Pages

Wednesday, October 31, 2012

Study tour at Narunyu day four (picha na maelezo)

NTRODUCTION

This day was stream D turn, and guest tutors in this journey were Selemani Nannume and Hilal S Hilali. As usual normal protocols were followed and for that matter the time table arranged followed too.

 

SPRAYRACE

There is huge sprayrace at Narunyu Sisters centre, where by a lot of animal can get cleaned one at a time. Student got opportunity to see it and Sister Mbunda demonstrated to them how water is pumped from the tank untill they reach to sprinkler. The sprinkrers can watering animals in each sides, up and bottom, left and right, once got cleaned animals are directed to resting yard.

 

COST

This sprayrace is operated by electricity motor and it is very expensive for a normal farmer to afford. A lot of agriculture insitutes do not posess this machine because of it is high initial cost of purchasing.

 

SOURCE OF WATER

Narunyu sisters center has plenty of water which help them to run their activities efficiently. There is Nyasa liver stream which pass through 2500 hectare of their area, and they use the stream to find their sources of water, and got big tanks to collects water. As sister Mbunda said to establish the huge project like they run you need to have plenty of water. One cattle can drink 47 litres of water per day, the instute has 630 cattles, hence water is very important to them for rising cattle as well as increasing production.
 
It was very fun.
concentration
                                                           spinkler on
                                                                       top sprinkler
                                                                     concentration
resting yard
                                                    full watering from sprinkler

Tuesday, October 30, 2012

Kikwete akubaliana na Mnyika kuondoa udhaifu, Kabaka na Werema watakiwa kutoa kauli bungeni

Raisi J M Kikwete
 
Rais Jakaya Kikwete amemuagiza Waziri wa Kazi naAjira kutoa kauli bungeni ya kubatilisha tangazo la fao la kujitoa ili wafanyakazi kuendelea kuruhusiwa kupokea fao la kujitoa.

Rais Kikwete amemuagiza pia mwanasheria mkuu wa serikali kuondoa sehemu ya sita katika muswada wa marekebisho wa sheria ya mbalimbali iliyotaka kuruhusu fao la kujitoa kwa mfuko mmoja wa PPF pekee.

Hatua hiyo imekuja siku chachebaada ya mbunge wa Ubungo kutaka Kikwete kuingilia kati kuondoa udhaifu ulioonyeshwa na SSRA, Wizara ya Kazi na Ajira na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu suala hilo.

Habari kutoka vyanzo ndani ya serikali vinaonyesha kwamba Rais Kikwete alifikia uamuzi huo ili kuepusha Serikali kuingia katika mgogoro na wafanyakazi ukimhusisha yeye baada ya kubainika kwamba kwa ndiye mwenye mamlaka ya kikatiba.

Hatua hiyo inakuja siku chache kuelekea mkutano mkuu wa CCM na imetafsiriwa na wadadisi wa mambo kuwa Rais kama Mwenyekiti wa CCM ameepusha chama hicho cha wakulima na wafanyakazi kuingia katika mgogoro kuelekea mkutano huo ambao serikali itaeleza mafanikio yake katika kipindi cha miaka miwili ikiwemo kuhusu kazi na ajira.

Kwa mara ya kwanza wazo la kutaka agizo la SSRA litenguliwe na kubainisha kuwa agizo hilo halitokani na marekebisho yaliyofanyika bungeni tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali marekebisho ya miaka ya nyuma lilitolewa la Mnyika mwanzoni mwa mwezi Agosti wakati akiomba muongozo wa Spika ambao pia alitaka kuwasilishwe muswada wa sheria kurekebisha hali hiyo.

Siku chache baadaye mapendekezo yote mawili yalichukuliwa na Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo katika maelezo yake bungeni aliyoyawasilisha tarehe 6 Agosti 2012 na hatimaye Spika akaliongoza bunge kuweka maazimio.

Kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa hata baada ya azimio la bunge Mnyika aliendelea kutaka kauli ya Serikali ya kutengua agizo la SSRA tarehe 7 Agosti 2012, hata hivyo Waziri hakuzingatia ndani na nje ya bunge na pendekezo hilo ndio sasa Serikali hatimaye imekubali kulitolea kauli bungeni baada ya maelekezo ya Rais Kikwete.

Suala la fao la kujitoa limeleta malumbano kwa muda toka tangazo hilo la SSRA huku upande wa Serikali pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ukikataa suala hilo na wafanyakazi wakiongozwa na wafanyakazi wa migodini pamoja na wabunge wakiongozwa na Jafo na Mnyika wakitaka fao hilo lirejeshwe.

Kwa nyakati mbalimbali wabungehao wameeleza kusudio la kuwasilisha miswada binafsi ya sheria kuhusu sualahilo, wa kwanza kueleza kusudio hilo alikuwa Mnyika ambaye katika muongozo wakewa tarehe 3 Agosti 2012 pamoja na mkutano wake na waandishi wa habari baada ya muongozo huo alieleza kuwa aliandika kwa katibu wa bunge barua ya kuwasilisha muswada binafsi kwa hati ya dharura na kuanza kukusanya saini za wabunge.

Siku chache baadaye katika maelezo yake Bungeni tarehe 6 Agosti 2012 Jafo naye akataka serikali ilete muswada kwa hati ya dharura na kuahidi kwamba isingeleta angewasilisha. Mjadala wa muswada binafsi uliibuka tena baada ya tarehe 15Agosti 2012 Mnyika kueleza vyombo vya habari kuwa amewasilisha tena kusudio kwa katibu wa bunge baada ya kuona serikali haijawasilisha muswada kwa hati yadharura kama ilivyoahidi.

Siku chache baadaye Jafo naye akaeleza kwamba amewasilisha kusudio la hoja binafsi. Hata hivyo, wabunge wote wawili walitakiwa kuvuta subira serikali iwasilishe muswada huo na kuelezwa kwamba kwakuwa jambo hilo lina azimio la bunge ikiwa serikali haitaleta muswada, muswada huo ungewasilishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia suala hilo. Uamuzi wa Serikali kutoa kauli kuhusu suala hilo katika mkutano wa bunge unaondelea umezima mjadala mkali uliotarajiwa kuhusu matatizo ya wafanyakazi na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Source: Jamii forum

Monday, October 29, 2012

Study tour at Narunyu with stream C (Pic and Explanation)


INTRODUCTION

Todays tour we were accompanied by Mr S Mosha and this time we were with Stream C. We left at our institute at 06:30 AM and we reached at Narunyu at 08:30. As usual student were introduced to Sister Mbunda there after schedule of activities went on.

 

RECORD KEEPING

This time student learnt the importance of keeping records. At the animal zoo there is identification of each animal with their names, date of birth, mating date and death date. So each animal will be known to its efficiency of producing milk per day as well as its status.

 

BREEDING

The present cattle milk are of fourth breed where by their ability to produce milk is a little lower compared to the first breed. There are two reason which can be able to explain this case.

a) Scientific reason

Phenotype- These are external factors which influence the internal factor not to work properrly in such a way that the abilty of cattle to produce more cattle reduced.

b) Economic reason

The law of diminishing return can justfy this case efficiently. As you add more unit of successive input (feeds, medicine, mating to produce cattle in order to collect more milk) it will reach a point the output (milk) will be reduced.

 

First breed were able to produce 20 litres each, while the fourth breed are able to produce 8-15 litres per day. As entrepreneur you cant go on with this project because it is invaluable.

 

Establishment

The Narunyu Sister Agricultural centre was established in 1988 by Father Leonard Kobe. Momentarily it has 680 cattle in which 50 are milk cattle while the rest are beef cattle, the institute has several farm structures such as haye storage, silo pitt, animal zoo and biogas system.

student listening carefully
student at the top of biogas structure
learning session
Electric circuit -biogas
tools used to generate electricity-biogas
 

Sunday, October 28, 2012

Utajiri wa Kamanda Barlow unatisha

Marehemu Barlow

Frederick Katulanda, Mwanza
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa
Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji
Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

“Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia,” alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

“Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu,” alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

“Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria.”

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi
Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

“Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, ” alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata
Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima
Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

"Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

“Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza,” alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.
 
Source: Mwananchi

Saturday, October 27, 2012

Kikwete ataonya na kushangaa hadi lini?


Kwa mara nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameendelea kulalamika kuhusu rushwa ndani ya chama chake. Safari hii akifunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT) mjini Dodoma (Oktoba 22, 2012), ameshangaa kuona eti wanawake nao wameingia katika gulio la ununuzi wa uongozi.
 
Kuendelea kulalamika kwake kunatoa tafsiri kwamba pengine yeye ni kiongozi asiyejua nguvu za kimamlaka alizonazo katika kudhibiti rushwa. Ni kama anasubiri kiongozi mwingine wa juu yake asikie anavyolalamika ili wala rushwa waogope au wajirekebishe.
 
Kwa sasa CCM, rushwa ni sikio la kufa lisilosikia dawa. Ukweli ni kwamba dawa pekee ya kukabili janga la rushwa CCM, yaani uadilifu ni kama haipo. Kama ipo basi ni adimu mno na kasi ya ugonjwa kushambua ni kubwa.
 
Malalamiko ya Kikwete kama ilivyo kwa wanachama wenzake wakiwamo wale wanaoshindwa chaguzi kutokana na kutoa kiasi kidogo cha rushwa kuliko wenzao, yamesikika sana na yanatuchosha achilia mbali kukera.
 
Baada ya kauli za mara kwa mara kutoka kwa Kikwete kuhusu rushwa CCM, tulitarajia safari hii kushuhudia vitendo vya kijasiri kukabili rushwa hiyo.
 
Kinyume chake, tunasikia ‘mashairi’ yenye vina vya kushangaa eti hata wanawake wa chama hicho nao ni wadau wa rushwa. Kimsingi, anayeshangaa wanawake hao, yeye ndiye ambaye watu wanastahili kumshangaa kwanza.
 
Watu wanapaswa kumshangaa kwa kutotambua ukweli kwamba, kufumbia macho tatizo maana yake ni kulistawisha.
 
Sisi tunamweleza Kikwete, hatushangai hali hiyo kwa sababu kila wakati yeye amekuwa kiongozi wa maneno matupu kuhusu kudhibiti rushwa ndani ya CCM.
 
