Pages

Tuesday, July 31, 2012

BAVICHA yaunga mkono maandamano kupinga kufungiwa kwa MwanaHALISI


Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tukiwa ni sehemu ya wadau wa sekta ya habari nchini, tunaunga mkono maandamano ya amani mliyoitisha ya kupinga hatua ya serikali kulifungia gazeti la MwahaHALISI.

Tunawapongeza wahariri kwa mshikamano wenu katika kipindi hiki cha majaribu; endeleeni kusimama pamoja, ni umoja wenu ndio utakaokuwa kinga ya pamoja dhidi mtu au chombo chombo chochote kinachoingilia uhuru wenu. Mshikamano wenu ni ishara ya kushindwa kwa mkakati wa ‘wagawe uwatawale’ na imani kwamba umoja ni nguvu. Wahariri wote hawapaswi kukaa kimya kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI kwa kuwa leo ni kwa gazeti hilo, kesho itakuwa kwa gazeti lingine; hivyo ni vyema kuungana pamoja kulinda uhuru, taaluma na sekta ya habari nchini.

Kwetu sisi hatua hiyo ya serikali tunaitafsiri zaidi ya kufungia gazeti la MwanaHALISI; ni hatua ya kufungia uhuru wa kusambaza habari na uhuru wa kupokea habari. Hivyo hatua hiyo ni kinyume cha haki za binadamu, kinyume cha utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo. Hakika serikali na viongozi wake wamevuka mstari wa kukubali kukosolewa na sasa wameamua kuanza kufungia uhuru wa fikra mbadala.

Hatua ya Waziri mwenye dhamana na sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji ni mwelekeo mbovu wa kupuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki. Uamuzi uliofanywa na serikali hauna tofauti na unaofanywa na raia wanaojichukulia sheria mikononi(mob justice). Kwa serikali inayoheshimu misingi ya asili ya haki, tulitarajia chombo chochote cha habari, kikivunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka ama malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari(MCT) ama Mahakama.

Hatua ya serikali kufungia gazeti la MwanaHALISI pamoja na kuwa imechukuliwa kwa mujibu wa sheria iliyopo, imekiuka misingi ya asili ya utawala wa sheria. Kwani kulikuwa na sheria nyingine nzuri ambazo serikali ingeweza kutumia kupitia mahakama lakini ikaamua kuchagua kutumia sheria mbaya kwa kutumia mamlaka ya Waziri. Itakumbukwa kwamba wadau wa sekta ya habari na hata serikali yenyewe imekuwa ikikiri kwamba Sheria hiyo iliyotumiwa ni sheria mbovu inayohitaji kufutwa ama kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwemo kupunguza mamlaka makubwa ya viongozi wa serikali dhidi ya vyombo vya habari. Sheria yoyote inayotambulika kuwa mbovu katika jamii yoyote, inapoteza uhalali wa kihaki(legitimacy) miongoni mwa umma na hivyo kuendelea kuitumia ni kuteteresha misingi ya utawala wa sheria na kutoa mfano mbaya kwa vijana nchini na wananchi kwa ujumla. Hivyo, tunachukua fursa hii kuitaka serikali kuharakisha mchakato wa kupitisha sheria ya vyombo habari na sheria ya uhuru wa taarifa.

Aidha tumeshangazwa na uamuzi wa serikali kufanya maamuzi yake kwa ubaguzi kwa kulichukulia hatua gazeti la MwanaHALISI na kukwepa kuyachukulia hatua magazeti mengine ambayo yameandika habari inayoshabihiana na maudhui ya habari iliyoandikwa na gazeti hilo. Kwa muda mrefu sasa, habari za uwepo wa viongozi ama makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) yenye kupanga ‘kumng’oa’ Rais Jakaya Kikwete miongoni mwa wanaotarajiwa kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2010 zimeandikwa na magazeti mbalimbali. Hatua hii ya kibaguzi inaibua maswali kuhusu dhamira ya serikali kulifungia gazeti hilo wakati huu ambapo mchango wa gazeti hilo na mengine yaliyo mstari wa mbele kupinga ufisadi na kutetea rasilimali za taifa unahitajika kwa kiasi kikubwa. Hata baada ya kulifungia gazeti la MwanaHALISI, habari za aina hiyo zimeendelea kuandikwa ikiwemo na vyombo vya habari vya nje; mathalani tarehe 24 Oktoba, 2008 kutoka Ufaransa gazeti la Africa Intelligence inayomtaja Rostam Aziz kukusanya fedha kwa ajili ya kufadhili kundi lake katika uchaguzi huo. Katika muktadha huo, serikali inapaswa kulifungia gazeti la MwanaHALISI mara moja, kama imeonyesha wazi kushindwa kuyachukulia hatua magazeti mengine.

Kadhalika kwa mtiririko wa matukio katika taifa letu, kuna mwelekeo wa Serikali na CCM kuminya maoni yenye kumkosoa au kumgusa Rais Kikwete. Mjadala wa Rais Kikwete ‘kung’olewa’ katika uchaguzi mwaka 2010 unaelekea kuichukiza kwa kiasi kikubwa Serikali na CCM. Gazeti la MwanaHALISI liliandika habari ya namna hiyo, likafungiwa na Serikali. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika ‘Operesheni Sangara’, alitoa hoja hiyo na matokeo yake CCM ikaibuka na kujibu kwa vitisho na vioja.

Vijana wa Tanzania wangependa kupata mfano uongozi bora wenye kukubali kukosolewa na kukubali mabadiliko badala ya uongozi legelege wenye kuendeleza udikitekta wa kimawazo na hivyo kuminya fikra huru. Si dhambi kwa CHADEMA ama mtu yoyote kutaka kuiondoa CCM ama kiongozi wake yoyote madarakani mwaka 2010 kupitia njia za kidemokrasia.

Mwisho, tunatoa mwito kwa watanzania wote kusoma alama za nyakati na kuunga mkono harakati hizi za wahariri na wadau wa sekta ya habari kutetea uhuru wa kweli katika taifa letu. Jamii itambue kwamba kitisho cha uhuru na haki kwa mtu Fulani au mahali Fulani ni tishio kwa watu wote na mahali pote. Yanayofanywa kwa vyombo vya habari, yanaweza pia kufanywa kwa watetezi wengine kwani hivi karibuni taifa limeshuhudia Asasi ya HAKIELIMU ikitishiwa kutokana na jitihada zake za kuhamasisha mabadiliko ya fikra katika sekta ya elimu na kupiga vita ufisadi unaoathiri sekta hiyo. Tuko katika kipindi cha majaribu; kuibuka kwa mijadala yenye kuchochea mgawanyiko/ubaguzi, kuongezeka kwa matabaka na malalamiko juu ya hali za maisha. Katika wakati huu ambapo misingi ya nchi yetu iliyopo katika Ngao ya Taifa ya Uhuru na Umoja inapotikiswa ni wakati wa kuunganisha “Nguvu ya Umma” kupinga aina zote za ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa kuhamasisha maadili, fikra mbadala na mabadiliko ya kweli. Kuunga mkono maandamano ya wadau wa sekta ya habari ni sehemu ya azma hiyo. Mshikamano, daima; pamoja, tutashinda!

Wasalaam,

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa.

Maoni yangu kuhusu mgomo wa walimu

                                    
" Elimu ndio ufunguo wa maisha" hii ni kauli maarufu na kila mmoja wetu anafahamu umuhimu wa elimu katika maisha. Elimu kwa maana isiyo rasmi ni mchakato wa kuelimisha ama kuelimishwa jambo usilolijua ili uweze kupata ufahamu chanya ama hasi wa jambo hilo.

Ni miaka mingi imepita tangu nianze kusikia matatizo ya walimu na serikali, kikubwa walimu wakilalamikia maslahi duni wanayopata huku serikali ikjigamba kutatua matatizo haya pale inapoulizwa.

Kama nilivyotambulisha awali maana ya elimu kuwa ni kupata ufunuo kwa jambo usilofahamu, hapa wanafunzi wanaelimishwa mambo mbalimbali na walimu katika utaratibu maalum ambao nchi imejipangia ili kuweza kukamilisha malengo mbalimbali.

