Pages

Thursday, November 29, 2012

Polisi waua Raia Dar

                                   
 
Kijana mmoja huko Tegeta amepigwa risasi ya moto na kufariki na wengine kujeruhiwa vibaya sana baada ya polisi kurusha risasi hiyo wakiwa kwenye operesheni ya kuondoa magari yanayopaki barabarani.
Kijana huyo alikuwa kwenye duka la magodoro akifanya manunuzi.
 
Chanzo: Jamii Forum

Sunday, November 25, 2012

Dr. Kitila Mkumbo: Kushangilia utekelezaji wa majukumu ya serikali ni Uzuzu!

 
Pamoja na mambo mengine akiongea katika kipindi cha changamoto kinachorushwa na startv Dr.Kitila Mkumbo wa Udsm amesema kushangilia utekelezaji wa majukumu ya serikali ni uzuzu.

"Watu wanashangilia kama mazuzu eti serikali imetujengea barabara ya lami wakati ni haki yao kujengewa barabara na huo ni wajibu wa serikali kuwaletea wananchi maendeleo hakuna haja ya kushangilia na kuwapongeza mawaziri"

Amesema miongoni mwa mambo yanayofanya huduma za jamii kuwa mbovu ni pamoja na gharama kubwa ya uendeshaji wa serikali(utawala),"serikali inaacha kuwajengea wananchi zahanati,shule lakini inakimbilia kuongeza mikoa na wilaya jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida."Hiyo mikoa mipya inamsaidia nini mwananchi?amehoji.

"Ukitaka kuharibu taifa ua elimu,Somalia wamefika pale walipo kwa sababu waliua elimu na ndio maana mpaka leo wako vile walivyo.

Akiongelea Swala la katiba mpya amesema ilitakiwa utaratibu wa ukusanywaji wa maoni uboreshwe zaidi kwa kushirikisha mawazo ya vyama vya siasa kama Chadema na vinginevyo,Amesema mwananchi hana haja ya kujua maana ya katiba bali aseme nini anataka kifanyike kwa ajili ya maisha yake.

Friday, November 23, 2012

Mawaziri wazomewa mbele ya KInana Mkoani Mtwara

 
MAWAZIRI watatu wa Rais Jakaya Kikwete juzi walizomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.

Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Mtwara ambako Kinana na mawaziri hao walikuwa katika ziara ya chama kujibu kero mbalimbali za wananchi.Mawaziri waliokumbwa na dhahama hiyo ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) Naibu wake, Aggrey Mwanri.

Chiza ndio alikuwa wa kwanza kukumbana na zomeazomea hiyo, lakini mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Ghasia ambaye alizomewa tangu alipoanza kuzungumza mpaka alipomaliza.Ghasia ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Vijijini, alirushiwa makombora na Rukia Ismail Athumani ambaye alimshutumu yeye pamoja na Mbunge wa Mtwara mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

“Ghasia na Murji kwanini mnaudanganya umma kwa kupeleka gesi Dar es Salaam, sisi hatuna ubaya na chama ila hatutaki gesi iende huko” alisema Athumani huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.Kabla ya dada huyo kuteka hisia za wananchi kwa kuwasilisha kero hiyo, Kinana alimruhusu mwananchi mwingine, Issa Kambona ambaye pia alieleza kuwa hakubaliani na suala la gesi hiyo kupelekwa Dar es Salaam.

Kinana alisema amesikia hoja hizo za wananchi na kwamba atamueleza Waziri wa Nishati na Madini azungumze na wananchi wa Mtwara kuhusu gesi hiyo.Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu, Ghasia alilazimika kupanda jukwaani kujibu makombora aliyokuwa akirushiwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

“Sio kweli kwamba hatutetei maslahi yenu, gesi iliyopo ni nyingi hamuwezi kuitumia na kuimaliza, kuna futi za ujazo trilioni 20,000 na tunaweza kuitumia kwa zaidi ya miaka 90, hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini imetoa ofa ya kuwalipia chuo vijana 150 kila mwaka,” alisema Ghasia, lakini wananchi hao waliendelea kumzomea.“Uongo, uongo, hatutaki, hatutaki, huyoo, huyooo” walisikika wakisema wananchi hao, hali iliyomfanya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kuingilia kati, kujaribu kuwatuliza.

“Kelele unazozisikia dada (Ghasia) zinaashiria kuna jambo, nafasi hizo 150 hawazipati, kama zinatolewa basi kwa upendeleo,” alisema Nape huku akishangiliwa na wananchi hao.Baada ya hali kutulia kiasi, Ghasia alijaribu kuendelea kutoa ufafanuzi, lakini kitendo cha kuanza kuzungumza, wananchi hao walianza tena kuzomea.