Kwa sababu alishindwa tangu mwanzo na tatizo hilo kuvuka hadi kwa hao anaowashangaa, tunamshauri ajiandae kushangaa kushuhudia hata chipukizi wa chama hicho wakisaka uongozi kwa rushwa.
 
Tunamshangaa kwa kuwashangaa watoa rushwa wa kike CCM. Ajue rushwa ya sasa ni ya kimfumo si suala la mwanamke, mwanamume au mtoto. Rushwa haijifuti kwa kauli zake za kushangaa wengine.
 
Rushwa inafutwa kwa kupandikiza uadilifu na njia za kupandikiza uadilifu ni kuonya lakini inaposhindikana ni kutumia nguvu za sheria, sambamba na busara.
 
Kabla ya kuwataka wala rushwa wabadilike, Kikwete abadilike kwanza katika vita hii ngumu dhidi ya rushwa vinginevyo hali itakuwa mbaya.
 
Source: Raia mwema

Thursday, October 25, 2012

STUDY TOUR AT NARUNYU (25/10/12) (PIC AND EXPLANATION)


Today we had another journey with student of certificate from stream B. In this tour student were accompanied by Mr Chihwhalo, Mrs Shomari, Mr Mlanzi and Mr Nangameta, and student were very comfotable as all of them sat in the three minibus hired by them as a part of transport. The purpose of this tour is to get familiar with    how agriiculture centre of Narunyu perfom its several activities of Agriculture. Student had the  opportunity to learn and see exactly what they have been taught, as well as to get new skills in practicals.
 

Agriculture centre of Narunyu has both livestock and crops production , and it has got several tools which are used in production such as chopping machine, tractors, abotours and sealage house. Student  spent much of their time to learn new things and to retrieve materials which they learnt from MATI-Mtwara.

 
Narunyu Saint Mary has 2500 hectares whereby both livestock and crop production projects are implemented. They have 630 cattles for meat production and 50 cattle for milk production. For milk cattle have the ability to produce 150 litres of milk per day, and sent to Lindi region to several customers. These project helps this institute to increase income, to have food security as well as to help society around them.

 
Peace of advice were given out to students upon how to establish projects like of those kind.For establishing new project such as rising livestock for milk production one has to consider water resources, food (feeds) and market. Water and food helps toward initial production, whereas market helps in income generation so as to attain economic gain. Some of the profit is used as scholarship to sisters who need further education and some is saved into bank account.


Problems which face this institute includes: some of their animal got killed (19 cattle killed last time) along the road during grazing time, and some time occurence of foot and mouth desease  cause the loss of these animal.


Students asked so many questions and responded well to the answer which had been provided. This tour is much valuable to them as they can learn as well as see, its better for their memory as they can retrive what they learn much easier, than if they learn without practice.
 
 
 
 
 

Monday, October 22, 2012

ZIARA YA KIMAFUNZO NARUNYU (MAELEZO NA PICHA)

Jumatatu tarehe 22/10/2012, tumekuwa na ziara ya kimafunzo kwa wakurufunzi wa ngazi ya cheti mkondo A, safari hii ilihusisha walimu watatu ambao walifundisha somo la Principal of Agricultura Technology and dissemination na mmoja aliyeambatana nasi kama mlezi.

Walimu hao ni Lucas Chihwalo, Mgeni Shomari pamoja na Mkali Mlanzi, Mwalimu mkude aliambatana na walimu hao kama Mlezi. Wanafunzi walijifunza mambo mengi ikiwamo aina ya ng’ombe wa maziwa waliopo katika kituo cha masista Narunyu. Tulipokelewa vizuri na wageni wetu ambao ni sista Editha Mbunda na Diana Millanzi ambao ndio walikuwa waelekezaji wakuu.

Masista hawa walituonesha mashine inayotumika kukata kata majani yanayotumika kulishia mifugo (chopping Machine). Mashine hiyo ina uwezo wa kukata kata majani na kuwa madogo kabisa hivyo kumuwezesha ng’ombe kula kiurahisi.

Kwa upande wa mifugo tumejionea aina mbili ya Ng’ombe wa maziwa ambao ni jess ambao wana rangi aina ya dark red pamoja na fresian wenye mabaka meusi na meupe. Katika aina hizi mbili fresian ndio hutoa maziwa kwa wingi ukilinganisha na aina nyingine. Kuna changamoto kadhaa zinazofanya mifugo hii isitoe maziwa kwa wingi ama zinazo zoretesha afya za mifugo hii. Mifugo hii huathiriwa kwa kiwango kikubwa na Tsetse fly wanaosababisha ugonjwa wa Typanasimiosis, na kupe wengine wanaosababisha ugonjwa wa ECF. Njia zinazotumika kuzuia magonjwa haya ni njia ya kuosha mifugo hiyo mara kwa mara kwenye josho kubwa lililopo kituoni hapo. Aidha kuna sista ambaye ana elimu ya kutibu mifugo hivyo hutibu mifugo hiyo mara isumbuliwapo na magonjwa hayo.

Kuna karakana kubwa iliyokuwa inatumika kuzalishia umeme kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe (biogas) zamani. Wanafunzi walijionea jinsi kinyesi cha ng’ombe kinavyoweza kutumika kuzalisha umeme kwa mafanikio.

Miradi mingine inayopatikana katika kituo hiki ni kuku wa nyama pamoja na shamba kubwa la miwa, mpunga ndizi pamoja na bustani. Wanafunzi wamejifunza mengi ambayo hayapatikani katika chuo chetu, ni muhimu kwa safari hizi kufanyika kwani huwaongezea ujuzi na uzoefu wanafunzi wetu ambao kwa muda mwingi huwa wanajifunza kinadharia tu na si kivitendo.

Nawasilisha wadau.




 
 


Sunday, October 21, 2012

Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislam Tanzania


Ndugu zangu.

Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.


Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu, wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.


Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana wa jua kali.


Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.


Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia za amani kupata suluhu.


Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.


1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao endana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya ushindani na pia viongozi bora wa dini.


2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa kura za waislamu. Lazima tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm wakapiga kura za kuhadaiwa lakini baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.


3.Bakwata imekuwa ni kama taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao. Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia kurejesha imani kwa bakwata. Napendekeza Qualification ya kuongoza Bakwata iwe ni pdh kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu cha mum kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe shahada moja na kuendelea.


4.Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya. Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya tutawaepuka wale wanao utumia uislamu wetu kama daraja ambalo baadae hutuchafua wote. Mfano wale walio ingia kuchoma na kuvunja kanisa na kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya kanisa na mikate.


"Uislamu ni unadhifu" hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu kipenzi Muhammad S. W. A. Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili tumuenzi kipenzi chetu.

 

Friday, October 19, 2012

Huyu panya atumie namba gani kufikia keki?

Je huyu panya atumie namba ipi kati ya hizo namba 1,2,3. Ili aweze kufkia keki?.
 
Namba ipi itakayo wahi kumfikia Queen?........................ .............1,2,3?

 

Tuesday, October 16, 2012

Afya ya Spika Makinda yazua Utata


na Ratifa Baranyikwa
 
KUNA taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambapo inadaiwa kuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo nchini India.
 
Habari za ambazo gazeti hili limezipata toka nchini India kwa watu wake wa karibu, zimeeleza kuwa Spika amelazwa tangu wiki iliyopita katika hospitali hiyo.
 
Vyanzo vyetu hivyo vilisema, Spika Makinda ameongozana na watu watano ambao wamekuwa wakionekana naye hospitalini hapo.
 
Hata hivyo, gazeti hili halikuweza kufahamu mara moja ugonjwa unaomsumbua kutokana na jambo hilo kuwa siri kati ya mgonjwa na madaktari wake.
 
Taarifa za ndani zinasema kuwa baadhi ya watu waliofika kumuona waliambiwa kwamba anasumbuliwa na macho.
 
Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, alikiri kuwa Spika alikwenda nchini humo kwa shughuli mbili ikiwamo ya kufanya uchunguzi wa afya wa kawaida.
 
Alisema Makinda alikwenda nchini humo mwanzoni mwa mwezi huu kwenye mkutano wa Maspika Wanawake (IPU) na baada ya kumaliza shughuli hiyo ndipo akaenda kufanya uangalizi wa afya yake.
 
Kashilila ambaye hata hivyo alikwepa kuzungumzia kama Spika amelazwa, aliishia kusema tu kwamba alipitia kufanya uangalizi wa kawaida wa afya yake na amekuwa akifanya hivyo kila mwaka.
 
Kwa mujibu wa Kashilila, Spika atarejea wiki ijayo baada ya kumaliza taratibu zote za kuangalia afya yake.
 
Wakati Dk. Kashilila akisema hivyo, mitandao mbalimbali ya intaneti, ilionyesha kuwa mkutano huo wa maspika wanawake ulifanyika kati ya Oktoba 3 hadi 4 mjini New Delhi, nchini humo.
 
Hivyo, endapo Spika alitoka kwenye mkutano na kupitia moja kwa moja kuangalia afya yake, atakuwa ametumia takriban siku 11 hadi kufikia leo.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa kwenye mitandao ya intaneti, katika mkutano huo ambao mada kubwa iliyokuwa ikijadiliwa ni masuala ya jinsia, Spika Anne Makinda, alichangia kuhusu suala hilo akisema wanawake maspika wana jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba mabunge yanazingatia ujinsia.
 
Akichukulia mfano hatua ambazo Tanzania imechukua katika kufanikisha masuala ya kijinsia katika Bunge, Makinda alielezea umuhimu wa maspika wanawake kuhakikisha suala hilo linafanyika kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuanzisha kamati ya usawa wa kijinsia pamoja na suala zima la bajeti sanjari na kuimarisha muundo wa mabunge.
 

Monday, October 15, 2012

Taarifa kwa umma:Madini,mafuta na gesi


Spika wa Bunge Anna Makinda ndani ya wiki moja atumie madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itayoshughulikia masuala ya gesi asili kabla na wakati wa mkutano wa tisa wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 kufuatia hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.

Pamoja na mambo mengine aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu Sekta Ndogo ya Gesi Asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi, madai ya mapunjo ya fedha za mauzo ya Gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.