Kwa kuwa elimu ni muhimu katika jamii yetu, ubora wa elimu nao ni jambo la msingi katika muktadha wa Nchi yeyote ile. Walimu wanapaswa wapate maslahi bora kuanzia mishahara yao na posho zao ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi wao.

Walimu wanapaswa kuwa na nyenzo bora zitakazowawezesha kutoa elimu bora. Mfano wa nyenzo hizi ni kuwa na vifaa vya kisasa vya kufundishia (ICT), maabara bora, maktaba na wanaoelimishwa kuwa na madawati na vitendea kazi. Haya ni baadhi ya mambo muhimu yanayomzunguka mwalimu na mwanafunzi.

Endapo mwalimu atakosa mambo haya ya msingi, basi mwalimu huyu kuna uwezekano mkubwa wa kutotoa elimu bora hivyo taifa kukosa wataalamu watakaoliletea tija taifa letu.

Serikali kwa upande wake inakubali kwamba walimu wanahitaji maslahi bora, wanafunzi pia wanahitaji mazingira bora kiujumla ili waweze kuelimika vizuri, ila tatizo ni uwezo mdogo wa kibajeti. Nijuavyo mimi serikali iliyowekwa madarakani na wananchi inapaswa kutatua kero za wananchi, na si kutoa sababu kwa wananchi ya kutotekeleza ama kutatua kero.

Serikali ni lazima ihitimishe suala hili kwa kutatua kero za walimu kwa kuangalia chanzo na si matokeo, la sivyo kila mwaka kutakuwa na migongano baina yake na jamii katika kada tofauti. Mgomo wa madaktari una kishindo kikubwa kwa kuwa muathirika huenda akafa, lakini kishindo cha mgomo wa walimu ni kibaya zaidi kwa kuwa muathirika hapati elimu bora, hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Mathalani masomo mengi hufundishwa kwa kuwaandaa wanafunzi kinadharia na si vitendo, hii hupelekea wanafunzi kushindwa katika soko la ajira na pia kupungua kwa ubunifu hapa nchini kwetu.

Nahitimisha kwa kupendekeza walimu watekelezewe maslahi yao kwa asilimia mia moja, ili watoto wa wakulima waje wapate fursa katika nchi hii, pia mfumo wa elimu ubadilike uwe wakivitendo zaidi ili tupate wabunifu watakaolivusha taifa hili katika janga la umaskini na kuepuka mambo mengi ya kuiga kutoka kwa wanzetu.

Mkali

Monday, July 30, 2012

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya colorado asomewa mashtaka 24 ya mauaji


CENTENNIAL, Colo. (AP) --
Mwendesha mashtaka wa colorado amemsomea mashtaka ya mauaji 24 na mengine ya kujaribu kuua 116, mhitimu wa wa fani ya neuroscince, leo siku ya jumatatu katika mashambulizi ya kustukiza yaliofanyika katika maonesho ya filamu mpya iitwayo Batman  huko colorado.

James Holmes ambaye alionekana kama amechanganyikiwa kwa mara ya kwanza alipojitokeza mahakamani wiki iliyopita,aliweza kubadilishana mawazo na mmoja wa mawakili wake mahakamani hapo. Mwenendo wa kesi hiyo mpaka sasa bado haujulikani vizuri.

Mashambulizi hayo ya usiku yaliacha watu  12 wakipoteza maisha na 58 wakijeruhiwa vibaya. Baada ya kukamatwa kwake polisi walisema makazi ya kijana huyo si ya kawaida, na moja ya mashtaka alosomewa leo hii ni kukutwa na vitu vya mlipuko. Wachunguzi wa mambo ya kisheria wamesema kesi hiyo itagubikwa na ushindani wa hoja ya kuhusiana na akili ya kijana huyo kama ni punguani ama la.

Source: Reuters
Translation: Mkali

Saturday, July 28, 2012

Mahojiano yangu na Zitto kweye Twitter


Kufuatia sakata la baadhi ya wabunge kushutumiwa kwamba wamekula mlungula ili wafanikishe kumuwajibisha waziri wa Nishati na madini na Katibu mkuu wa wizara hiyo, kwa kukiuka sheria za manunuzi ya umma, Nilimtweet Mheshimiwa Zitto Kabwe kuhusiana na kadhia hiyo., Ilikuwa hivi

Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
Spika ni vema aikubali hoja ya ndg. Vita Kawawa kwamba suala la tuhuma kwa baadhi ya wabunge kuhongwa na lijadiliwe mahususi >>

Mkally Mlanzi@MkallyMlanzi
nakufuatilia sana mheshimiwa,, but kama vile utoe kauli maana these statement they meant u....tunapata shida ss wafuas wako

Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
usiwe mfuasi wangu. Fuata 'principles' ninazoamini. 'Justice' ndio msingi hapa. Sitatolea kauli tuhuma za kubumbabumba.

Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
>> kwenye mjadala mahususi ushahidi utatolewa na watuhumiwa kujieleza. Vinginevyo hizi ni siasa tu zenye malengo Maalumu dhidi ya mtu fulani

Mheshimiwa Zitto aliendelea kutweet kwa kumquote Nguli wa mashahiri wa kiswahili Shabani Robert akionesha kushikilia msimamo wa  yale anayoaamini.

Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
Shabaan Robert alisema, "msema kweli huchukiwa na rafiki zake, sitaona wivu juu ya wale wapendwao na marafiki zao siku zote,">>
Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
>> 'siwezi kuikana kweli kwa kuchelewa upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga.

Jumamosi njema wadau.
Mkali- 0688323837

Friday, July 27, 2012

Maisha magumu, ni utegemezi wa mafuta kwenye umeme-Mnyika

Udhaifu wa kutokutekeleza mipango ya uzalishaji wa gesi na makaa ya mawe kwa wakati umesababisha utegemezi mkubwa kwenye matumizi ya mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura. Takribani nusu ya umeme unaozalishwa nchini hivi sasa unazalishwa kwa kutumia dizeli, mafuta ya ndege na mafuta mazito hali ambayo imeongeza mahitaji makubwa ya uagizaji wa mafuta toka nje ya nchi.


Hii imesababisha mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza mafuta na hivyo kuchangia katika kuporomoka kwa thamani ya shilingi. Aidha, ongezeko kubwa la uagizaji toka nje limeathiri urari wa biashara na hivyo kuchangia katika mfumuko wa bei. Hivyo, Watanzania hivi sasa wanabeba mzigo wa kupanda kwa bei za bidhaa na gharama za maisha kwa ujumla kutokana na ufisadi kwenye mikataba, ubadhirifu katika matumizi, uzembe katika uongozi na upungufu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali kwenye sekta ya nishati.

Mzigo huu usingekuwa mkubwa iwapo Serikali ingetekeleza katika mwaka wa fedha 2011/2012 maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya kuhakikisha nyongeza ya fedha kwenye bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa upande wa sekta ndogo ya Gesi kwa ajili ya mitambo ya umeme na kuharakisha kuwekeza katika Bomba la Gesi pamoja na ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Gesi (LPG extraction Plant).

www.mnyika.blogspot.com

Misamaha ya kodi kwenye gesi NO- Mh Zungu


Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa kamati ya bunge Mh Zungu, ameionya serikali kuhusu kuweka msamaha wa kodi kwenye gesi inyopatikana katika mikoa ya kusini.

Akichangia kwa hisia hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati na madini, Mheshimiwa Zungu amesema gesi ni rasilimali ambayo itaipatia Nchi ya tanzania mapato ya kutosha ili kuondokana na tatizo la umaskini.

Mheshimiwa Zungu ameitaka serikali kutoa misamaha ya kodi katika sekta nyingine na wala si gesi, na kuionya kwamba endapo isipofanya hivyo bungeni hapatakalika.

Mkali
0688323837

Thursday, July 26, 2012

Serikali yatangaza neema kijiji inakochimbwa gesi


SERIKALI imetangaza neema kwa wakazi wa Kitongoji cha Mchepa katika Kijiji cha Madimba, wilayani Mtwara ambalo litakuwa kitovu cha mradi wa uchimbaji wa gesi asilia, itakayokuwa suluhisho la matatizo ya umeme nchini. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliwaambia wananchi hao wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo kuwa, wakazi wa Mchepa na Madimba, wataunganishiwa umeme bure.