“Kila mtu amelelewa katika mazingira tofauti, hilo halinihusu…watu wangu wa Mtwara vijijini wamenielewa,” alisema Ghasia na kuteremka jukwaani hali iliyozidisha kelele za kumzomea.Nape alisawazisha mambo kwa kusema, hoja ya wananchi hao imechukuliwa na itawasilishwa kwa Serikali ili kuona namna ambavyo inaweza kukaa na wananchi hao na kuweka maslahi yao mbele.

Ilivyoanza
Panzia la zomea zomea lilifunguliwa na Chiza alipopanda jukwaani kujibu hoja ya kuyumba kwa soko la zao la korosho, ambapo wananchi walimpinga baadhi ya kauli alizozitoa.“Tatizo la korosho ni baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na wengine ni watendaji wa Serikali …nipo hapa na wala siondoki, nitalishughulikia hili ili korosho zinunuliwe” alisema Chiza huku sauti za wananchi zikimpinga kwa kusema “uongooo”.

Hata hivyo, Chiza aliweza kukabiliana na hali ya zomeazomea jukwaani baada ya watuliza wananchi kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuwapo Mtwara, kushughulikia tatizo hilo ili ununuzi uendelee.Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwanri alipata wakati mgumu mara alipopanda jukwaani na kuanza kuzungumzia namna ya kumaliza kero ndogondogo zinazoletwa na mamlaka zake, wananchi walikuwa wanazoea “huyoo…hatutaki” lakini baada ya kuanza kuongea alionekana kuiteka hadhira na mambo yakawa shwari. “

“Tumesema wauza vitumbua, wasibughudhiwe … mkurugenzi njoo jukwani, nakuagiza kuanzia leo marufuku wanafunzi kurudishwa shuleni kwa sababu ya michango” alisema Mwanri huku akishangiliwa.Awali Kinana alisema mkutano huo unalenga kuzipatia ufumbuzi kero za wananchi ambazo zinawezakuwa kikwazo kwa chama hicho kuingia madarakani mwaka 2015.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala alisema umefika wakati wa chama kusimamia utendaji wa Serikali kutatua kero za wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni pamoja na kuyumba kwa soko la korosho na gesi.“Najua hapa kuna kero kubwa mbili, korosho na gesi, nimekuja na Mawaziri hapa watatoa majibu leo” alisema Kinana huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu ulioudhuria mkutano huo.

Sifa mgombea urais
Katika hatua nyingine, Kinana amevunja ukimya kuhusu mbio za urais mwaka 2015 na kusema CCM itamtosa bila kumuonea haya mwanachama yeyote atakayeomba kuteuuliwa kugombea urais kwa tiketi yake, huku akiwa kinara wa kutegemea makundi kumwigiza katika nafasi hiyo.Badala yake akaeleza kuwa chama hicho kitamteua mgombea mwadilifu, anayekubalika na watu na asiye na makundi.

Mbali na sifa hizo Kinana pia ameeleza kuwa mgombea huyo wa CCM atakuwa msafi, makini, mchapakazi, mzalendo ambaye anajali maslahi ya wananchi na kwamba Mei 2015 wataanza kutoa fomu kwa wana CCM wanaowania nafasi hiyo.Kinana alisema hayo jana katika kijiji cha Isesa, Sumbawanga Mjini wakati akifungua tawi la CCM na kuzungumza na wanachama.

Katika kipindi cha kuuliza maswali, wanachama hao walitaka kufahamu namna chama hicho kilichojipanga kumpata mgombea urais makini ambaye hatakuwa mzigo kumnadi dhidi ya wapinzani.“Tumejipanga vizuri, atapatikana mgombea urais bora, vigezo vipo wazi tunataka mgombea urais mwadilifu, makini, mchapakazi, mzalendo ambaye anakubalika na wananchi,”alisema Kinana.

Aliongeza kwamba chama hicho kitatoa fomu kwa wanaotaka kuwania nafasi hiyo na vikao vya chama ndivyo vitakavyoamua,”alisema Kinana.“Tuna utaratibu mzuri wa kupata wagombea urais bora kwa sababu vigezo vyote viko wazi na kwamba wagombea hao watapimwa kwa vigezo hivyo,” alisema Kinana.