Hatua hii ni muhimu kufuatia ukimya wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kuhusu kauli yangu ya tarehe 4 Oktoba 2012 ya kutaka Taarifa ya ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 21 Septemba 2012 ifutwe kwa kuwa italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini ilieleza kuwa maandalizi ya sera ya gesi asili yapo katika hatua za mwisho wakati ambapo kamati mbalimbali za kudumu za Bunge hazijahusishwa katika mchakato huo muhimu pamoja na kuwa mamlaka ya kutunga sera kwa mfumo wetu wa sasa ni ya Baraza la Mawaziri hata hivyo kwa unyeti na upekee wake sera ya gesi Spika wa Bunge anapaswa kuwezesha Kamati za Kudumu za Bunge zihusishwe ili pawepo mashauriano na maridhiano kwa mapana na marefu.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini ilieleza kuwa mikataba 26 ya TPDC ni sehemu ya nyaraka muhimu za kuboresha utayarishaji wa sera ya gesi asili, hata hivyo mikataba hiyo imeendelea kuwa siri hivyo Spika aingilie kati kuziwezesha Kamati za Kudumu za Bunge kuisimamia serikali kurekebisha mikataba ya sasa na kuboresha mikataba ijayo kwa Serikali kutekeleza mwito wangu wa toka mwaka 2011 wa kutaka mikataba hiyo iwasilishwe bungeni na iwekwe wazi kwa umma.

Izingatiwe kwamba katika Mkutano wa Nane wa Bunge Spika alitangaza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imevunjwa na kwamba majukumu yaliyokuwa yakishughulikiwa na kamati hiyo yatashughulikiwa na kamati nyingine kwa mujibu wa madaraka na mamlaka ya Spika. Irejewe kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 116 na Kanuni ya 114 fasili ya 14 Spika ana mamlaka na madaraka ya kukabidhi mambo mengine yashughulikiwe na Kamati ya Kudumu ya Bunge nyingine kama atakayoelekeza.

Ikumbukwe kuwa Julai 2011 na Julai 2012 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza namna nchi yetu ilivyojaliwa utajiri wa gesi asilia katikati ya lindi la umasikini wa wananchi na kwamba taifa letu lina fursa ya kuwa nchi kiongozi katika gesi Afrika na kushindana kimataifa ikiwa tutaweka mstari wa mbele upeo, umakini na uadilifu katika sekta ya nishati kuepusha laana ya rasilimali.

Hata hivyo, mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2011/2012 yanaonyesha bado serikali haichukui hatua thabiti kushughulikia ufisadi na udhaifu wa kiuongozi katika sekta ndogo ya gesi asili hivyo hatua za haraka zisipochukuliwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 na kuendelea rasilimali inaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuhatarisha pia usalama wa nchi.

Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza bungeni tarehe 15 Julai 2011 kuhusu tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa mikataba katika sekta ndogo ya gesi inaoihusu pia Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAT) na kutaka kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza suala hilo.

Badala yake Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini uliunda kamati ndogo ya iliyofanya uchunguzi uchunguzi wa masuala husika na taarifa kuwasilishwa bungeni mwaka 2011 ; hata hivyo mpaka sasa maamizio ya bunge kufuatia taarifa hiyo hayajatekelezwa kwa ukamilifu.

Tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa kiasi cha dola milioni 20.1 zilizopunjwa kifisadi hazijareshwa na kuitaka serikali iache kutumia kisingizio cha kuundwa kwa Timu ya Majadiliano (GNT) kuchelewesha utekelezaji wa maazimio, suala ambalo Wizara ya Nishati na Madini itapaswa kueleza hatua iliyofikiwa iwapo Spika atazingatia mwito huu na kuchukua hatua za haraka.

Ifahamike pia kwamba mwaka 2011 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini niliitaka serikali ambazo kuweka wazi bungeni na kwa umma mikataba ya madini, mafuta na gesi asili katika nchini ili kuongeza tija na uwajibikaji.

Aidha nilitoa mwito mwito kwa wananchi na wabunge kuongoza marekebisho ya kikatiba na kisheria ili kuweka vifungu vya kulazimisha uwazi katika mikataba katika hizo muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi.

Uwazi katika mikataba utadhibiti pia mianya ya ufisadi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwa mikataba hiyo itajadiliwa na umma na hivyo kupunguza uwezekano wa viongozi kutanguliza maslahi binafsi na kuwa na mikataba bora ya baadaye yenye kuzingatia maslahi ya umma.

Usiri katika mikataba ni tatizo kwa sababu masharti kama ya kushughulikia madhara ya kimazingira na kuchangia katika huduma za jamii pamoja na kulipa kodi zinazokusudiwa yanaweza yasitekelezwe kwa ukamilifu kama hayatafahamika kwa wabunge na umma.

Aidha, ipo mikataba yenye vifungu ambavyo vinakinzana na sheria nyingine ama vinalinda kupindukia makampuni dhidi ya sheria nyingine za nchi zinazotungwa masuala ambayo yanaingilia mamlaka ya bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Sheria mpya ya madini Tanzania ya mwaka 2010 ina kifungu kinachotaka uwazi hata hivyo kimejikita katika uwazi wa rekodi na ripoti hakijaweka bayana mfumo wa uwazi katika mikataba ya madini, sheria ya mafuta nayo haina kifungu cha uwazi katika mikataba na sheria ya gesi haipo kabisa; hali ambayo inahitaji kurekebishwa.

Pamoja na mapato uwazi katika mikataba utachangia katika kupata tija ya ziada katika uchimbaji kwa kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuweka mfumo mzuri zaidi wa makampuni kununua bidhaa za ndani kwa majibu wa vifungu vya mikataba hali ambacho itawezesha rasilimali kunufaisha wananchi wengi zaidi.

Uwazi katika mikataba utawezesha wabunge na wadau wengine kusimamia ipasavyo taasisi za kiserikali kuhusu mifumo ya kifedha na kibenki ambayo itaongeza mchango wa sekta za nishati na madini katika kuimarisha uchumi kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu wakati huu ambapo thamani ya mauzo imeongezeka duniani lakini mzunguko umejitika katika masoko na mabenki ya nje.

Kwa ujumla, uwazi katika mikataba utapanua pia uwajibikaji wa kuongeza umiliki wa nchi na wananchi wa michakato ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili. Pamoja na kuwa ibara ya nne ya katiba inasema kwamba rasilimali na mali asili zote ziko chini ya usimamizi wa serikali; na ibara ya 63 inaeleza kwamba bunge ndicho chombo kikuu cha kuisimamia serikali kwa kutunga sheria na kupitisha mipango, katiba haijalazimisha mikataba ya madini, mafuta na gesi kuridhiwa na bunge hivyo katika kipindi cha sasa mikataba hiyo iwasilishwe kwa rejea na mapitio.

Katika muktadha huo, tarehe 4 Oktoba 2012 nilimtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo afute taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa lengo la agizo lake la kupitiwa kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ni “kuhakikisha kwamba endapo kuna mapungufu katika mikataba hiyo, mapungufu hayo yasijirudie tena katika mikataba mipya ya baadaye” kwa kuwa ikiachwa ilivyo italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.

Nilieleza kwamba ufafanuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini unatoa mwanya kwa mikataba mibovu kulindwa wakati ambapo kuna madai tuliyotoa toka mwaka 2011 kwamba baadhi ya mikataba hiyo imeingiwa kifisadi na mwaka huu wa 2012 zimeibuka tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji mafuta na gesi asili.

Aidha, pamoja Serikali kuwasilisha bungeni mikataba inapaswa pia kuwasilisha mipango kabambe (master plan) ya mafuta na gesi asili yenye kuzingatia mabadiliko ya kisera na kimfumo yenye kuwezesha nchi na wananchi kunufaika na rasilimali husika.

Kauli hii nimeitoa leo tarehe 14 Oktoba 2012 ikiwa ni Siku ya Kumbukumbu ya Hayati Julius Nyerere ambaye alipinga ufisadi na kutaka rasilimali za nchi zitumike kwa manufaa ya maisha ya wananchi:

John Mnyika (Mb) Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

Friday, October 12, 2012

Vice Presdnt Joe Biden amrudisha Obama mstarini


 
Raisi Obama akifuatilia kwa makini Mdahalo uliowahusisha wagombea wawaili wa umakamu wa raisi Joe Biden wa democrats na Paul Ryan wa Republican. Vituo vingi vinaonesha kuwa Joe Biden ameshinda mahalo huo kwa kiwango kikubwa, kwa kuonesha utulivu mkubwa, kuchambua hoja kwa kina na kuwa na uso wa tabasamu kwa muda mrefu..Ni dhahiri shahiri ushindi huo umemrudisha Obama kwenye nafasi ya kutetea kiti chake baada ya kushindwa kwenye mdahalo wa awali na mgombea wa Republican bwana Mitt Romney.

Wednesday, October 10, 2012

Msisitizo huu wa Zitto Kabwe...



Mh Zitto Kabwe amepost hivi kwenye wall yake ya FB

Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005 — in Kigoma, Tanzania.

Ni ripoti ya kijinga-Mwanakijiji


Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!

Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:

Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?

Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.

Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:
kuzuia shughuli za Siasa (mikutano na maandamano) kipindi cha zoezi la kitaifa la Sensa kuanzia tarehe 25 Agosti 2012 hadi 08 Septemba 2012”. Uhalali wa Amri/Zuio hili ulithibitishwa pia na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika barua yake Kumb Na. DA. 112/ 123/ 01/ 34 ya tarehe 28/08/2010 na wakati wa mahojiano na Kamati ya uchunguzi tarehe 22 Septemba 2012.
 
Kumbe zuio lilihusu "mikutano na maandamano". Kwamba inaweza kujengwa hoja ya kuwa "mikutano" ilimaanisha "mikutano yote" ni vigumu kutetea hasa kwa vile wakati huo huo mikutano mingine ya kisiasa ilikuwa ikifanyika sehemu mbalimbali nchini bila kuzuiwa. Kamati ili kuonesha ulinganifu ingejaribu kutafuta maelezo ya Polisi Zanzibar kwanini waliruhusu CCM kufanya mkutano wake kule wakati kuna zuio. Lakini vile vile ni vigumu kusema kuwa mikutano yote ya kisiasa ya ndani haikuwa imeruhusiwa! Ni vyama vingapi ambavyo vilikuwa na mikutano ya ndani ya kamati zake mbalimbali kati ya August 26-Septemba 8?

Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.

Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?

Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?

Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!

Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:

Kwenye tukio la Nyololo ambapo mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa, mwandishi wa habari mwengine Godfrey Mushi alipigwa na Polisi na inasemekana kujeruhiwa vibaya na baadaye kukamatwa na Polisi.
Huyu Godrey Mushi ni mzima? kwanini alipigwa? Kwanini alikamatwa baada ya kupigwa? Hivi hawa watu hawakuona kuwa kulikuwa na kashfa mbili pale? ile ya Mwangosi na ile ya Mushi? Hivi ingekuwa Mwangosi hajafa pale hii kamati ingechunguza nini kama siyo kupigwa na polisi kwa Mushi?

Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:

"Na hata hii habari ya kifo kimesababishwa na nini - pengine nyinyi mngeitaka zaidi - ipo wameandika lakini siyo kwa 'public consumption' kwa sababu za kisheria. WAmesema nani anaweza kuwajibika hapa wamesema lakini huweza kwenda nayo kwenye press unasema hivi, yule mtuhumiwa ataitumia hiyo kushinda kesi; atasema "nimeshahukumiwa kabla ya kusikilizwa!"... Sisi tukawa badala ya kamati ya kusaidia ndio tunaenda kumtoa mtu hatiani"
Sasa mwenyewe Nchimbi hapa inawezekana aliamini kuwa amezungumza "pointi" sana. Katika mawazo yake haki ya adui yake siyo haki. Kumbe yule mtuhumiwa anayo haki ndio maana mahakamani kwenye kesi hizi wale wa upande wa mashtaka wanatakiwa waweke wazi ushahidi wote ambao wanao hata ule unaoweza kutumiwa kumtoa mtuhumiwa hatiani katika kile kinachoitwa "discovery" kabla ya kesi kuanza. Lengo ni kuhakikisha kuwa ushahidi wowote - wa kumtia mtu hatiani au kumtoa - unawekwa wazi kwa upande mwingine ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapewa nafasi ya haki.

Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?

Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?

Simply put, Ni ripoti ya kijinga.

Source: Jamii forum

Tuesday, October 9, 2012

Ripoti: Kamati ya Nchimbi kuhusu kifo cha mwangosi


TAARIFA YA UCHUNGUZI WA KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN BW. DAUD MWANGOSI

1.0 UTANGULIZI


Mnamo tarehe 03 Septemba mwaka 2012, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (MB) aliteua Kamati ya watu watano kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi, kilichotokea tarehe 02 Septemba 2012, katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa. Kituo cha kazi cha marehemu Daud Mwangosi kilikuwa mkoa wa Iringa ambapo pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa (IPC).

Wajumbe wa Kamati hiyo ni:

Jaji (Mst.) Steven Ihema – Mwenyekiti

Bibi Pili Mtambalike – Mjumbe

Kanali (Dkt. Eng) Wema Wilson Wekwe – Mjumbe

Bwana Theophil Makunga – Mjumbe

Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Juma. Mngulu – Katibu

Sekretarieti ya Kamati ni:

Bi. Edith T. Assenga – Wizara ya Mambo ya Ndani

Bwana Nasoro H. Msumi – Wizara ya Mambo ya Ndani

2.0 HADIDU ZA REJEA

Kamati ilipewa Hadidu za rejea zifuatazo:

- Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa na CHADEMA eneo la Nyololo,Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba, 2012 na kuwepo kwa uvunjifu wa amani.

- Kama yalikuwepo makubaliano au maelekezo kuhusu mikutano ya hadhara au maandamano nchini katika kipindi cha Sensa.

-Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu iliyosababisha kifo cha Marehemu Daud Mwangosi na wengine kuumizwa, na uwiano wa nguvu hiyo na tukio.

-Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha kuna madai ya kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi limepanga kuwashughulikia.

-Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu zinazotoa uwezo kwa Jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama vya Siasa na Mamlaka ya Rufaa endapo vyama hivyo havitaridhika na amri hizo.

-Hali ya Mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa nchini katika Utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.

3.0 MUDA WA UCHUNGUZI

Kamati ilipewa muda wa siku 19 kuanzia tarehe 11 Septemba 2012 iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha Ripoti yake ifikapo tarehe 02 Oktoba 2012.


4.0 NJIA ZILIZOTUMIKA KUFANYA UCHUNGUZI:

4.1 Mahojiano na watu mbalimbali waliokuwepo kwenye tukio.

4.2 Kupitia nyaraka na vielelezo mbalimbali.

4.3 Kutembelea eneo la tukio.

4.4 Majadiliano na vikundi mbalimbali (viongozi wa dini ngazi ya kijiji na wilaya hadi ya mkoa; viongozi wa vyama vya siasa kwenye ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa na Taifa, viongozi wa serikali ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa, Taifa) na wanakijiji wa Nyololo.

5.0 UCHUNGUZI

Kamati ya Uchunguzi ilifanya mahojiano na watu mbalimbali ikiwa pamoja na watendaji wa serikali hususan Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya wilaya Mufindi na mkoa wa Iringa viongozi wa Jeshi la Polisi viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Waandishi wa Habari na wananchi wa kawaida (ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa).

6.0. YALIYOJITOKEZA

Baada ya Kamati kukutana na makundi ya watu mbalimbali katika Mkoa wa Iringa na Viongozi wa Vyama vya Siasa wa kitaifa jijini Dar es Salaam, mambo kadhaa yalijitokeza na baadhi yao ni:

-Hofu ya kutoweka kwa amani miongoni mwa viongozi na wananchi hasa katika mikutano na maandamano ya siasa ambayo yameanza kuota mizizi ya uvunjifu wa amani na mengine kusababisha mauaji. Viongozi na wananchi wengi waliotoa maoni yao mbele ya Kamati wameonyesha hofu kuwa hali hiyo isipodhibitiwa mapema inaweza kulipeleka pabaya Taifa letu.

-Kuna walakini wa mahusiano kati ya waandishi wa habari na Jeshi la Polisi mkoani Iringa.

-Uwepo wa utashi wa makusudi/dhati kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi ya vyama.

-Umuhimu wa Ushirikiano na mahusiano baina ya vyombo vya serikali, vyama vya siasa, wanahabari na wananchi kwa ujumla badala kuonyeshana ubabe ambao umetufikisha hapo.

- Haja ya kufanya mabadiliko ya kisheria katika mfumo wa usimamizi na utendaji wa masuala ya siasa nchini

- Haja ya kuwa na mabadiliko ya kimfumo katika Jeshi la Polisi badala ya ulioko sasa ambao kwa maoni ya baadhi ya watu waliozungumza na Kamati ni wa kitaifa zaidi na kuacha serikali za mitaa bila ya wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao.

-Kwamba nguvu kubwa inatumika na vyombo vya dola/usalama dhidi ya raia na hivyo kupunguza imani ya jamii kwa vyombo hivyo.

-Kupungua kwa maadili/uzalendo miongoni mwa Watanzania kuanzia viongozi hadi wananchi hususan kwenye shughuli za kisiasa.

-Haja ya kusisitiza elimu ya uraia kwa jamii kuanzia kwa watoto hadi kwa watu wazima hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi ili kujenga umoja wa kitaifa.

-Kuwepo kwa mikutano na maandamano ya vyama vya siasa yasiyokuwa na kikomo.

-Muonekano wa Jeshi la Polisi mbele ya jamii.

7.0. MATOKEO YA UCHUNGUZI KUTOKANA NA HADIDU ZA REJEA

7.1 Kuhusu “Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa na CHADEMA eneo la Nyololo, Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba 2012 na kuwepo uvunjifu wa amani”, uchunguzi wa Kamati umebaini yafuatayo:

Tarehe 30 Agosti 2012 CHADEMA iliandika barua, Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mufindi kutoa taarifa kuhusu ratiba ya mikutano ishirini na sita (26) kwenye majimbo ya Mufindi Kusini na Kaskazini tarehe 02-03 Septemba 2012. Awali ratiba ya mikutano hiyo ilikubaliwa, lakini baadaye siku hiyo ya tarehe 01 Septemba 2012 mikutano hiyo ilisitishwa kwa barua Kumb. Na MFG/A.24/9/54 kutokana na kuongezwa siku za zoezi la Sensa ya watu na Makazi hadi tarehe 08 Septemba 2012.

CHADEMA walikataa kusitisha ratiba ya mikutano hiyo kama inavyothibitishwa na Justin Leornard Mpotwa Katibu wa Wilaya ya Mufindi kwa barua yake Kumb. Na CDM/M4/002/Vol.01/2012 ya tarehe 01 Septemba 2012 kuwa “pia tunaomba ieleweke bayana kwamba kisheria shughuli zetu hazina mwingiliano na wala kuhusiana na program iliyoongezwa ya Sensa. Kwa barua hii tunakuarifu kuwa mikutano tuliyokutaarifu kuifanya kuanzia kesho tarehe 02 septemba 2012 itaendelea kama ilivyopangwa – CHADEMA VEMA”.

Aidha kuwepo kwa zuio la mikutano ya Siasa ya CHADEMA Mkoani Iringa wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linathibitishwa na Amri ya Utendaji (Operation Order) ya Kamanda wa Polisi Mkoa (SACP Michael Kamuhanda) ya tarehe 01 Septemba 2012. Amri ya Utendaji ambayo ni amri halali ilitolewa ili “kuzuia shughuli za Siasa (mikutano na maandamano) kipindi cha zoezi la kitaifa la Sensa kuanzia tarehe 25 Agosti 2012 hadi 08 Septemba 2012”. Uhalali wa Amri/Zuio hili ulithibitishwa pia na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika barua yake Kumb Na. DA. 112/ 123/ 01/ 34 ya tarehe 28/08/2010 na wakati wa mahojiano na Kamati ya uchunguzi tarehe 22 Septemba 2012.

Licha ya zuio/amri hii Viongozi wa CHADEMA walikataa kutii amri hiyo. Kutokana na taarifa hizi, Kamati ya Uchunguzi inathibitisha kwamba hapakuwepo na uhalali wa mkusanyiko/mkutano ulioitishwa na CHADEMA eneo la Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba 2012. Kuhusu kuwepo kwa uvunjifu wa amani Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012 Kamati ya Uchunguzi ilibaini mambo yafuatayo:

-Tukio la kuuawa kwa Daud Mwangosi jioni ya tarehe 02 Septemba 2012 lilitokea baada ya Operesheni ya Jeshi la Polisi kumalizika. Hii ni kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa na Joseph Senga Mpiga picha/Mwandishi Tanzania Daima.