“Tumeamua kwamba kila atakayehitaji umeme ataunganishiwa umeme huo bure, kwa hiyo kazi yenu ninyi, ni kuweka waya na vifaa vingine katika nyumba zetu halafu kazi ya kufikisha umeme kwenye nyumba zenu itakuwa ya Serikali, kwa hiyo jamani kazi kwenu,”alisema Profesa Muhongo. Alisema Serikali pia imefanya mazungumzo na kampuni tatu za ujenzi wa bomba hilo, ili zianze kununua mazao ya wananchi wa eneo hilo zikiwemo mbogamboga na matunda, badala ya kuagiza mazao hayo kutoka Kenya na Afrika Kusini.


Profesa Muhongo alisema mipango iliyopo ni kuwezesha ujenzi wa viwanda vya usindikaji wa matunda na mbogamboga katika eneo la machimbo hayo ya gesi, ili kuwezesha bidhaa za wananchi wa eneo hilo kupata soko kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasa.


“Pia tumeamua kwamba katika Chuo cha Veta cha Mtwara tutawasomesha vijana 50 bure kutoka Mtwara na katika ngazi ya taifa, tumeanza programu za kuwandaa wataalamu wa sekta ya gesi kwa kuanzisha mafunzo katika vyuo vyetu vya ndani na kuwapeleka wengine nje ya nchi,”alisema waziri huyo. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi alisema kupitia mradi wa ujenzi wa bomba hilo, Kitongoji cha Mchepa na Kijiji cha Madimba vitaboroshewa huduma za kijamii.


“Hapa tunasema kwamba lazima maisha yabadilike maana ndipo lilipo chimbuko la gesi, kwa hiyo huduma za elimu, afya na shughuli za michezo kwa kujenga viwanja vya michezo hiyo vitaboroshwa,”alisema. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika alisema lazima wananchi wa Mtwara wawe tayari kuupokea mradi huo kwa manufaa yao na nchi kwa jumla.

“Kuna baadhi ya watu hapa wanapita wanasema maneno ya uongo kwamba eti mradi huu utawanufaisha watu wengine kwa sababu gesi inapelekwa Dar es Salaam, sawa lakini huu ni mradi wa kitaifa, gesi ipo ya kutosha na hata ile inayozalishwa sasa watu wa Mtwara hawawezi kuitumia yote,”alisema Mkuchika.


Alisema kuanza kwa ujenzi wa mradi huo kuna maana kubwa ya kuwa sasa ni wakati wa wananchi wa mikoa ya Kusini, kupiga hatua za kimaendeleo”

Wednesday, July 25, 2012

Makampuni ya simu yaingiza bilioni 43 kwa mwaka kupitia ringtone-Zitto


Mbunge wa Kigoma kaskazini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe, amesema makampuni ya simu yanajipatia kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni 43 kupitia Ringtone.

Mh Zitto ameyasema hayo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Mawasiliano iliyowasilishwa mapema asubuhi bungeni mjini Dodoma Leo.


Mh Zitto alisema kuwa makampuni ya simu yanapata 80% ya mapato yote yanayolipwa na mteja kwa huduma ya ringtone, 13% kwa makampuni ya kati na 7% ikienda kwa msanii ambaye kimsingi ndiye huangaika na utunzi wa nyimbo.

Mheshimiwa Zitto ameitaja kuwa kampuni ya OWN MOBILE ndiyo inayoendesha biashara hiyo ya ringtone, huku ikiingia mikataba na kampuni ya AIRTEL na VODACOM na kuwa kampuni hiyo mpaka sasa haijasajiliwa.

Mhe amezidi kuishauri serikali kuwa ni lazima wasanii wenyewe wapate si chini ya asilimia 50 ili waweze kufaidika na jasho lao na kulitaka shirika la posta lijiandae kuanza kusambaza kazi za wasanii, ili kupunguza mianya ya rushwa katika kazi za wasanii.

Mkali
0688323837

Tuesday, July 24, 2012

Ghana President Mills dead: presidential statement


(Reuters) - Ghana's President John Atta Mills has died unexpectedly, a presidential statement said, and an aide said his death occurred on Tuesday after he took ill on Monday night.
The death of the president of the world's No. 2 cocoa grower comes months before Mills was due to stand for re-election at the helm of the West African country that posted double-digit growth in 2011 and has been praised for its strong democracy in a turbulent region.
"It is with a heavy heart...that we announce the sudden and untimely death of the president of the Republic of Ghana," a statement sent to Reuters by the president's office said.
It said that Mills, 68, died a few hours after being taken ill but no further details were given.
A presidential aide, who asked not to be named, said the president had complained of pains on Monday evening and died early on Tuesday afternoon when his condition worsened.
Mills, who oversaw the start of oil production in Ghana, returned from medical checks in the United States several weeks ago.

(Reporting by Kwassi Kpodo; Writing by David Lewis; Editing by Michael Roddy)

Monday, July 23, 2012

Mambo yanayosababisha ajali za meli


KUZAMA kwa meli ya Skagit Jumatano iliyopita ni ajali ya tatu ya aina hiyo kutokea hapa nchini na kusababisha vifo vya watu wengi.Mwaka 1996, ilitokea ajali ya MV Bukoba iliyozama Ziwa Victoria, ambayo kwa mujibu wa takwimu za Msajili wa Vizazi na Vifo Wilaya ya Mwanza, ilisababisha vifo vya watu 1,020.
Mwaka jana ikiwa miezi kumi imepita hadi sasa, pia ilitokea ajali nyingine ambapo meli ya MV Spice ilizama katika ukanda wa Bahari eneo la Kisiwa cha Nungwi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200.
Matukio mawili ya Mv Spice na Skagit yaliyotokea nchini kweye Bahari ya Hindi, katika kipindi cha miaka miwili mfululizo yameshtua wengi.
Ajali zote tatu zilizotokea kwa vyombo hivyo majini zilitokana na sababu mbalimbali.
Bila shaka Watanzania wengi watapenda kufahamu nini kilisababisha ajali hizo na pengine kitafutiwe ufumbuzi wa haraka.

Ili kuweza kufahamu hayo ni vyema kujua namna meli inavyofanya kazi na kuifanya ielee kwenye maji.

Meli inavyoelea
Utengenezaji wa meli hufuata kanuni ya Mwanasayansi, Newton ambaye katika utafiti wake aligundua kuwa ili kitu chochote kiweze kuelea kwenye maji kunakuwa na nguvu inayokisukuma juu.
Katika hali hiyo kinachofanya kisizame ni kusukuma nje kiwango cha maji kinacholingana na uzito wake.

Watengenezaji wa meli hutumia kanuni hiyo katika kutengeneza meli za aina mbalimbali na kuweka bayana kiwango cha uzito kinachofaa kubebwa na chombo hicho.

Uzito unapoongezeka huwa ni hatari, kwa sababu meli hiyo itakuwa inazama kwenye maji.

Maelezo ya kiufundi yaliyopatikana katika mtandao wa Wakala wa Meli wa Kimataifa yanaeleza kwamba, meli imetengenezwa kwa namna ambayo uzito wake unasukuma nje maji yanayolingana na uzito wake wakati ambapo sehemu yake bado imebakia juu ya uso wa maji.

Licha ya kutumia kanuni hiyo, inaelezwa kuwa watengenezaji wa meli huzingatia vigezo vingine kama vile joto, ambalo linaweza kubadilisha uzito wa maji kulingana na kipimo cha ujazo.

Kwa sababu hiyo, inaelezwa: "Msukumo wa kwenda juu wa kwenye maji ndiyo unaosababisha meli kuelea na injini zake ndizo zinazoiwezesha kutembea.”

Kasi ya kutembea kwa meli hutegemeana na uwezo wa injini pamoja na namna nahodha wake anavyoamua, kulingana na mazingira yanavyomruhusu.

Hata ikiwa injini za meli zitakuwa hazifanyi kazi, meli huelea kwenye maji kwa sababu utengenezaji wake unaifanya isizame.

Aina za meli
Kwa kawaida zipo aina zaidi ya 16,000 za meli. Lakini zinaweza kuwekwa katika makundi makuu sita.

Makundi hayo ni ya meli zinazobeba makontena, malighafi maalumu, mizigo, mafuta, kemikali, meli maalumu za kuvunja barafu, za kusafirishia abiria na zile za kivita.