Alisema Wanasumbawanga wasiwe na wasiwasi watampata mgombea ambaye atakuwa mwiba kwa vyama vya upinzani.Alisema kiongozi mwenye makundi na asiyekuwa mwadilifu hatakuwa na nafasi ya kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.“Haya si maneno yangu bali ni vigezo vya chama vilivyo wazi ambavyo vinatumiwa kwa kila mgombea wa nafasi hiyo kubwa kushinda zote,” alisema

Alisema anakifahamu chama hicho na kwamba kitavitumia vigezo hivyo ili kupata mgombea urais ambaye wananchi wanamkubali.Awali wanachama wa chama hicho wakiongea kwa hisia kali, walisema wanataka chama hicho kimsimamishe mgombea urais atakayekuwa mwiba kwa wapinzani.

“Tunayasikia majina ya watu wanaowania nafasi hizo, chonde chonde katibu mkuu tunaomba apatikane kiongozi ambaye hatatupatia kazi ya kumnadi, awe mwadilifu ambaye akitangazwa watu wafurahi bila kunung’unika,” alisema Peter Lilata.Alisema, “tukikosea kuteua kiongozi bora tutakuja kujuta hapo baadaye.”

Vijana CCM, Chadema nusura wazipige
Katika ufunguzi wa tawi la CCM la Isesa nusura vijana CCM na wa Chadema watwangane makonde baada ya vijana wa Chadema kuwatuhumu CCM kwamba wamewaibia bendera ya chama chao.

Mabishano kuhusu bendera hiyo yaliendelea katika kipindi chote ambacho Kinana alikuwa akizungumza na wanachama wa tawi hilo.“Hawa CCM wameng’oa bendera yetu hapa huo siyo ustaraabu ni lazima mturudishie bendera yetu vinginevyo patakuwa hapatoshi,” mmoja wa vijana wa Chadema alisikika akisema.
Hata hivyo, busara za askari polisi waliokuwa katika mkutano huo zilisaidia kuzima hasira zavijana wa Chadema.
 
Source: Mwananchi

Tuesday, November 20, 2012

Upelelezi kesi ya LULU bado gizani

 
Na :James Magai
KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, imeendelea kupigwa kalenda kutokana na upelelezi wake kutokukamilika.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa marehemu Aprili 7, mwaka huu.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Agustina Mmbando, jana ilitajwa mahakamani hapo lakini kwa mara nyingine upande wa mashtaka uliendelea kudai kuwa upelelezi haujakamilika.Wakati kesi hiyo ilipotajwa Novemba 5, mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilisha ili hatua nyingine ziweze kufuata, Wakili wa Serikali, Seth Sekwao alidai upelelezi haujakamilika.

Kutokana na taarifa hiyo ya upande wa mashtaka, mmoja wa mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Peter Kibatala alitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo, ili iweze kusonga mbele.

Wakili Kibatala, ambaye pia ni Makamu Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alidai kila mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika, jambo ambalo linaifanya kesi hiyo ishindwe kuendelea katika hatua nyingine.

“Ni muda mrefu sasa, kesi hii imekuwa ikitajwa mara kwa mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika. Hivyo tunawakumbusha upande wa mashtaka ujitahidi kuharakisha upelelezi ili iweze kusonga mbele,” alidai Wakili Kibatala.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka huu itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.Lulu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili 11, mwaka huu na kusomewa shtaka moja la mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

Akimsomea shtaka hilo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Elizabeth Kaganda alidai Aprili 7, mwaka huu eneo la Sinza Vatcan alimuua msanii, Steven Kanumba.
Source: Mjengwa blog

Sunday, November 18, 2012

Kinana acharuka: Adai kampuni ni yake lakini meno ya tembo si yake!

 
KADA maarufu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema hahusiki na usafirishaji wa meno ya tembo nje ya nchi, ikiwa ni siku moja tu tangu gazeti moja la wiki, lichapishe habari iliyomuelezea kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyosafirisha meno hayo.

Hata hivyo, kada huyo amekiri kuwa mmiliki wa Kampuni ya uwakala wa meli ya Sharaf Shipping Agency, iliyohusika kusafirisha makontena yaliyokuwa na nyara hizo za serikali, kabla ya kukamatwa nchini China yakiwa safarini kupelekekwa Hong Kong.

Gazeti hilo lilimtaja Kinana kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa na hisa 7,500 kati ya 10,000 katika kampuni hiyo, huku hisa nyingine 2,500 zikiwa zinamilikiwa na mshirika mwenzake, Rahma Hussein. Thamani ya hisa hizo ni sh 1,000 kila moja.