- Kitendo cha kutotii amri halali ya Kamanda wa Polisi kuagiza wafuasi wa CHADEMA watawanyike kutoka kwenye eneo la ofisi ya Kata ya CHADEMA ilikuwa chanzo cha vurugu.

Uamuzi wa CHADEMA kung’ang’ana kukusanyika isivyo halali eneo la Nyololo ikizingatiwa kuwepo kwa ujumbe wa SMS kutoka kwa Dkt. Slaa, Katibu wa CHADEMA uliosema, “IGP nasubiri simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha. Mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Den Hague. Ni afadhali tufe kuliko manyanyaso haya”. Dr. Slaa. : ujumbe huu ukiashiria umwagaji wa damu ni ushaidi tosha kuwepo kwa uvunjifu wa amani. CHADEMA ndiyo Chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012.

7.2 Kama yalikuwepo makubaliano kuhusu mikutano ya hadhara au maandamano nchini katika kipindi cha Sensa. Katika kuzungumzia hoja hii tukianzia na Uongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa, Kamati ya Uchunguzi ilithibitisha kuwepo kwa maagizo ya kusimamisha mikutano/maandamano ya Vyama vya Siasa wakati wa kipindi cha Sensa ya Watu na Makazi yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, na kuongezwa muda wa Sensa hadi tarehe 08 Septemba 2012 na Kamishna wa Sensa hapo tarehe 01 Septemba 2012.

Aidha hoja hii imethibitika kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa barua yake yenye Kumb Na DA. 112/ 01/ 34 ya terehe 28 Agosti 2012 kwenda kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa akiwasihi kusimamisha shughuli zote za mikutano na maandamano ya Vyama vyao kwa kipindi chote cha Sensa ya Watu na Makazi. Aidha kwa mujibu wa Gazeti la Serikali Na 29 VOL 93 ya tarehe 20 Julai 2012, Mhe. Rais, JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu namba 14 cha Sheria ya Takwimu sura 351 alielekeza kwamba Sensa ya Watu na Makazi itafanyika kuanzia tarehe 26 mwezi wa nane, mpaka tarehe 08 mwezi wa tisa mwaka 2012.

Kamishna wa Sensa aliratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kumalizika ifikapo tarehe 01 Septemba 2012. Hata hivyo kutokana na tathmini aliyofanya, kazi hiyo ilikuwa imekamilika kwa asilimia 95%. Hivyo tarehe 01 Septemba 2012 alitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kwamba ili kila mwananchi apate nafasi ya kuhesabiwa watu watakaokuwa wamesalia ambao ni chini ya 5% wanaombwa kutoa ushirikiano ili zoezi hili likamilike. Hivyo, wale wote mmoja mmoja waliobakia wataendelea kuandikishwa hadi tarehe 08 Septemba 2012.

Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ujumbe wa simu Kumb Na S8.7/ 2/ A/ VOL XIV/ 59 ya tarehe 28/08/2012, pia simu yake Kumb Na C.28/ B/ 44 ya terehe 01/ 09/ 2012 aliwaelekeza Makamanda wa Polisi wa Mikoa kutoruhusu mikutano na maandamano wakati huu wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mpaka litakapokamilika tarehe 08 Septemba 2012.

Kimsingi Kamati ya uchunguzi imethibitisha kwamba maelekezo kwa Vyama vya Siasa kutoendesha shughuli za mikutano ya hadhara au maandamano yalitolewa kwa mujibu wa Sheria.

7.3 Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu iliyosababisha, kifo cha marehemu Daud Mwangosi na wengine kuumizwa, na uwiano wa nguvu hiyo na tukio.

Hoja kuwa Polisi walitumia nguvu kubwa katika kudhibiti mkutano wa CHADEMA iliungwa mkono na Viongozi wa Serikali ya Kijiji, Viongozi wa dini na Viongozi wa siasa Kijijini Wilayani na Mkoani pamoja na Waandishi wa Habari. Hata hivyo Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya na Mkoa na Viongozi wa Jeshi la Polisi waliona nguvu hizo ni za mazingira ya hali ilivyokuwa.

Uchunguzi wa suala hili umebaini kwamba tarehe 02 Septemba 2012 muda wa saa 10 za jioni huko eneo la Sokoni, Kijiji cha Nyololo kulikuwepo na mkutano usio halali ulioandaliwa na viongozi wa CHADEMA. Upo ukweli kwamba uongozi wa Polisi ulitoa ilani kuamuru wafuasi wa CHADEMA waliokuwepo mkutanoni hapo waondoke la sivyo nguvu itatumika. Walikaidi amri hiyo na ilipoagizwa viongozi wakamatwe ndipo walianza kurusha mawe kwa Askari Polisi. Baadhi ya Askari walijeruhiwa, akiwamo G 9934 PC Mgaka alivunjwa mkono wa kulia. Pia kofia (helmet) tatu ziliharibiwa.

Kutokana na hali hiyo amri ya kupiga mabomu ya machozi na ya kishindo ilitolewa, kwa mujibu wa Kifungu 77 hadi 79 cha Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 – R.E 2002. Operesheni hii ilimalizika baada ya kukamatwa viongozi na wafuasi wa CHADEMA jumla yao saba.

Baada ya zoezi hilo kukamilika Askari Polisi walioshiriki kwenye Operesheni waliamriwa kuingia katika magari tayari kwa kuondoka. Wakati Askari wakipanda kwenye magari kishindo kikubwa kilitokea umbali wa zaidi ya mita 100 kutoka sehemu ambayo operesheni ilikuwa inafanyika na iligundulika kwamba kishindo kile kimesababisha kifo cha Mwandishi wa Habari Daud Mwangosi.

Upelelezi wa awali pamoja na picha za mnato unaonyesha kwamba marehemu alikuwa amemkumbatia Mkuu wa Polisi Kituo cha Mafinga ASP Assel Mwampamba na huku akiwa amezungukwa na Askari Polisi wasiopungua sita ambao licha ya kumzunguka marehemu Daud Mwangosi kuna madai yaliyotolewa na mwandishi wa Habari Joseph Senga kwamba, Askari Polisi hao walikuwa wanamshambulia marehemu kwa kumpiga, ndipo askari mmoja aliyetambuliwa kuwa ni G 2573 PC Pasificus Cleophace Simon alifyatua Bomu la kishindo na kusababisha kifo cha Daud Mwangosi.

Tukio hili linaweza kugawanyika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ni wileamapamebas(mni ya kutawanya watu na ya pili ni ile ya mauaji ya Daud Picha Namba 15: Askari Polisi wakimpiga Marehemu Daud Mwangosi, huku OCS M wenye kifimbo) akijaribu kuwazuia. Mwangosi. Katika tukio la kwanza idadi ya Askari walioshiriki ni Sekisheni Tukio hili linaweza kugawanyika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ni lile ya Operesheni ya kutawanya watu na ya pili ni ile ya mauaji ya Daud Mwangosi.

Katika tukio la kwanza idadi ya Askari walioshiriki ni Sekisheni tatu ambapo ni askari wasiozidi thelathini. Kwa maelezo yaliyotolewa na Mwandishi wa Habari mbele ya Kamati, Bw Joseph Senga anaeleza kuwa watu walishatawanyika na hali kutulia mara baada ya Operesheni hii kukamilika na Polisi kujiandaa kuondoka kwenye eneo la tukio. Tukio la mauaji ya Daud Mwangosi lilisababishwa na kupigwa bomu la kishindo.

Maswali ya kujiuliza katika tukio la mauaji ni Je, kulikuwepo na uwiano unaolingana na tukio hili?, Je Palikuwa na uhalali wa kutumia Bomu la kishindo?, na Je, utumiaji wa Bomu hilo ulikuwa na umuhimu?

Kulingana na tukio lenyewe majibu ya maswali hayo ni kama ifuatavyo:

-Hapakuwa na uwiano wa Bomu na tukio la mauaji, kwa vile utaratibu wa matumizi ya bomu hilo unaelekeza kulenga juu usawa wa nyuzi 45 na umbali mita 80 mpaka mita 100.

-Hapakuwa na uhalali wa kutumia Bomu la Kishindo kwani lengo la ulipuaji wake ni ili watu waogope na kukimbia.

- Hapakuwepo umuhimu wa kutumia Bomu la Kishindo kwa sababu hata ingekuwa ukamataji tayari Askari Polisi wapatao sita walikuwepo eneo la tukio.

Kwa misingi hiyo Kamati imeona kwamba nguvu iliyotumika mwanzo hadi kumaliza Operesheni haikuwa kubwa. Kuhusu tukio la kuuawa Bw. Daud Mwangosi na kuumizwa baadhi ya Askari Polisi halikustahili kabisa.

7.4 Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha madai ya kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi limepanga kuwashughulikia.

Katika kupata ukweli wa jambo hili, Kamati ilikutana na wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa na pia iliwahoji Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, Nyigesa Ramadhani Wankyo na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani Iringa Said Abdallah Mnunka.

Pia, wakati Kamati inakutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, ilileta suala la mahusiano kati ya Polisi na waandishi wa habari na watendaji wakuu wa serikali wa mkoa wa Iringa.

Katika mkutano na waandishi wa habari, ilionekana kuwa katika thathmini yao uhusiano kati yao na Polisi hapo mkoani ni mbaya sana. Walieleza matukio kadhaa ya kunyanyaswa waandishi wa habari wakati wapo kazini, ikiwamo kupigwa, kutishiwa kuharibiwa na kuharibiwa vifaa vyao vya kazi na hata kutishiwa maisha ili wasiripoti mambo ambayo Polisi wana maslahi nayo.

Kwa mfano, mwandishi wa habari wa Star TV, Oliver Moto alieleza Kamati kuwa: “Waandishi wa habari hawana mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi, na hata wanapofika ofisi za Polisi huwa hawapewi ushirikiano. Kutokana na uhusiano mbaya wanahabari walifanya maandamano tarehe 06 Machi 2012 kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na Jeshi la Polisi hapa Iringa”.