Hata hivyo, wataalamu hao wanasema kuwa kwa kawada meli zimetengenezwa kwa ajili ya kubeba mizigo, lakini zipo maalumu ambazo hutumika kwa ajili ya kuvusha abiria katika safari fupi.

Ajali za meli
Zipo aina nyingi za ajali za meli, lakini nyingi zimekuwa ni za meli za kubeba mizigo, ambazo mara nyingi ndizo zinazosafiri umbali mrefu.

Mara nyingi mambo yanayoweza kusababisha ajali za meli ni kubeba vitu vinavyozidi uwezo wake, upangaji mbaya wa mizigo, machafuko ya bahari, vyombo kugongana pamoja na kugonga miamba baharini.
Nyingine ni moto wa ghafla unaoweza kusababishwa na hitilafu ya umeme au mizigo iliyobebwa na chombo husika.

Tatizo jingine linaelezwa kuwa ni kuchakaa kwa chombo na matatizo mengine ya kibinadamu kama vile uzembe katika matengenezo na ukarabati.

Uimara wa aina ya chuma kinachotumika kutengeneza meli ni mojawapo ya mambo ambayo wataalamu hao wanaeleza kuwa yanazingatiwa katika kuipa uwezo wa kudumu kwa miaka mingi ikifanya kazi bila kuharibika.

Kwa kawaida vyuma hupata kutu na kusababisha matundu yanayoweza kusababisha meli ipate ajali, hivyo ukarabati na uchunguzi wa mara kwa mara hufanyika.

Ufanyaji kazi wa meli, unaelezewa kitaalamu kwamba huwa na mwisho, ambapo haifai tena kwa ukarabati wa aina yoyote kuirudisha katika hali yake ya kawaida.
Katika hali hiyo ikifanyiwa ukarabati na kulazimishwa kufanya kazi, hapo inaweza kusababisha ajali ya ghafla.

Moja ya mambo yanayosababisha vyuma vya meli kupata kutu haraka hasa inavyokuwa imezama baharini ni uwepo wa chumvi kwenye maji bahari au maziwa.

Hata hivyo, mambo mengine yanayoweza kusababisha ajali ya meli nje ya uwezo wa kawaida wa kibinadamu inaelezwa kuwa ni hali ya hewa kama vile upepo mkali na vimbunga.

Wataalamu hao wanasisistiza kuwa kwa namna meli ilivyoundwa ajali zake nyingi hutokana na matatizo yanayosababishwa zaidi na makosa ya kibinadamu.

Hii ni kwa sababu wataalamu wameweka masharti mbalimbali ya kutumia chombo hicho kama ikiwamo muda wa kutumika, muda wa matengenezo na namna sahihi ya matumizi.

Vilevile inaelezwa kuwa iwapo waongozaji wa chombo hicho watafanya kazi muda mrefu bila kupumzika, wanaweza kupoteza umakini katika kukiongoza.

“Suala la usimamizi ni la msingi na muhimu katika kuepusha chombo cha majini kisipate madhara. Kwa kawaida nahodha huchunguza mazingira ambayo chombo kinapita na kuhakikisha kinasonga mbele kwa usalama," inaeleza ripoti hiyo ya wataalamu wa meli.

Ili kuepusha ajali za vyombo vya majini, inaelezwa kuwa utendaji wake wa kazi umewekewa masharti kadhaa, ambayo husimamiwa kitaifa na kimataifa kwa usalama wa watu na mali zao.

Mmoja wa makapteni wa meli nchini Marekani Cmdr Paolillo, ambaye meli aliyokuwa akiiendesha ilipata ajali, alisema ajali hiyo ilitokana na sehemu ya chombo chake iliyozama ndani ya maji kugota kwenye mwamba ndani ya bahari.

Anasema kosa hilo lilitokana na uzembe wa kutofuata njia salama, hasa ikizingatia meli aliyokuwa anaiendesha ilikuwa ni ya kizamani.

Anasema meli za kisasa zina uwezo wa kuchunguza njia na kufahamu kama kuna hatari ya meli kugota popote.

Habari hii imeandikwa na Leon Bahati kwa msaada wa taarifa mbalimbali ( www.mwananchi.co.tz)

Waziri wa mawasiliano na miundombinu ajiuzulu Zanzibar


Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu mjini Zanzibar, Hamad Masoud amejiuzulu wadhifa wake baada ya kuwepo kwa shinikizo la kuachia ngazi lilitoka kwa wananchi.

Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua.

www.mwananchi.co.tz

Sunday, July 22, 2012

Zanzibar says 145 people were killed in ferry disaster last week


DAR ES SALAAM, July 22 (Reuters) - Authorities in Zanzibar said on Sunday that 145 people had been killed in last week's ferry disaster in the Indian Ocean, a day after the operation to find survivors was called off.

The overcrowded MV Skagit/Kalama, which had also been carrying some foreigners, was en route to Zanzibar, a popular tourist destination, from mainland Tanzania last Wednesday when it capsized and sank.

"We have recovered five more bodies today, bringing the total number of bodies found so far to 73. The ferry had 290 people onboard and 145 were rescued, which means that 72 people are still unaccounted for," Mohammed Mhina, a spokesman for Zanzibar police, told Reuters.

"It has now been four days since the ferry capsized - it's impossible to find any more survivors. Those who are still missing are presumed dead, so the ongoing operation is for the recovery of bodies rather than a search for survivors."

Police said they had arrested six suspects on Sunday as part of an investigation into the ferry disaster.

"The owner of the boat, Saidi Abdulrahman, and the captain of the vessel who survived the accident, Mussa Makame Mussa, and four other crew members have been arrested," said Mhina.

"Investigations into the cause of the accident are still proceeding and the suspects will be taken to court if found with a criminal case to answer."

On Friday, riot police clashed with supporters of a separatist Islamist group in Zanzibar who had gathered at a mosque to pray for victims of the disaster.

Police said they had arrested 43 members of the Uamsho (Awakening) group following the violence.

Some of the victims' relatives have vented anger at the authorities for what they say were lax safety regulations which did not appear to have been improved since last September when more than 200 people were killed in another ferry accident in what was Zanzibar's worst maritime disaster.

(Reporting by Fumbuka Ng'wanakilala; Editing by Yara Bayoumy and Andrew Osborn)-Reuters Africa.