Kinana alitoa ufafanuzi huo katika mahojiano maalum na Tanzania Daima.

“Nimeisoma habari hiyo na kwa bahati mbaya sioni anayenilaumu wala kitu ninacholaumiwa nacho. Kwamba nina hisa katika kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf ni kweli.

“Lakini mimi sina nafasi yoyote ya kiutendaji na wala sishughuliki na uendeshaji wa kampuni hiyo. Kwa kweli sikujua na wala sikuhusika kwa namna yoyote ile na usafirishaji wa makontena hayo na mengine yoyote,” alisema Kinana.

Alisema anachojua yeye ni kwamba, maofisa wa kampuni hiyo waliuliza na kuambiwa kuwa shehena iliyokuwa katika makontena hayo ni plastiki zilizotumika.

Alifafanua kuwa, wenye wajibu na mamlaka ya kukagua shehena zote zinazosafirishwa nje ya nchi ni mamlaka za serikali na si kampuni ya uwakala wa meli.

Alisisitiza kuwa, hana mamlaka kwa mujibu wa sheria kukagua mali inayosafirishwa japokuwa anaweza kuuliza bidhaa iliyopo katika makontena hayo.

“Ni dhahiri kabisa kwamba, habari hii imeandikwa na jina langu kutumika katika malengo ambayo siyajui. Nahisi kama jina langu limetumika kama pilipili katika kachumbari ili kunogesha habari.

“Kwa bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa kupasha habari, basi umma umedanganywa,” alisema Kinana.

Kwa mujibu wa habari hiyo, sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali liliibuliwa kwa mara ya kwanza na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, katika Bunge lililopita la bajeti.

Ilidaiwa kuwa, nyaraka hizo zilionyesha kuwa, kilichokuwa ndani ya makontena hayo ni plastiki zilizodurufishwa na baada ya ukaguzi kufanyika, iligundulika kuwa, kilichokuwemo ni pembe za ndovu.

Habari ya gazeti hilo hata hivyo, ilimnukuu ofisa mwandamizi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, akieleza wazi kuwa kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani, wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Source: Tanzania Daima

Thursday, November 15, 2012

CCM msitegemee polisi: JK

 
Na Julius Magodi na Habel Chidawali, Dodoma
RAIS Jakaya Kikwete juzi (Jumatatu) aliwaonya wanachama wa CCM akiwataka waache kubweteka kwa kuwategemea askari polisi katika masuala ya kisiasa, kwani kufanya hivyo watakuwa wanajidanganya.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM uliofanyika kwa siku tatu mfululizo katika Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema kitendo cha wanaCCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la Polisi hakipaswi kukubaliwa kwani kimepitwa na wakati.

“Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao…au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,”alisema Kikwete na kuongeza:

“Sasa mnataka wakisema Serikali ya CCM haijafanya kitu polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, polisi wakawakamate? Kama wakisema hatujafanya kitu ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine.”

Licha ya kwamba hakuwataja moja kwa moja, kauli za Rais Kikwete zilikuwa zikielekezwa kwa uogozi wa Chadema ambao kimsingi kinaonekana kuwaumiza vichwa CCM.

Huku akirudia mara kadhaa maneno hayo alisema, “Nataka mfahamu ndugu zangu kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli.”

Kikwete aliwatuhumu viongozi wa upinzani kwamba ni waongo na kwamba wakati mwingine wamekuwa wakizusha mambo ambayo hayapo, huku wakijifanya kuwa na ushahidi wa kimaandishi.

Alimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwamba kuna wakati aliwahi kuzusha kwamba yeye (Kikwete), na makada kadhaa wa chama hicho wakiwamo Rostam Aziz walikuwa jijini Mwanza usiku, wakati si kweli kwani siku waliyodai alikuwa Nachingwea mkoani Lindi kwenye mikutano ya kampeni za urais.

Katika mazingira hayo, aliwataka wanaCCM kila mahali kujibu hoja za wapinzani kwa kauli na vitendo na wasikubali kuburutwa kwani uongo ukiachwa kwa muda mrefu unageuka kuwa ni ukweli.

Aliwaeleza kuwa ukimya wao katika kujibu hoja za wapinzani ni sumu kwao na kwamba wenzao wameanza kuaminika zaidi yao licha ya kuwa CCM ndio wenye majibu yote.

“Mkijibu kwa hoja wanatulia, sio Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani,” alisisitiza Kikwete.