Mwandishi mwingine wa habari Zulfa Shomari ambaye anaandikia gazeti la Mwananchi alieleza kuwa kuna matukio kadhaa ambayo Polisi wamewazuia waandishi kufanya kazi zao mojawapo ni lile ambalo Polisi walikataza kupigwa picha tukio la kukamatwa kwa pembe za ndovu.

Kamati pia iielezwa na mwandishi wa habari wa ITV, Bw. Laurian Mkumbata mkasa wa kuvunjwa kamera yake na OCD Iringa kwenye tukio moja. Ilibidi OCD alipe kamera hiyo kwa maagizo ya RPC.

Pia walisema kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa hivi sasa ana mawasiliano duni sana na waandishi wa habari na juhudi za wengi wao kumfuata ili athibitishe tukio zimekuwa zikishindwa kwani ameweka maagizo getini kuwa mtu yeyote ambae anataka kumuona ni lazima aeleze anataka kumuona kwa sababu gani ndipo aruhusiwe kuingia. Kwa sababu hii waandishi wa habari wengi wamekata mguu kwenda ofisini kwake.

Mwandishi mmoja wa Ebony FM Bw. Raymond Francis, aliiambia Kamati kuwa yeye binafsi alitishiwa kuuawa na baada ya kuandaa kipindi kuhusiana na watu wanaoshukiwa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya ambao wanahusiana na baadhi ya Polisi wasio waadilifu.

Mwandishi wa Habari Greyson Mgoi wa gazeti la Kwanza Jamii aliiambia Kamati kuna tukio la kuanguka kwa lori la mafuta eneo la Ifunda karibu na Mafinga ambapo waliwakuta wananchi na polisi wakichota mafuta kutoka kwenye hilo gari.

Alisema kuwa waliamua kupiga picha tukio hilo lakini Polisi waliwakamata na kuwalazimisha wafute hizo picha walizopiga. Kwa kuogopa shari walikubali kuzifuta na wakaruhusiwa kuendelea na safari yao.

Waandishi wa Habari hata hivyo walibainisha kuwa uhusiano wao na Polisi hapo mkoani ulikuwa mzuri sana kipindi cha uongozi wa RPC Advocate Nyombi. Walisema kuwa wakati wa RPC Nyombi, alikuwa na utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari na pia alikuwa anafikiwa na waandishi wa habari kwa urahisi kwa simu au ofisini kwake. Walisema lakini ulianza kuharibika alipohama na nafasi yake kuchukuliwa na RPC Mangara na kuwa mbaya zaidi alipokuja Kamuhanda. Walidai kuwa Polisi wa Iringa si waadilifu na wamekuwa wakijiona kama miungu watu.

Waandishi walieleza Kamati, kitu kilichowaudhi sana ni yale majibu yaliyotolewa na RPC baada ya mauaji ya Daud Mwangosi ambayo yalionekana yalikuwa ni ya kupanga ili ukweli usijulikane. Walisema kama si picha zilizotolewa na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye tukio, hawadhani kama umma wa Watanzania wangepata ukweli wa tukio hilo.

Walisema tarehe 06 Machi 2012, walifanya maandamano ili kupinga manyanyaso ya Polisi wa mkoani Iringa yaliyopokelewa na Mkuu wa Mkoa. Waandishi wa Habari mkoani Iringa pia walionyesha masikitiko yao kuwa tangu kutokee kwa mauji ya Daud Mwangosi, hawajapokea pole kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na watendaji wake wa juu hata kama ni ya “kinafiki”.

Kwa upande wa pili, yaani Jeshi la Polisi, Kamati ilipata taswira tofauti. RPC Kamuhanda alisema kuwa yeye anaona mahusiano ya Polisi na waandishi wa habari kwa ujumla ni mzuri na yeye binafsi amekuwa akikutana na waandishi wa habari takriban kila siku asubuhi saa nne kuwapa habari. Pia aliiambia Kamati kuwa waandishi wa habari walishiriki kikamilifu katika kuripoti michuano ya mpira ya Kikombe cha Kamuhanda yaliyofanyika mjini Iringa.

Msimamo huo pia ulichukuliwa na viongozi wa juu wa kiutawala akiwemo Mkuu wa Mkoa Dkt. Christine Ishengoma, Katibu Tawala wa Mkoa Bibi Getrude Mpaka ambao walisema kuwa hapakuwa na uhasama wowote kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa Habari. Wote wawili walisema kuwa walimfahamu marehemu Daud Mwangosi na aliteuliwa katika kamati kadhaa za kimkoa ikiwa ni pamoja na ile ya kuandaa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani, Kamati ya Masuala ya Katiba ya Mkoa na Kamati ya Kukuza Utalii ya Mkoa.

Kuhusiana na hisia kuwa Mkuu wa Mkoa na watendaji wake hawakujumuika na waandishi katika msiba wa Daud Mwangosi, Dkt. Ishengoma alisema si kweli hawajatoa rambirambi zao kwa kifo cha Mwangosi lakini alitoa pole kwa waandishi wakati ameenda na IGP Mwema kijijini Nyololo na pia kupitia radio katika kipindi kilichotayarishwa na mwandishi wa habari Francis Godwin.

Baada ya kuongea na pande hizo mbili, Kamati imebaini kwamba kuna walakini wa mahusiano kati ya waandishi wa habari na baadhi ya askari polisi mkoani Iringa. Kuhusu madai ya kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao jeshi la polisi limepanga kuwashughulikia.

Kwenye tukio la Nyololo ambapo mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa, mwandishi wa habari mwengine Godfrey Mushi alipigwa na Polisi na inasemekana kujeruhiwa vibaya na baadaye kukamatwa na Polisi.

Kwa mujibu wa Joseph Senga mpiga picha/mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima ambaye alikuwepo kwenye tukio na kupiga picha, alimuona marehemu akipita nyuma ya gari moja la Polisi ambalo lilikuwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA. Punde tu alimwona mtu amezungurukwa na askari akipigwa lakini hakujua ni nani na yeye aliendelea kupiga picha tukio hilo mpaka nae alipokamatwa na Polisi watatu ambao walimwuliza kama nae anataka aende kuungana na mtu anayepigwa pale.

Senga alisema wakati kipigo kinaendelea, kuna askari mmoja mwenye nyota tatu (OCS Mwampamba) aliteremka kutoka kwenye gari na kwenda pale ambapo Yule mtu aliyekuwa anapigwa huku akiwaambia “mwachieni, mwachieni, namfahamu mimi huyo ni mwandishi wa habari!”

Senga alisema mara alisikia kishindo kikubwa na wale askari ambao walikuwa wanamshikilia walikimbia ndipo yeye akaendelea kupiga picha sasa za marehemu Daud Mwangosi ambaye alikuwa amekwisha sambaratishwa na bomu. Alieleza kuwa alimsikia yule askari ambaye alikuja kumsaidia marehemu Mwangosi akisema “afande wameniuwa”, “afande wameniuwa”, akimwambia RPC ambaye alikuwa karibu nae kwani nae aliumizwa vibaya katika mlipuko huo. Senga aliiambia Kamati wale wote ambao walikuwa wame mzunguka marehemu kama wanavyoonekana kwenye picha alizopiga walikuwepo wakati anapigwa.

Maelezo ya Bw. Senga yanatofautiana sana na yale yaliyotolewa na RPC na OC FFU kuwa Marehemu alimvamia OCS Mwampamba na kuwa wale askari huenda walidhania kuwa mkubwa wao alikuwa amevamiwa ndipo walipoamua kwenda kumsaidia. OCS Mwampamba mwenyewe wakati akihojiwa na Kamati ilipokuwa Mafinga alisema hakumbuki kitu.

Hata hivyo, kwa maelezo ya Bw. Senga, ambayo yanakubaliana na yale ya RPC na OC-FFU, kitendo cha kupigwa na mauaji ya marehemu Daud Mwangosi kilitokea baada ya kuisha ile operesheni ya kusambaratisha mkutano wa CHADEMA na hapakuwa na mabishano yeyote au purukushani iliyotokea kabla ya marehemu kuzungukwa na kuanza kupigwa.

Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?

Kwa nini kuna maelezo yanayokinzana kati ya Bw. Senga ambaye alikuwa karibu sana na tukio na yale ya RPC na OC-FFU ambao katika maelezo yao kwa Kamati walisema kuwa wao walikuwa mbali kidogo na tukio kwa hiyo hawakuweza kuona kwa dhahiri kilichotokea. Maelezeo ambayo yalirudiwa na viongozi wa juu wa Polisi ikiwa ni pamoja na Kamishna wa Upelelezi (DCI) Robert Manumba na Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema katika mahojiano na Kamati.

Uchunguzi wa Kamati haukuweza kupata ushahidi wa kubainisha kama kupigwa kwa waandishi hao kulitokana na njama yeyote ya Polisi kuwashughulikia au ilitokea kwenye purukushani ya vurugu zilizotokea baada ya FFU kuamriwa kutawanya wanachama wa CHADEMA.

Pia Kamati haikupata ushahidi wowote wa kuonyesha kuwa mauaji ya Daud Mwangosi yalikuwa ni ya kupangwa. Kutokana na maelezo ya hapo juu, Kamati inapendekeza yafuatayo:-

-Taasisi za habari zinazosimamia maadili na weledi wa vyombo vya habari, hususan Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri wafanye utaratibu unaostahiki za upatanishi kati ya waandishi wa habari, Jeshi la Polisi na uongozi wa mkoa wa Iringa. Hii itasaidia kurejesha uhusiano mzuri kati ya vyombo hivyo muhimu katika mkoa;

-Waandishi wa habari wapewe mafunzo ya jinsi ya kuripoti matukio ya hatari/ghasia;

-Waandishi wa habari wavae vivazi maalum vya kuwatambulisha wakiwa katika matukio hasa kwenye maeneo hatarishi;

- Waandishi wa habari wafanye kazi kwa weledi, uadilifu, uwazi na wasijibainishe na vyama vya siasa;

- Polisi ambao walihusika katika kumpiga marehemu Daud Mwangosi kabla hajauawa wachukuliwe hatua stahiki za kisheria;

- Kamati ya Ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari iliyoanzishwa mwaka 2008 ifufuliwe. Na kamati hizo ziteremke hadi kwenye ngazi ya mkoa kama ilivyokuwa awali.