Kuzama kwa MV Skagit ni matokeo ya kutotibu kiini cha ajali zilizopita

                            
Na: Maggid Mjengwa,
WATANZANIA tumekumbwa tena na balaa la ajali kubwa ya meli kuzama. Ni wakati sasa wa kujifunza kutokana na yaliyotokea huko nyuma.
Maana ajali ya Mv Skagit inaonekana dhahiri kuchangiwa na uzembe. Na uzembe kwa nchi yetu unalelewa na mfumo mbovu. Na mfumo mbovu unatokana na Katiba mbovu.
Maana, ni katika mazingira haya ya kufanya mambo ya hovyohovyo ndipo tunapokuwa na wanasiasa wa hovyohovyo wenye kuhusika pia na biashara ya uchukuzi na usafirishaji wa abiria. 
Ni vigumu kwa mfumo wetu wa sasa, kwa watendaji wa vyombo au taasisi zisizo huru kikatiba na kisheria kuweza kuwasimamia wafanyabiashara dhalimu ambao miongoni mwao wamo baadhi ya wanasiasa wetu.
Tuna lazima sasa kupitia Katiba yetu ijayo, kuvipa nguvu za kisheria vyombo na taasisi zetu muhimu kwa nchi yetu. Tuwe na vyombo na taasisi huru ambazo utendaji wake hauwezi kuingiliwa kirahisi na mamlaka nyingine.
Fikiri leo kama tungekuwa na utaratibu wa kwamba mmiliki wa chombo cha majini au angani na atakayebainika kuingiza nchini chombo kilicho chini ya viwango vinavyokubalika kimataifa na hata chombo hicho kikasababisha ajali ya kuua raia kuwa mmiliki huyo atafungwa jela na kufilisiwa mali zake? Naamini, tungekuwa na vyombo madhubuti na ajali zingetokea kwa bahati mbaya kwa maana yake halisi.
Ni nini basi cha kujifunza kutoka kwenye ajali iliyopita ya Mv Spice Islanders?
Ikumbukwe, Ripoti ya Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islanders ilipendekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari, Mustafa Aboud Jumbe pamoja na wahusika wengine wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kutokana na uzembe waliofanya na kusababisha kuzama kwa Meli hiyo. Mpaka leo hii hatujasikia adhabu walizopewa wahusika wa ajali ile.
Maana, bado tunakumbuka kuwa, ripoti ile ilibainisha kuwa miongoni mwa watu ambao walibainika na makosa katika ajali ya Mv Spice Islanders ni pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar, Haji Vuai Ussi, Mkuu wa kituo cha usimamizi wa usalama wa vyombo vya baharini wa Shirika la Bandari, Usawa Khamis Said na Kaimu Mdhibiti wa Bandari ya Malindi, Sarboko Makarani Sarboko.
Wengine ni pamoja na Wanahisa wa Kampuni inayomiliki meli hiyo Jaku Hashim Ayub ambaye ni Mwakilishi na Mbuge wa Jimbo la Muyuni, Salim Said Mohammed, Makame Hasnuu Makame na Yussuf Suleiman Issa.
Alikuwamo pia nahodha wa meli Said Abdallah Kinyanyite na wasaidizi wake, Ofisa usafirishaji wa Shirika la Bandari Hassan Mussa Mwinyi na Mkaguzi wa Meli wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini, Juma Seif Juma.
Ndiyo, wakati bado hatuna hakika ya hatua zipi zilichukuliwa dhidi ya wahusika hawa leo tunaomboleza msiba mwingine kwa taifa. 
Hakika, inasikitisha sana, kuwa hata mwaka haujatimu kukumbuka ajali iliyopita ya Septemba 9, 2011, Watanzania tunapatwa na msiba mwingine. Na misiba yote miwili inatokana na uzembe na wala si ya kusingizia ‘Kazi ya Mungu’.
Watanzania sasa tunataka kuona hatua kali za kisheria na kinidhamu zinachukuliwa, tena kwa haraka dhidi ya wahusika waliochangia kwenye ajali ile ya Mv Skagit.
Kwa kuanzia jina la mmiliki wa meli liwekwe hadharani. Na Tume itakayochunguza ajali hii itabaini kuwa mwenye meli ameingiza chombo chakavu, basi, awe wa kwanza kutolewa mfano.
Maana, kama taifa, bila kuwa wakali katika haya ya msingi, basi, tunahatarisha usalama wa taifa letu pia. Kamwe tusiruhusu hilo kutokea. Nahitimisha.

Saturday, July 21, 2012

Naibu spika Ndugai apindisha kanuni tena


Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano Mh Job Ndugai leo amepindisha kanuni waziwazi kufuatia hoja iliyotolewa na Mbunge wa kuteuliwa, ndugu James Mbatia kuhusu kuahirisha bunge.

Mheshimiwa Mbatia alitoa hoja hiyo mara tu waziri wa kilimo chakula na ushirika Mh chizza kumaliza kutoa majumuisho ya bajeti ya wizara yake.

Mh Mbatia alisema kwa kuwa idadi ya wabunge waliopo bungeni haifiki nusu ya wabunge ambao ni 176 kwa muda huo, kanuni haielekezi bunge kuendelea kufanya maamuzi ya kupitisha bajeti ya wizara hiyo.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge Mkosamali pamoja na Machali lakini Naibu spika aliamuru bunge kuendelea na kikao hicho. Kuona hivyo mnadhimu mkuu wa upinzani Ndugu Tundu lissu nae alisimama kuendelea kuomba kanuni hiyo kufuatwa lakini dhahiri shahiri Naibu spika alionekana wazi kutopendelea suala hilo kufanyika.

Chanzo- TBC LIVE - Bungeni leo
Mkali

Friday, July 20, 2012

Taarifa za hivi karibuni-Zanzibar kumechafuka tena


Kuna vurugu zinaendelea Zanzibar. Polisi wapiga mabomu na risasi kutawanya waislamu waliokuwa msikiti wa mbuyuni wakifanya muhadhara.(UAMSHO)
Ilikuwa zamu ya amir farid kuzungumza baada kumaliza kuzungumza kwa Shekhe suleiman haji,mara wakatokea polisi nakuanza kurusha mabomu bila sabab,.bila yakuzingatia taifa kama limo kwenye msiba kwa kupoteza jamaa zao.
 
Fuatilia taarifa mbali mbali za vituo vya television kwa taarifa zaidi usiku huu.

Chanzo: blogs mbalimbali na wikis.

Zitto aitaka Serikali Kuvirudisha Viwanda vya korosho kwenye Milki yake.



Kaimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, na mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe ametaka serikali kuvirudisha haraka viwanda kumi (10) vya korosho vilivyopo mkoani Mtwara katika milki yake.

 Akichangia bajeti ya wizara ya kilimo, iliyowasilishwa mapema asubuhi hii ya leo, Zitto amesema wamiliki wa viwanda hivyo wameshindwa kuviendesha viwanda hivyo kulingana na sheria za ubinafshaji.

Mheshimiwa Zitto amesema Tanzania huuza korosho ghafi kwa zaidi ya asilimia themanini (80%) nchi za nje bila ya kuziongezea thamani. Kwa kufanya hivyo Watanzania wengi wanakosa ajira ambazo wangezipata kupitia viwanda ambavyo vingeongeza thamani ya zao hilo.

Mkali
0688323837

Tani 300 za dawa mbovu kwa korosho zakamatwa Mtwara


Mtwara
OFISI ya Mkaguenzi Mkuu wa Afya ya Mimea, imekamata tani 300 za viwatilifu vya ‘salfa’ ya vumbi ambavyo havionyeshi mwaka ulivyotengenezwa wala siku ya mwisho wa kutumika kwake.

Viatilifu hivyo vimekamatwa katika ghala la kampuni moja inayojihusisha na usambazaji wa dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia maua ya korosho, lililoko mjini Mtwara.

Kukamatwa kwa kiasi hicho kikubwa cha viwatilifu,kunafuatia ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Afya ya Mimea, Cornelius Mkondo, katika maghala yanayohifadhi viwatilifu hivyo mjini Mtwara.

Viwatilifu hivyo vyenye jina la Falcon-S Dust licha ya kukosa mahali panapoonyesha muda wa kutengenezwa na mwisho wa kutumika, pia vimekutwa vikiwa vikiwa vimeganda mithili ya jiwe ili hali ni kiwatilifu cha vumbi.

Mkondo alisema kumbukumbu zilizopo katika mifuko iliyotumika kuhifadhia dawa hizo, zineonyesha kuwa zimetengenezwa India na zipo kwa majaribio na kwa msingi huo, haziruhusiwi kusambazwa kwa wakulima.

“Hapa zinaonyesha kuwa zipo kwa majaribio, kwa hiyo ni kosa la kisheria kuwasambazia wakulima, zinapaswa kufanyiwa majaribio kwa misimu mitatu halafu mamlaka husika ithibitishe,” alisema.

“Naizuia dawa hii kwa sasa isisambazwe kwa wakulima, nitachukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi na kama itabainika kuwa haifai kwa matumzi, itateketezwa na gharama hizo zitakuwa za kampuni hii,” alisisitiza Mkondo.

Hali hiyo imejitokeza wakati madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Masasi, wakilalamikia kusambaziwa kwa viwafitifu vya vumbi, viliyoganda, jambo linalowalazimisha wakulima kuitwanga kwenye vinu ili wapate unga.

Mmoja wa madiwani hao, Victor Mmavele alisema hivi karibuni katika kikao cha baraza kuwa wakulima wa kata yake ya Nanjota ni miongoni mwa waliokutana na adha hiyo.

Hali ya usambazaji wa pembejeo za ruzuku mkoani Mtwara, inaendelea kuwa tete kiasi cha kusababisha wakulima washindwe kuhudumia mikorosho yao.
Boharia wa kampuni hiyo ya Export Trading, ambayo ni miongoni mwa kampuni zilizopewa zabuni ya kusambaza viwatilifu vya ruzuku vya korosho kwa wakulima, Dismas Mtuhi alikiri kukutwa kwa tani hizo 300 za ‘salfa’ ya vumbi zikiwa zimeganda katika ghala lake na kwamba zilifikishwa katika ghala hilo kwa makosa na kwamba.