Mbali na hilo aliwaonya kuacha malumbano ya mara kwa mara akieleza kuwa hali hiyo inakibomoa chama.

Alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakitumia muda mwingi kukosoana wao kwa wao, huku wakitoa nafasi kwa adui zao.

Mwenyekiti huyo alisema hakuna mtu kutoka nje ya chama anayeweza kukidhoofisha CCM kwa hoja isipokuwa chama hicho kinaumizwa na wanachama wake ambao wamekuwa wakilumbana bila sababu.

Akizungumzia suala la wagombea urais aliwataka wanachama wenye nia kufuata taratibu zote za chama pamoja na kuvumiliana ili ifikapo Mei 2015, mkutano utafanya uamuzi wa nani anasimama kupeperusha bendera ya chama hicho.

“Kwa wale mnaotaka kugombea, andikeni hiyo tarehe tutakuja hapa kuteua, lakini msituvuruge lazima mfuate utaratibu. Utaratibu huo utatangazwa, maana mkianza kupita huko na huko ndiko tunakopata matatizo,” alisema Kikwete.

Kikwete juzi alichaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata asilimia 99.92 ya kura zilizopigwa, huku kura mbili zikimkataa. Kadhalika mkutano huo uliwachagua Dk Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania – Zanzibar) na Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara).


Source: Jamii Forum

Wednesday, November 14, 2012

Mzee Makamba Atikisa, Amuokoa JK na kura za Maruhani

 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) jana kimenusuru Rais Jakaya Kikwete kupigiwa kura za maruhani, baada ya kubadili taratibu za uchaguzi, huku Katibu Mkuu wake wa zamani, Yusuph Makamba akiwapiga vijembe waliokuwa wamepanga mbinu hizo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa CCM, Spika wa Bunge, Anne Makinda, muda mfupi kabla wajumbe hawajaanza kupiga kura alitangaza utaratibu mpya kwamba kila mkoa utapiga kura katika sanduku lake.

“Kila mkoa utakuwa na sanduku lake la kupigia kura,” alisema Makinda na bila kufafanua, hali iliyowafanya baadhi ya wajumbe kushangaa uratatibu huo kwani kwa kawaida chaguzi za kumpata mwenyekiti na makamu wake hufanyika kwa wajumbe kupiga kura kwa ujumla, bila kufuata utaratibu wa mikoa.

Uamuzi huo ulikuja wakati kukiwa na taarifa kwamba baadhi ya wajumbe, walikuwa wamepanga kumpigia kura za maruhani, mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Dalili kuwa CCM kiligundua njama za hujuma hiyo, zilionekana mapema wakati Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba alipokuwa akimwombea kura Rais Kikwete.

Makamba na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai waliteuliwa na NEC ya CCM kumwombea kura Rais Kikwete kwa wajumbe wa mkutano huo.

Makamba aliwataka wajumbe wote kumpigia kura za ndiyo Rais Kikwete kwani wakipiga kura za maruhani wanataka mwenyekiti awe nani.

“Mpigie kura za ndiyo mwenyekiti wetu Kikwete, wale ambao mnataka kupiga kura za maruhani mnataka mwenyekiti awe nani?” alihoji Makamba, huku wajumbe wakimshagilia. Viongozi waliotarajiwa kuchaguliwa ni Mwenyekiti wa CCM na makamu wake wawili kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Waliopendekezwa na Halmashauri Kuu kuwania nafasi hizo ni Rais Kikwete kwa nafasi ya mwenyekiti, wakati Philip Mangula na Dk Ali Mohamed Shein walipendekezwa kwa nafasi za umakamu wa Bara na Visiwani sawia. Hadi tunakwenda mitamboni, matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa bado yanasubiriwa.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa CCM, katika uchaguzi huu kuziba mwanya wa kufanyika hujuma, baada ya Jumapili kubadilisha ghafla ratiba yake ya uchaguzi na kuanza na uchaguzi wa wajumbe wa Nec, badala ya uchaguzi huo kufanyika jana.

Hali hiyo iliwafanya wagombea na wapambe wao kushindwa kupata muda mrefu wa kufanya kampeni ikiwamo kutoa rushwa.

Makamba atikisaAkitumia aya zilizopo katika vitabu vitakatibu vya Biblia na Koran, Makamba aliwambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Rais Kikwete ana wito wa Mungu.

“Tembo hashindwi kubeba mikonga yake miwili, sasa wanaosema kuwa tupige kura za maruhani wanataka awe nani, nasema washindwe kabisa kwa jina la Yesu,” alisema Makamba huku akishangiliwa kwa nguvu na wajumbe wa mkutano na baadhi yao waliinuka kwenda kumtuza fedha.