- Viongozi wa polisi wanapotoa taarifa za tukio, ziwe zimefanyiwa utafiti wa kina ili zisipotoshe jamii.

7.5 Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu zinazotoa uwezo kwa Jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama vya Siasa na Mamlaka ya Rufaa ambapo Vyama hivyo havitaridhika na amri hiyo.

Sheria Namba 5 ya 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 7 ya 2009 inaratibu mahusiano ya kiutendaji kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa. Kwa mujibu wa Sheria hii Jeshi la Polisi limepewa madaraka ya kutoa zuio kwa maandishi na kuweka bayana sababu za kuzuia mikutano au maandamano. Zuio aina hii ni halali kwa mujibu wa Sheria na ni sherti Chama cha Siasa kiheshimu na kutii. Fungu la 11 vifungu vidogo Na 1, 4, 5, 6, 7 na 8 ya Sheria ya Vyama vya Siasa likisomwa pamoja na mafungu Namba 43, 44, 45 na 46 ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Auxiliary Forces Act Sura 322 vitatumika kusimamia uendeshaji mikutano ya Vyama vya Siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na kwamba Vyama vya Siasa vinatakiwa kutoa taarifa na siyo kuomba idhini, Jeshi la Polisi limepewa uwezo na madaraka juu ya mikutano hiyo kuhusu kuzuia au kuruhusu na au kutoa maelekezo stahiki, kama vile kupendekeza, na kushauri eneo mbadala na tarehe tofauti ya kufanya mikutano/maandamano.

Aidha kutotii amri/zuio ya Jeshi la Polisi ni kosa la Jinai kwa mujibu wa Fungu la 74 la Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 RE.

Vilevile kwa mujibu wa Fungu la 43 (6) ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Auxiliary Forces Act, Waziri wa Mambo ya Ndani ndiye Mamlaka ya Rufaa dhidi ya amri/zuio linatolewa na Jeshi la Polisi.

Pamoja na kuwepo kwa Sheria hizi mbili bado kuna mapungufu katika uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Siasa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Kwa mfano pamoja na madaraka aliyonayo Msajili wa Vyama vya Siasa ya kukifuta Chama cha Siasa kwenye rejesta ya usajili kwa mujibu wa Fungu la 19 na 20 ya Sheria ya Vyama vya Siasa, kusimamisha utoaji wa ruzuku na matumizi yake, uratibu wa shughuli za vyama hivyo hauko mikononi mwake.

Wadau wanashauri umuhimu wa kuimarisha uhusiano katika shughuli za utendaji kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi ili kudumisha utulivu na amani na utii wa sheria bila shuruti kwa upande mmoja na kukuza mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa kwa upande mwingine.

7.6 Hali ya mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa nchini katika utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.

Kamati ya Uchunguzi wa Kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi katika kupata majibu kwa hadidu hii ya rejea, ilizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kutoka ngazi za Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa na Viongozi wa kitaifa jijini Dar es Salaam na viongozi wa dini kutoka ngazi za Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa.

Kwa ujumla, kila kiongozi wa chama cha siasa wa ngazi zote ambaye Kamati imezungumza naye kuhusu hadidu hii ya rejea, ameelezea umuhimu wa Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao na wangependa jeshi hilo liachwe huru katika kutekeleza majukumu yake bila ya kuingiliwa na wanasiasa ili lifanye kazi zake kwa weledi na uadilifu.

Hata hivyo taswira iliyojitokeza ni kwamba kuna mgawanyiko wa mtizamo kuhusu jinsi Jeshi la Polisi linavyoshughulikia mikutano/maandamano ya Vyama vya Siasa.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaamini kuwa Jeshi la Polisi linakipendelea Chama cha Mapinduzi na kubinya vyama vya upinzani, huku viongozi wa CCM kutoka ngazi ya kijiji hadi Taifa wakilisifia Jeshi hilo kuwa linafanya kazi yake vizuri na kwa weledi mkubwa.

Mgawanyiko wa taswira kuhusu madai kuwa Jeshi la Polisi kuipendelea CCM hauko tu kati ya vyama vya upinzani na CCM bali pia kwa viongozi wa dini kuanzia ngazi za kijiji, wilaya hadi mkoani Iringa kwa maelezo kuwa hawajasikia hata siku moja mtu anauawa na Polisi kwenye mkutano wa CCM. Mwandishi mmoja alitoa udadisi wake kuwa huwa wanapata shida sana kuandika habari za mikutano ya CHADEMA kutokana na jinsi Polisi wanavyojipanga kwenye mikutano ya chama hicho.

Kudhihirisha umuhimu wa Jeshi la Polisi katika jamii, hata wale wanaolituhumu kuwa linakipendelea CCM, katika kutoa maoni yao kuhusu hatua za kuchukuliwa askari wanaoharibu sifa ya Jeshi hilo, wanapendekeza kuwa askari wahusika wachukuliwe hatua na kuomba Jeshi hilo liendeshwe kwa weledi hasa inapotokea askari akalazimika kutumia silaha kukabiliana na fujo isifikie kuua.

Kwa mfano, Mchungaji Peter Katanga wa Revival Baptist Church, alishauri chombo cha Polisi kisitumike kufanya mauaji, au kisitumike na mtu, watu, au kikundi chochote kufanya matendo yasiyo mazuri kwa jamii kwa sababu chombo hicho kipo kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wote na mali zao.

Viongozi wa siasa wengine bila kujali itikadi zao, wameonekana kukerwa sana na tabia ya watu kuuawa wakati Jeshi la Polisi linatuliza ghasia na hii ikiachiwa iendelee inaweza kuleta uvunjifu wa amani katika nchi. Kwa mfano, Mchungaji wa Kanisa la EFATA Nyololo, Mkombozi Kiliwa alishauri Polisi watumie njia zinazofaa kukabiliana na wanaovunja sheria na si kuua.

Pia Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyololo, Obby Kimbale, alielezea kutokukubaliana kwake na kitendo cha mauaji ya Daud Mwangosi, alipendekeza elimu ya uraia itolewe kwa jamii nzima vikiwemo vyombo vya dola, viongozi wa serikali, wanasiasa na wananchi kwa ujumla wao ili kila mtu kwa nafasi yake akaelewa namna ya kutimiza wajibu wake ndani ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.

Kwa upande mwingine, wengi waliotoa maoni yao juu ya mahusiano ya Polisi na vyama vya siasa, pamoja na kulaumu Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa katika kukabiliana na wafuasi wa CHADEMA, pia waliwalaumu viongozi wa chama hicho, kwa kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi hatimaye kusababisha Polisi kutumia nguvu kiasi hicho.

Kitendo cha kuuawa kwa Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi na tabia ya kutokea mauaji katika mikutano ya CHADEMA kimeonekana kuwakera viongozi wengi wa vyama vya siasa kwani wanaamini kuwa Polisi huwa wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi ‘wanapotuliza ghasia’ katika mikutano ya CHADEMA.

Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa, Zakaria Mwansasu alielezea sababu ya matukio ya namna hii kuwa ni kutokana na mmomonyoko aliouita mkubwa wa maadili hasa katika vyama vya siasa na akashauri viongozi wa vyama vya siasa wakapewa elimu ya uraia.

Maoni mengi ya viongozi wa vyama vya siasa yamejikita zaidi katika hofu ya nchi kuingia kwenye vurugu na kutoka kwenye kisiwa cha amani na hivyo kutoa uashauri kwa viongozi wa vyama vya siasa na Jeshi la Polisi kuweka mbele maslahi ya taifa.

Mchungaji Yokonia Koko wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), alielezea ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari Polisi kuwa umetokana na jeshi hilo kuajiri vijana ambao hawana maadili na kwamba watuhumiwa wa mauaji kwenye matukio yanayolihusisha Jeshi la Polisi wakati wa kuzuia fujo katika mikutano/maandamano ya vyama vya siasa wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa askari wengine.

Kasi ya CHADEMA kuendesha mikutano katika sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kujiimarisha kichama, imepokewa kwa hisia tofauti na vyama vingine vya siasa. Wakati kuna makundi ya watu katika jamii wakidhani kuwa hiyo ni haki yao kama chama cha siasa kinachotaka kukua na kukubalika kisiasa, wengine wanaiona mikutano hiyo ya hadhara ya CHADEMA kama ni kuwapunguzia muda wa kufanya shughuli zao za maendeleo hasa baada ya kipindi cha uchaguzi kumalizika.

Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, alishauri kufanyiwa marekebisho kwenye sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992 itakayoweka wazi shughuli za vyama vya siasa baada ya Uchaguzi Mkuu. Alisisitiza kuwa shughuli za siasa baada ya Uchaguzi Mkuu zihamie bungeni kwa wanasiasa kuhoji mipango ya maendeleo ya serikali na matumizi ya rasilimali za nchi na wananchi waachwe wachape kazi zao za maendeleo.

Kuhusu Jeshi la Polisi, Mukama alisema mfumo uliopo wa Jeshi hilo unalifanya lionekane la kitaifa zaidi na kushauri libadilishwe kimuundo ili liweze kutandaa hadi serikali za mitaa kuongeza nguvu katika mpango wa ulinzi shirikishi ulioanzishwa na Jeshi hilo.

Mwanasiasa John Shibuda alizungumzia mahusiano kati ya vyama vya siasa na Jeshi la Polisi kwa kutoa lawama kwa vyama vya siasa kuwa havitoi malezi kwa wanachama wake ambayo yatawafanya wawe waadilifu, wazalendo, waaminifu na watiifu wa sheria.

Alisema vyama vya siasa havina mfumo wa kujihakiki, kujikosoa na kujiwajibisha na akapendekeza kuanzishwa kwa mfumo huo kisheria ambao utawajibisha vyama vya siasa kwa matendo ya viongozi au wanachama wao.

Shibuda alifafanua kwamba sheria anayopendekeza iwe na nguvu ya kutoa adhabu kwa chama cha siasa na kwa kiongozi au mwanachama ambaye atathibitika kuwa ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.

Kuhusu Jeshi la Polisi mwanasiasa huyo alipendekeza kufanyike kwa marekebisho ya utendaji ili wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe nguvu za kiutawala ambazo huwafanya wakati mwingine kutoa maagizo ya kisiasa kwa Jeshi la Polisi na hatimaye kulifanya Jeshi hilo lionekane linatekeleza maslahi ya wanasiasa badala ya kuwa chombo cha kulinda amani.