Alisema lengo lilikuwa kuzipeleka katika machimbo ya madini.
“Tumezipokea tangu Machi, mwaka huu, baada ya kuziona zimeganda tulizizuia, hatukusambaza kwa wakulima…hizi zililetwa huku kwa makosa, zilikuwa zinaenda machimbo ya madini…zipo tani 300” alisema Mtuhi

Thursday, July 19, 2012

Spika kung’olewa?


Baadhi ya wabunge wameanza kuwahamasisha wenzao kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge.
Wabunge hao walifikia hatua hiyo kwenye kikao cha dharura walichokifanya jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa kwa lengo la kufanya maandalizi ya kwenda Zanzibar kuhudhuria msiba wa wenzao waliozama katika ajali meli ya Skagit.

Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahimu Sanya (CUF), alisema Spika Makinda hana utu ndiyo maana aligoma kuahirisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi ya watu kushiriki kwenye jambo hilo.

“Huyu Spika hatufai, yaani vifo vikitokea kwa watu wa Bara yeye ndiyo ataona kuna uzito…hapa alikufa Amina Chifupa tukaahirisha Bunge, sasa iweje wenzetu wamekufa kule Zanzibar yeye akatae kuahirisha shughuli za Bunge? Jamani tujipange kupiga kura za kutokuwa na imani naye, ameonyesha kushindwa kulihimili Bunge,” alisema.

Mbunge mwingine kutoka Zanzibar alisema hawaoni sababu ya kuendelea na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu wapiga kura wao ndio waliofariki dunia.

“Tuna raha gani ya kuendelea kujadili hotuba ya bajeti, huyu Spika tumedhihirisha hana uwezo wa kutuongoza, hatufai, waliokufa kule ni binadamu si paka wala wanyama,” alisema.


 Chanzo:Tanzania daima

Wednesday, July 18, 2012

Watu saba wafariki dunia kwenye ajali ya meli Zanzibar


Waziri Emmanuel Nchimbi akiongea na TBC1 amesema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”

Chanzo: TBC 1.

Mwito wa Polisi, Singida: Yanayojiri!- Mnyika


Nimefika Singida kuitikia mwito wa Polisi kutoa maelezo kuhusu mkutano nilioalikwa Iramba kwa nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Nimekutana na RPC, amesema kwamba nisubiri mpaka saa 10:30 alasiri ndiyo nikutane nao kwa kuwa kwa sasa kuna kikosi cha upelelezi toka Dar Es Salaam kimekwenda eneo la tukio. Nimemuuliza RPC maswali mawili;

1. Wameniita kutoa maelezo kama mtuhumiwa au shahidi?
Amenijibu kuwa ni mahojiano ya kawaida.

2. Kwanini mpaka sasa watuhumiwa 12 waliofunguliwa jalada NDG/RB/190/2012 kwa kurusha mawe kwenye mwanzo wa mkutano wakati Bwana Waitara akitoa hotuba ya utangulizi huku polisi wakiachia hali hiyo. Baada ya kufungua jalada na polisi wa juu kupigiwa simu kuwa kuna njama kati ya Polisi na CCM hali ilitulia, Waitara akamaliza hotuba yake, Dkt Kitila akasalimia name nikahutubia kwa amani na kwenda kwenye mkutano mwingine. Mauaji yalitokea baadae mbali na tulipohutubia.



John John MNYIKA,

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)

18 Julai, 2012

Meli yazama kisiwa cha Tumbe Zanzibar


Kuna habari za sasa hivi meli iliyokuwa imebeba abria zaidi ya 200 ikitoka dar kwenda zanzibar imezama muda SI mrefu,chanzo breaking news radio one Kwa Habari za Kinai tutazidi kuwajulisha
www.mjengwablog.com

Tuesday, July 17, 2012

Majibu..how many triangle are there in this diagram?


Swali lilikuwa hapo juu...

Hapa chini ndio majibu..triangle zipo 26 kama hakuna intesection kama hujalizika nitafute. Fuatilia solutions.



Mkali
0688323837,0719466466

Tutibu kiini cha tatizo sekta ya nishati na umeme-Mnyika


Kwa nafasi ya Uwaziri Kivuli wa Nishati na Madini,nafahamu kuna ufisadi na ubadhilifu ndani ya TANESCO ambao uchunguzi ni muhimu kwa ajili ya uwajibikaji.Kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa TANESCO na maafisa wengine wa shirika hilo kupisha uchunguzi ni muhimu,lakini si muarubaini wa uozo wa kimfumo katika sekta ya nishati nchini nitatoa vielelezo vya kina wakati nitakapo wasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni katika wizara ya Nishati na Madini.

Hata hivyo ni vyema nikatahadharisha mapema kuwa tukio hili linapaswa kutafakariwa kwa upana kwa kuwa linahusisha masuala mengi ambayo mengine Bodi ya Wakurugenzi imeyaacha nyuma ya pazia.Ukweli wote utakapotoka hadharani wengine zaidi watapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa maslahi ya Taifa!

Kwa nyakati mbalimbali toka mpango wa dharura wa umeme uwasilishwe bungeni,nimekuwa nikiitahadhalisha na kuihoji serikali(kama sehemu ya jukumu langu la kibunge) kwa uzembe,ufisadi na udhaifu wa kiutendaji katika serikali ambao hasara yake utairejesha nchi katika mgao wa umeme hali ambayo imedhihirika hivi sasa!

Kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa Tanesco na watendaji wake ni kafara ya kuficha uzembe na udhaifu wa serikali kwa ujumla wake kwa kuwa taarifa za utendaji wa Tanesco kuhusu mpango wa dharura wa umeme zimekuwa zikijadiliwa kwenye vikao vya wizara ya nishati na madini na hata vikao vya baraza la mawaziri bila hatua muafaka kuchukuliwa.Ninazo nyaraka za ndani za serikali na taasisi zake.Iwapo serikali haitatoa kauli bungeni ni kwanini Waziri wa Nishati na Naibu wake anayehusika na Nishati kutoa taarifa potofu bungeni kuwa hakuna mgao wa umeme,aidha waeleze mkakati dhaifu waliokuwa wakiufanya kupunguza mgao katika kipindi cha bunge ili kuficha udhaifu na uzembe uliokithiri serikalini na katika wizara mahsusi!

John John Mnyika,
Mbunge wa Ubungo (Chadema),
16 Julai,2012

Mhando aivuruga Serikali, wabunge


Fredy Azzah
HATUA ya Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando imeibua mvutano kati ya wabunge na Serikali.
Mwishoni mwa wiki, bodi hiyo iliwasimamisha kazi Mhando, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Huduma za Tanesco, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Ununuzi, Harun Mattambo.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge walio katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na wengine wa Kamati ya Nishati na Madini, wamesema uamuzi huo umejaa maswali kuliko majibu.

Moja ya maswali hayo ni mchakato wa kumsimamisha wakihoji kikao kilichochukua uamuzi huo kuitishwa na wizara badala ya bodi, kupatikana Mkaguzi Kampuni ya Ernst&Young kukagua hesabu za Tanesco bila kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma na tuhuma za ukabila dhidi ya bosi huyo wa Tanesco.

Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo za wizara kuingilia mamlaka ya bodi, alijibu: “Kesho (leo) tunakutana na kamati, kwa hiyo siwezi kuzungumza chochote nitazungumza ndani ya kamati.”

Hata hivyo, habari kutoka kamati hizo za Bunge zinasema mkutano kati ya watendaji wa wizara, bodi na wajumbe wa kamati hizo unatarajiwa kuwa na mvutano mkali.

Tayari baadhi ya wajumbe wa POAC wamehoji tuhuma za ukabila ambazo anatuhumiwa kuwa nazo Mhando, huku wakimnyooshea kidole Maswi na waziri wake.

“Hivi Mhando ukabila wake ni nini...? Hivi, tunapaswa kujadili uwezo wa mtu au kabila lake?” alihoji mmoja wa wajumbe wa POAC.

Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alipoulizwa kuhusu kikao chao cha kesho alisema tayari wameshamwandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na wanatarajia kukutana na bodi kupata ufafanuzi.

