbaya na Serikali. Huwezi kudai kuwa mtetezi wa wananchi wa Mtwara kwa hoja za uongo na kufanya upotoshaji wa makusudi kabisa.
 
Ndugu Wananchi;
Ujenzi wa bomba la gesi ndiyo uliozua mzozo wote huu. Zilijengwa hisia kuwa gesi yote inapelekwa Dar es Salaam na kwamba Mtwara itakosa gesi na maendeleo yatayotokana na gesi hiyo. Na, wengine wakasema gesi inapalekwa Bagamoyo ili kuzidisha chumvi na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali kwamba Rais anapeleka gesi kwao. Kwanza, Kinyerezi iko Ilala na siyo Bagamoyo. Pili, ukweli ni kwamba pale Mtwara kuna gesi nyingi ya kutosheleza mahitaji ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam na kubaki. Gesi itakayoletwa Dar es Salaam ni asilimia 16 tu ya gesi yote iliyoko Mtwara kwa miaka ishirini ijayo. Hivyo asilimia 84 ya gesi itabaki Mtwara kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi na kupelekwa kwingineko nchini.
Kwa sababu hiyo, ndugu zetu wa Mtwara hawana sababu ya kuwa na wasiwasi. Ipo gesi ya kutosha kwa mahitaji ya sasa na ya miaka mingi ijayo. Viwanda vinavyotumia gesi kama mali ghafi na vile vinavyohitaji gesi kama nishati vyote vitapata gesi ya kutosha. Kwa upande wa uzalishaji umeme hali kadhalika ipo gesi ya kutosha kuzalisha umeme mwingi zaidi. Hivi sasa tunacho kituo kinachozalisha umeme wa megawati 15 unaotumika Mtwara, Lindi, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Ruangwa, na Mtama. Bado umeme huo hautumiki wote hivi sasa.
 
Ndugu Wananchi;
Nayaeleza yote haya kuwathibitishia wananchi wa Mtwara kuwa tunawathamini sana na kuwajali. Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuwapuuza na kuwatupa mkono wananchi wa Mikoa ya Kusini. Aidha, sitakuwa tayari kuwaruhusu watu au mtu ye yote Serikalini kuwapuuza wananchi wa Mikoa ya Kusini au mkoa wo wote hapa nchini. Hiyo haitakuwa sawa. Nilishasema siku za nyuma na napenda kurudia tena leo kuwa kwangu mimi hakuna mkoa ulio bora kuliko mwingine. Ni kutokana na msimamo wangu huo ndiyo maana tumeelekeza nguvu na rasilimali nyingi za Serikali katika mikoa iliyokuwa inadaiwa kuwa imesahauliwa. Kazi ya ujenzi wa barabara za lami iliyofanyika na inayoendelea kufanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Kigoma na Kagera inajieleza yenyewe. Mipango ya kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Mtwara kufikia hadhi ya kimataifa na uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Lindi na Kilwa ni ushahidi mwingine kati ya mambo mengi tunayoweza kuyataja.
 
Ndugu Wananchi;
Haya niliyoyasema ni sehemu ndogo tu ya yale yaliyofafanuliwa na kuelezwa kwa kina na Mawaziri na Wakuu wa Idara husika za Serikali na Mashirika ya Umma pale Mtwara katika mkutano wa Waziri Mkuu na viongozi wa Serikali, dini, vyama vya siasa na wazee wa Mkoa wa Mtwara tarehe 29 Januari, 2013.
Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya kule Mtwara. Uvumilivu wake, usikivu wake na utulivu wake vimesaidia sana kulivusha taifa katika moja ya mitihani mikubwa ambayo ingeikuta nchi yetu tangu Uhuru. Nawapongeza Mawaziri na Wakuu wa Mashirika ya Umma na Idara za Serikali kwa mchango wao muhimu walioutoa, uliosaidia kufafanua masuala ambayo yalikuwa hayaeleweki vizuri. Kwa wao nawasisitiza na kuwakumbusha wajibu wao wa kuelimisha jamii kuhusu shughuli wazifanyazo. Wakifanya hivyo mara kwa mara migongano haitakuwepo na wapotoshaji hawatapata nafasi.
 
Ndugu Wananchi;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama sitawashukuru viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, madhehebu ya dini, viongozi wa jamii, wazee, wana-Mtwara na makundi mbalimbali ya jamii, kwa muda waliotumia kuzungumza na Waziri Mkuu na kuwasikiliza wasaidizi wake wakifafanua masuala mbalimbali. Uvumilivu wao na uelewa wao npyo vilivyosaidia kurejesha hali kuwa ya kawaida. Nawaomba nao sasa, wote kwa pamoja washirikiane na Serikali kuelimisha umma kuhusu ukweli wa mambo. Pia watumie nafasi hiyo kutahadharisha jamii na kuwataka watu kuwa waangalifu na kupima maneno wanayoambiwa na watu. Wajiepushe na maneno au vitendo vinavyofarakanisha, kuchonganisha na kupandikiza chuki dhidi ya watu au Serikali. Waambieni kuwa ghasia hukimbiza wawekezaji kwani wakipata hofu kuwa hali ya amani na usalama ni ya mashaka, watatoka kwenda kuwekeza kwingine. Vyema iwe hapa hapa nchini, lakini wanaweza kwenda nchi nyingine na sisi kupoteza kabisa.
 
Ndugu Wananchi;
Nawapa pole wananchi wa Mtwara na Masasi kwa usumbufu walioupata kutokana na ghasia zilizofanywa. Nawapa pole waliofiwa na kujeruhiwa. Nawapa pole waliopoteza au kuharibiwa mali zao. Kwa kweli inasikitisha na kufadhaisha kuona watu wanafanya vitendo vya kuua, kuchoma moto nyumba za watu na majengo ya Serikali pamoja na , kuharibu na kuiba mali za watu. Huu ni uhalifu ambao hauna maelezo na haukubaliki. Tunaviachia vyombo husika vya dola na sheria kutimiza wajibu wao. Kwa waliohusika iwe fundisho kwao na kwa wengineo kutokubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine siku zijazo. Sasa wameachwa pekee yao wakati wenzao wako huru na kufaidi maisha
 
Ndugu Wananchi;
Hili sakata la bomba la gesi limefika mahali pazuri. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni Sana kwa Kunisikiliza!