Kwa ujumla Kamati kutokana na maelezo mbalimbali ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi, imeona kuwa kuna mahusiano hafifu kati ya baadhi ya Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi.

Kwa kuwa taasisi zote hizi ni wadau muhimu wa amani na utulivu nchini, Kamati inapendekeza:

-Kuwe na jukwaa la mazungumzo ya mara kwa mara kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa ili kila upande ujue wajibu wake na wa taasisi nyingine katika kudumisha amani ya nchi na utamaduni wa kuheshimu sheria zilizopo na kupunguza migongano.

-Kuhusu madai kwamba mauaji yanayotokea nchini yaundiwe Tume, Kamati imeona kuwa zipo sheria zinazotoa mamlaka ya kutafiti au kuchunguza endapo kuna mashaka ya kifo hicho.

-Muundo uliopo wa Jeshi la Polisi uangaliwe upya kisheria ili kuziba mianya inayotoa nafasi kwa wanasiasa kulitumia Jeshi hilo kwa manufaa ya kisiasa.

-Nafasi za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kiutendaji ziangaliwe upya ili zisitumike na mhusika kwa ajili ya manufaa ya kisiasa.

-Kwa kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwa ndiye mlinzi wa usalama wa raia na mali zao, siasa za ubabe kwa vyama vya siasa ziepukwe kwa kuwa zinaleta msuguano usio wa lazima na Jeshi la Polisi

8.0. MAONI NA MAPENDEKEZO:

Kutokana na uchunguzi uliofanyika kupitia mahojiano na Viongozi wa kada mbalimbali, kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya, Mkoa hadi Taifa, Kamati ina maoni na mapendekezo yafuatayo:

MAONI:

-Kuhusu madai kwamba mauaji yanayotokea nchini yaundiwe tume, Kamati imeona kuwa zipo sheria zinazotoa mamlaka ya kutafiti au kuchunguza endapo kuna mashaka ya kifo hicho.

-Nafasi za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kiutendaji ziangaliwe upya ili zisitumike na mhusika kwa ajili ya manufaa ya kisiasa.

-Kwa kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwa ndiye mlinzi wa usalama wa raia na mali zao, siasa za ubabe kwa vyama vya siasa ziepukwe kwa kuwa zinaleta msuguano usio wa lazima na Jeshi la Polisi

-Kuhusu operesheni ya uzuiaji wa mkutano wa CHADEMA usio halali Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012, Jeshi la Polisi lilitekeleza wajibu wake ipasavyo na kutumia nguvu sahihi. Operesheni iliyoandaliwa na kufanyika ilikamilika kwa kuwatawanya watu waliofika kwenye mkutano, kukamata baadhi ya Viongozi na wafuasi wa CHADEMA na hali ya utulivu ilirejea kwenye eneo husika.

MAPENDEKEZO

-Mauaji ya mwandishi wa habari Daud Mwangosi yalitokea baada ya operesheni kumalizika, na amri ya kuondoka kwa askari eneo la tukio kutolewa na Viongozi wa operesheni hiyo

-Jamii wakiwemo Viongozi waelimishwe umuhimu wa utii wa sheria, kanuni na taratibu ili kudumisha amani na utulivu hapa nchini. Viongozi wengi walionyesha hofu ya kuliingiza Taifa kwenye machafuko makubwa na uvunjifu wa amani iwapo jamii haitazingatia umuhimu wa kutii sheria, kanuni, taratibu na amri halali za Mamlaka.

-Msajili wa Vyama vya siasa afafanue majukumu ya vikundi vya Ulinzi vya Vyama vya Siasa kama vile Green Guard, Red Brigade, Blue Guard.

-Iwepo programu mahususi ya Elimu ya Uraia nchini ili kujenga uzalendo na kukuza maadili ndani ya jamii wakiwemo viongozi wa kada mbalimbali. Hivi sasa jamii inashuhudia kutoweka kwa uzalendo na kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii.

Njia zifuatazo zitumike:

- Elimu ya uraia iimarishwe katika mitaala ya elimu kuanzia Shule za msingi hadi Vyuo Vikuu.

- Uamuzi wa kurudisha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana utekelezwe mapema.

- Vyama vya Siasa, Madhehebu ya Dini, Tasnia ya Habari na Taasisi zisizokuwa za Serikali zishiriki kikamilifu katika uenezi wa Elimu ya Uraia nchini.

- Kuhimiza uzingatiaji wa weledi katika utendaji kazi kwa mujibu wa taaluma na miongozo inayotolewa kuleta ufanisi. Aidha elimu endelevu sehemu za kazi itiliwe mkazo.

-Kufanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya 1992 ili kuweka wazi shughuli za Vyama vya Siasa baada ya Uchaguzi Mkuu. Lengo ni kuwa Shughuli za Siasa zihamie Bungeni kujadili na kuhoji mipango ya Serikali na matumizi ya rasilimali za nchi. Kwa kufanya hivyo wananchi watapata nafasi kufanya kazi za maendeleo.

-Kuboresha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, hususan uanzishwaji wa ofisi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuratibu ushirikiano/mahusiano baina ya serikali (Jeshi la Polisi) na Vyama vya Siasa. Lengo ni kukuza mahusiano na kuondoa mgongano.

-Utaratibu wa kufanya mikutano mara kwa mara kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari uimarishwe ili kujenga mahusiano mazuri na kupata ufumbuzi wa haraka kwa matatizo yaliyojitokeza.

- Jeshi la Polisi nchini ni chombo muhimu katika ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Muundo uliopo wa Jeshi la Polisi uangaliwe upya Kisheria ili kuziba mianya inayotoa nafasi kwa wanasiasa kulitumia Jeshi hilo kwa manufaa ya Kisiasa. Aidha mipango ya kuboresha utendaji kazi kitaaluma iliyopo hivi sasa upewe msukumo stahiki hususan rasilimali watu na fedha.

- Wananchi wahamasishwe kushirikiana na Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi. Polis ishirikiane na Serikali za mitaa kufanikisha malengo hayo.

- Jeshi la Polisi liimarishwe ili litekeleze majukumu yake kikamilifu na kujenga mahusiano sahihi kati yake na Jamii, Vyama vya Siasa, Tasnia ya Habari na Asasi zisizo za Kiserikali.

-Taasisi za habari zinazosimamia maadili na weledi wa vyombo vya habari, hususan Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri wafanye utaratibu unaostahiki wa upatanishi kati ya waandishi wa habari, Jeshi la Polisi na uongozi wa mkoa wa Iringa. Hii itasaidia kurejesha uhusiano mzuri kati ya vyombo hivyo muhimu katika mkoa.

-Waandishi wa habari wapewe mafunzo ya jinsi ya kuripoti matukio ya hatari/ghasia.

-Waandishi wa habari wavae vivazi maalum vya kuwatambulisha wakiwa katika matukio hasa kwenye maeneo hatarishi.

-Waandishi wa habari wafanye kazi kwa weledi, uadilifu, uwazi na wasijibainishe na vyama vya siasa.

-Kamati ya Ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari iliyoanzishwa mwaka 2008 ifufuliwe. Na kamati hizo ziteremke hadi kwenye ngazi ya mkoa kama ilivyokuwa awali.

-Viongozi wa Polisi wanapotoa taarifa za tukio, ziwe zimefanyiwa utafiti wa kina ili zisipotoshe jamii.

-Kuwe na jukwaa la mazungumzo ya mara kwa mara kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa ili kila upande ujue wajibu wake na wa taasisi nyingine katika kudumisha amani ya nchi na utamaduni wa kuheshimu sheria zilizopo na kupunguza migongano.

9.0. CHANGAMOTO

Changamoto zilizojitokeza katika Uchunguzi zimegawanyika katika mtiririko ufuatao:-

9.1 Jeshi la Polisi:

- Ukosefu wa Mafunzo endelevu.

- Ukosefu wa Uvumilivu katika utekelezaji wa Majukumu.

-Uelewa mdogo wa Elimu ya Uraia.

- Mmomonyoko wa Maadili.

- Kukosekana kwa uzalendo.

- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na Taratibu

9.2 Vyama vya Siasa:

- Kukosekana kwa uvumilivu katika kuendesha shughuli za Siasa.

-Kukosekana kwa Elimu ya Uraia

- Uelewa mdogo wa baadhi ya Viongozi wa Vyama kuhusu uendeshaji wa Vyama vya Siasa.

- Ukosefu wa Sera/Mwongozo kwa Vyama vya Siasa kuendesha shughuli za Kisiasa baada ya uchaguzi mkuu.

- Kukosekana kwa Jukwaa linalokutanisha mara kwa mara Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi

- Mmomonyoko wa Maadili.

- Suala la Uzalendo.

- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na Taratibu

9.3 Jamii:

- Elimu ya Uraia.

- Mmomonyoko wa Maadili.

- Kukosekana kwa uzalendo.

- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

26

10 HITIMISHO

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusema kuwa, “ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne ambavyo ni watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watanzania kila mtu mahali pake, tunahitaji kuwa na siasa safi yenye kujenga ustawi, tija, mshikamano, amani, maendeleo na afya kwa taifa letu”.

Utulivu na amani kwa ajili ya mustakabali wa taifa, imekuwa ni kauli mbiu ya viongozi mbalimbali ambao Kamati hii imepata fursa ya kuzungumzia juu ya hali ya siasa na mahusiano yaliyopo baina ya Serikali, (Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama wilaya na mkoa), vyama vya siasa, viongozi wa dini na wananchi.

Wananchi na Viongozi wanataka kuona shughuli za siasa ya vyama vingi inaendeshwa kwa hoja zenye tija badala ya vurugu na utengano. Njia mojawapo ya kukabiliana na hali hii inayojitokeza ni kujenga uzalendo, maadili mema, na mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Kamati hii inashauri na kupendekeza kuwa maoni haya yazingatiwe na kutekelezwa.

Aidha Kamati imefaidika sana kupata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali kuanzia kijiji hadi taifa na walitoa ushirikiano wa dhati katika kutoa mchango wao wa mawazo. Kamati inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi (Mb) kwa imani yake kwa wajumbe wa Kamati ya Uchuguzi.