Kusimamishwa Mhando
Hatua hiyo ya kumsimamisha Mhando ilitangazwa mwishoni mwa wiki na bodi hiyo baada ya kikao cha dharura ambacho kilijadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya Tanesco.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert Mboma na kuchukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

“Hivyo, Bodi iliazimia pamoja na mambo mengine, kama ifuatavyo: Uchunguzi wa tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini,” ilieleza sehemu ya taarifa aliyoitoa Mboma kwa vyombo vya habari.

Mhando aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Juni Mosi, 2010 akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Dk Idris Rashidi ambaye alimaliza muda wake wa uongozi.

Mara baada ya uteuzi huo, Mhando alisema kwamba moja ya mambo ambayo atahakikisha anayatekeleza ni kuhakikisha kuwa wateja wote wa shirika hilo wanakuwa na mita za Luku.

Kabla ya uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo.

 

Monday, July 16, 2012

Benki KKKT Yalizwa 250m Kupitia ATM

 
Daniel Mjema, Moshi
WATEJA zaidi ya 50 wa Benki ya Uchumi Commercial Bank Ltd (UCB) ya Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wanasakwa na polisi kufuatia wizi wa karibu Sh250 milioni.
Vyanzo vya kuaminika vilidokeza kuwa ingawa taarifa zilizofunguliwa polisi na menejimenti ya UCB zinaonyesha kiasi kilichoibwa ni Sh224 milioni, lakini kinaweza kufikia Sh250 milioni kadri uchunguzi unavyoendelea.
Benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 baada ya kupatiwa leseni namba CBA 00031 na Benki kuu ya Tanzania (BoT), inamilikiwa na Watanzania wapatao 330,000 ambao ni waumini wa dayosisi hiyo.
Habari za uhakika zilizolifikia Mwananchi zilisema wizi huo ulifanyika baada ya kuparanganyika kwa mfumo wa kompyuta uliounganishwa na mashine za ATM.
Taarifa nyingine zilisema wizi huo ulitokana na baadhi ya wateja kuusoma mfumo wa kompyuta hiyo na kugundua kuwa kuna nyakati za usiku huchanganyikiwa na kutoa salio lisilo sahihi la wateja.
“Kilichotokea ni kuwa kuna watu walivujisha siri kuwa nyakati za usiku sana ukichomeka kadi kwenye hiyo ATM inatoa pesa hovyo hovyo hata kama hauna salio la kutosha”kilidokeza chanzo chetu.
Uchunguzi wa Mwananchi ulibaini kuwa wateja wa benki hiyo wapatao 50 walijihusisha na wizi wa fedha hizo kupitia ATM hiyo na tayari polisi imeanzisha uchunguzi maalumu wa kuwasaka.
Habari hizo zimedai kuwa baada ya kugundulika kwa dosari katika mfumo huo wa kompyuta za ATM katika benki hiyo, baadhi ya wateja walianzisha kuchukua fedha muda mfumo huo unapoharibika.
“Sio pesa zilizoibwa mara moja hapana yaani unakuta leo anatoa 500,000 kesho hivyo hivyo na ilikuwa ni wateja tofauti tofauti waliokuwa wamegundua siri hiyo”alidokeza mtumishi mmoja wa UCB.
Baadhi ya wanasheria walidai zipo changamoto nyingi katika kesi za aina hiyo hasa katika kuthibitisha kama wakati mtuhumiwa anatoa fedha hizo katika ATM,alikuwa amekula njama ya kutenda kosa hilo.
Meneja mkuu wa Benki hiyo, Angela Moshi alipoulizwa alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini akasema hakuwa katika nafasi nzuri ya kulielezea kwa vile alikuwa akielekea kanisani kwa ajili ya ibada.
"Naomba uje kesho (leo)tutazugumza vizuri tu juu ya hilo jambo nitakupa taarifa vizuri tu unajua leo ni siku ya ibada na sasa hivi naingia kanisani kwa ajili ya ibada"alisisitiza Meneja mkuu huyo jana.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz alipoulizwa na gazeti hili juzi alisema“ni kweli hilo tukio lipo kwa maana ya wateja ‘wame overdraw’ (wametoa zaidi) kutoka kwenye akaunti zao na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea”alisema Kamanda Boaz.
 

Shivji: Kutoijua katiba iliyopo kusiwafunge midomo


Joseph Zablon
TANZANIA hivi sasa inapita katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni juu ya katiba mpya baada ya ile ya mwaka 1977 ambayo iliundwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa wakati huo.
Mchakato huo unakuja huku kukiwa na maoni tofauti juu ya mfumo wa kukusanya maoni pia kuna watu ambao wanadai kuwa hawataweza kutoa maoni kwani hawaijui katika iliyopo.
Hata hivyo, Profesa Issa Shivji wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, anapingana na dhana kuwa ili uweze kuchangia vizuri katiba basi lazima uijue iliyopo.
Anasema hoja hiyo haina mashiko na imekuwa ikitumiwa na watawala kuwafumba midomo wananchi kutoa maoni yao na wao kujifanyia wanavyotaka.
Profesa Shivji anasema hoja ya msingi ni je, katiba ya sasa ni muafaka juu ya mifumo iliyopo? Na anasema mtu si lazima awe msomi ili kuweza kujua kuwa mifumo iliyopo katika katiba haifai.
Anasema mathalani mtu anaposhindwa kumpeleka mtoto wake shule, wananchi wanapolalamikia ukosefu wa barabara ni wazi mfumo uliopo hauna msaada kwao.
"Ukusanyaji wa maoni hautegemewi kuwa mwananchi wa kawaida eti atasema Ibara namba fulani siipendi, hakuna kitu kama hicho" anasema.
Profesa huyo anabainisha kuwa ni wajibu wa wasomi kufanya uchambuzi, iwapo mwananchi anasema hana barabara anamainisha nini.
Shivji anasema ili kupata katiba kwa amani ni lazima yawepo majadiliano huru na ya wazi katika kila eneo kuanzia katika migahawa, maofisini, mitaani na kwingineko.
Anasema mijadala ndio ambayo itazaa muafaka wa katiba kwani kupitia majadiliano watu watatoa maduku duku yao, kero zao, matumaini yao na changamoto ambazo zinawakabili.
Profesa Shivji anasema ili wananchi waweze kuchangia kwa upana katiba mpya ni vizuri wakajua historia ya katiba iliyopo, kuanzishwa kwake na dhana ya katiba kwa ujumla wake.
Shivji anawaonya wananchi kuwa makini na vyama ambavyo vinadai kuwa vinatetea maslahi ya wanyonge na kusema kuwa vinaweza vikawa na migongano ya kimaslahi baina yao.
MAANA YA KATIBA
Profesa Shivji anasema nenno katiba lina tafsiri tofauti kulingana na kulingana na uelewa wa watu kwani wanasheria wanaamini kuwa katiba ni sheria mama au ya msingi ambayo inabeba zingine zote.
"Wanamainisha kuwa sheria zote zinazotungwa ni kwa mujibu wa katiba na vyombo vya utungaji wa sheria hizo pia vimewekwa kwa mujibu wa katiba" anasema.
Anasema wanasheria bobezi wamekuwa wakidai kuwa katiba ni kanuni za kisheria zilizokusanywwa katika nyaraka mahsusi zinazohusu mhimili mitatu na haki za binadamu.
Msomi wa sayansi ya siasa anasema Shivji kuwa atasema katiba ni mkataba wa kijamii baina ya watawala na watawaliwa.
Dhana hiyo ya katiba mkataba anasema inatokana na wanafalsafa wa Uingereza John Louis na Thomas Hopes miaka ya mwanzoni ya 1900.
Anasema wakati ule mfumo ambao ulianza kuenezwa ulikuwa wa kibepari ambao ulijikita katika bidhaa (ununuzi na uuzaji) hivyo dhana ya mkataba ikawa inatawala.
Mwanafalsafa anasema kuwa walitumia dhana hiyo ya mkataba kueleza katiba na hata wasomi wa sasa wakiulizwa watawala na watawaliwa walitoka wapi ili kufunga mkataba wakati ule hawatakuwa na jibu.
Anasema, wasomi wa siasa uchumi wanaamini kuwa katiba ni muafaka wa wananchi kuhusu misingi na mfumo wao wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
"Maana zote tatu za katiba zina ukweli katika maana zote tatu lakini sio ukweli kamili kwa sababu ni kama hadithi ya vipofu na wasifu wa tembo" anasema.
Profesa huyo anasema kila mmoja alimuelezea tembo anavyomjua kulingana na pale alipomshika mnyama huyo hivyo kufanya asiwepo ambaye ana wasifu kamili wa mnyama huyo.
DHANA YA KATIBA
Anasema Shivji kuwa ili kuelewe katiba ni lazima dhana yake ikaeleweka na ni vigumu kuelewa dhana ya katiba bila kuangalia historia
"Kwangu mimi dhana ya katiba inatokana na historia ya nchi za Ulaya na ni lazima kukiri kuwa itikadi na hata dini zetu zinatokana na nchi hizo" anasema.
Anabainisha kuwa wazungu ndio ambao walitawala ulimwengu katika karne ya 15 na hadi leo hii labda bado dhana nyingi zinatokana na wao ikiwa ni pamoja na masuala ya elimu.
Historia ya dhana ya katiba anasema ilizaliwa wakati wa mchakato wa mageuzi na mapinduzi ya kutoka katika mfumo wa ukabaila kwenda wa kibepari.
Anafaafanua kuwa mfumo wa ukabaila msingi ambao ulikuwa unawajumuisha mabwana na watwana ambao ulifanya mkuu wa mamlaka kuwa mfalme.
"Chini yake walikuwepo mamwinyi ambao walikuwa wamehodhi umiliki wa ardhi" anasema na kuongeza kuwa mfumo huo ulihalalishwa na itikadi za dini.
"Kuubadili mfumo watawala wakati huo wakaleta utawala waliouita wa sheria ambao msingi wake ni ubepari" anasema na kwa kutumia misingi hiyo ndipo ilipozaliwa dhana ya katiba.
"Turidhia dhana hiyo kwa sababu tulitawaliwa na nchi za magharibi" anasema hata katiba mbili zilizopata kuandikwa kabla na baada ya uhuru zinaegemea huko.
Shivji anasema mapambano ndio ambayo yalizaa dhana ya katiba na suala hilo likiwekwa katika nadharia anasema kuwa katiba kama sheria ni uwanja wa mapambano.
"Wahenga wanasema sheria ni msumeno maana yake shheria ni uwanja wa mapambano ni vizuri sana kina mwanananchi akaelewa hilo" anasema.
Profesa Shivji anaongeza kuwa anaposema hivyo anamainisha kuwa kuna mgongano wa kimaslahi baina ya wanajamii kutokana na Taifa kugawanyika kimatabaka hivi sasa.
Anasema mgongano ni lazima kutokana na jamii kugawanyika katika makundi tofauti na njia pekee ya kupata muafaka wa katiba kwa njia ya amani ni majadiliano.
Anasema upande mmoja wa makundi hayo wapo watawala wa kiuuchumi kwao katiba ni chombo cha kuhalalisha utawala wao ili udumu na mfumo wa uchumi wanaosimamia usisambaratike.
"Hivyo kama wana mgongano ni wazi kuwa Taifa linaweza kusambaratika ndio maana wanaotawala muhimu kwao ni kuhalalisha utawala wao na ule kiuchumi ili ukubalike na watawaliwa.
Upande mwingine watawaliwa ambao ni wengi katiba ni fursa kwao ya kuweka mipaka na madaraka ya watawala ili angalu wasikandamizwe na haki zao zisibanwe.
Pia kundi hilo linataka maslahi yao angalau yatambuliwe katika katiba
Anasema Shivji kuwa ni vigumu kuangalia dhana ya katiba bila kuangalia muktadha huo wa mapambano lakini la msingi ni kuwa lazima uwepo muafaka.
"Huo muafaka baada ya mgongano ndio ambao utaingia katika katiba na ni wa kiasi gani itategemea nguvu za mvutano wa matabaka"anasema.

Lissu sasa matatani


Waandishi Wetu, Dodoma
MNADHIMU wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ameingia matatani kutokana na kauli yake kwamba Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiteua majaji wa Mahakama Kuu wasiopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Kutokana na kauli hiyo aliyoitoa wakati akiwasilisha maoni ya kambi yake, kuhusu hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) atajadiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Wakati akisoma hotuba yake, mbunge hiyo alisema majaji wanaoteuliwa na Rais hawafanyiwi vetting (uchunguzi) na tume hiyo kuona kama uwezo na ujuzi wao unafaa kukabidhiwa madaraka ya ujaji.

Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama ndiye aliyeamuru suala la Lissu kupelekwa katika kamati hiyo baada ya mbunge huyo kukataa kufuta kauli yake ambayo kwa mtazamo wa Serikali iliwadhalilisha majaji.

Hata hivyo, jana alipotakiwa kueleza kama ana taarifa rasmi za kuitwa kwenye kamati hiyo Lissu alisema: Sijaitwa, lakini nina taarifa kuwa naweza kuitwa.

Alisema, hata wakimwita hatakuwa na jambo lolote la kuzungumza kwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge aliyeongoza kikao hicho juzi (Jenista Mhagama), alikosea kwa kuwa ndiye aliyepaswa kumpa adhabu.
Mbunge huyo alisema, juzi aligoma kufuta kauli yake kama alivyotakiwa na Mwenyekiti kwani aliamini kuwa hata Mwanasheria Mkuu alikuwa amekosea.
Alibainisha kuwa endapo ataitwa katika kamati hiyo, atahoji kama waliomwita wamegeuka kuwa wenyeviti wa Bunge na kama si hivyo, anaamini watakosa neno la kumhoji.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kwa nyakati tofauti wakati wakijibu hoja za wabunge juzi jioni walisema: Lissu aliwakashifu majaji bungeni, hivyo alipaswa kuomba radhi.

Kwa upande wake Werema alimtaka Lissu kufuta kauli yake na kwamba ikiwa hatafanya hivyo basi awasilishe vielelezo vinavyothibitisha madai kwamba majaji huteuliwa bila kufanyiwa uchunguzi.

Lissu ni mtaalamu wa sheria, lakini kauli yake  imewafedhehesha majaji na inashangaza inapotolewa na wakili machachari kama yeye, alisema Werema.

Werema pia alimtaka Lissu kuondoa kauli yake kwa kuwataja watu ambao sio wabunge kwa kunukuu gazeti la Mwanahalisi lililowataja watu watatu kuwa wamehusika na mauaji ya Dk Steven Ulimboka.

Werema alisema iwapo Lissu hataondoa maneno yake suala hilo lipelekwe katika Kamati ya Maadili.

Kwa upande wake, Chikawe alimwombea radhi Lissu kwa majaji akisema anajua hakutoa kauli ya kuwadhalilisha majaji kwa kukusudia.

Lissu amemtuhumu hadi Rais katika uteuzi wa majaji, hili siyo sahihi, uteuzi wa majaji hupendekezwa na tume maalumu inayohusisha majaji wazoefu ambao ndio wanapendekeza majina kwa Rais, alisema Chikawe.

Baada ya maelezo hayo, Mhagama aliamuru Lissu kuondoa kauli yake hiyo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Werema wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa wizara hiyo.

Hata hivyo, Lissu alipopewa nafasi alisema hawezi kuondoa kauli yake kwa kuwa mchakato mzima wa kumtaka afanye hivyo haukufuata Kanuni za Bunge.

Lissu alinukuu kanuni ya 63 (1) ambayo inasema: Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kabisa kusema uongoƂ bungeni kwa sababu hiyo, mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni kweli na siyo jambo la kubuni au la kubabaisha tu.

Lissu aliongeza kuwa, Jaji Werema na Mhagama walivunja Kanuni za Bunge kwa kumtaka kuondoa kauli inayodaiwa kuwa ya uongo kinyume bila kufuata utaratibu.

Alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo jana, Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alisema kuwa siyo lazima kwa Watanzania kufahamu hilo.
Nilipozungumza jana (juzi) sikuzungumza na Watanzania bali nilizungumza na Bunge, hivyo siyo lazima Watanzania kufahamu jambo hilo na wala sioni sababu za kwa nini liandikwe magazetini, alisema Jaji Werema.