Wakati anatuzwa alikatisha hotuba yake kwa muda, hali ambayo iliwafanya wajumbe kulipuka kwa kicheko akiwamo Rais Kikwete, huku yeye mwenyewe akisema, “Ninakula sehemu yangu kama watu wa dini wanavyokula sehemu yao.”

Mbali na hilo, aliwakumbusha machungu baadhi ya wanaCCM waliogombea nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) kwa kusema wako mbali na watu na ndiyo baadhi yao waliadhibiwa kwa kunyimwa kura.

Makamba alisema kuwa Rais Kikwete yupo karibu na watu na kwamba muda wote amekuwa akitekeleza Ilani ya chama hicho, hivyo apewe nafasi nyingine ya kukiongoza chama hicho.

“Wengine wanapiga kelele kuwa tupunguze kura za mwenyekiti, lakini wanasahau kuwa wao wana kazi moja, lakini kazi hizo zinawashinda, sasa kelele ya nini ndugu zangu, mpeni Jakaya mtu wa watu,” alisema.

Alisema CCM imesajili wachezaji wazuri ambao ni watendaji waliopatikana katika chaguzi mbalimbali za chama hicho na kwamba sasa wanatafuta kocha wa timu ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Makamba aliwasuta baadhi ya viongozi wa mikoa akisema kama asingekuwa Rais Kikwete kuwakumbuka hivi sasa hawangepata uongozi, hivyo wanapaswa kuonyesha shukrani kwa kuisaidia CCM kutekeleza Ilani yake.

Aliongeza kuwa wako watu ambao wamekuwa wakijitafutia umaarufu mkubwa ikiwamo kutaka uongozi wa nafasi ya urais, lakini hawajipimi kama wanakubalika au la.

Alisema watu wana namna hiyo wanaweza kufika mahali wakajikuta wanapigiwa kura na watu wachache sana ikiwamo kura zao na wake zao kutokana na kuamua kufanya mambo bila ya kufanya tathmni.

Makamba alisema kiongozi ili upendwe na wananchi lazima ufanye kazi nzuri, kama aliyoifanya Rais Kikwete katika uongozi wake katika CCM.

Akiwa ameliteka jukwaa la wajumbe huku akishangiliwa kwa nguvu huku akiendelea kutuzwa, Makamba aliwatolea mfano baadhi ya wenyeviti na kueleza namna wengine walivyolia wakati wakitafuta nafasi hizo.

“Mfano ndugu yangu Kaborou (Walid, Mwenyekiti wa CCM) kule Kigoma ulikuwa ukinitukana, lakini leo upo hapa, Shekifu (Henry, Mwenyekiti Mkoa wa Tanga) kule Tanga ulihangaika sana, Madabida (Ramadhan, Mwenyekiti wa Mkoa Dar es Salaam) ulikuwa ukihaha kweli, lakini wewe Msukuma Mgeja, (Hamis, Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga) ulilia machozi kabisa, kwa nini leo mwenzenu anapotafuta nafasi hiyo mnakuwa na nongwa,” alisema.

Hata hivyo, hakufafanua jinsi viongozi hao wanavyohusika katika mchakato wa uchaguzi huo.

Kabla ya kuingia CCM, Kaborou alikuwa Mbunge wa Chadema wa Kigoma Mjini, huku Mgeja, Shekifu na Madabida walikabiliwa na upinzani mkubwa wakati wa uchaguzi wa nafasi zao.

Mstaafu huyo alitumia nafasi hiyo kuwatupia kombora baadhi ya wasaidizi wa Rais Kikwete kuwa wamelewa madaraka kiasi kwamba hata wakipigiwa simu huwa hawapokei na badala yake huwapa wake zao simu hizo, tofauti na Kikwete ambaye kupokea simu wakati wowote.

Hata hivyo, Makamba mbali ya kumnadi Kikwete alitumia jukwaa hilo kutoa dukuduku lake kuwa kilichomgarimu wakati akiwa ndani ya chama hicho ni kutokana na kusema ukweli.

Alisema kuwa amekuwa akisimamia katika ukweli na haki wakati wote jambo ambalo halikukubalika na watu wengi ndani ya chama.


Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

Tuesday, November 13, 2012

Urine Generator

 
Three of the four inventors of the urine-powered generator (Eric Hersman)Four African girls have created a generator that produces electricity for six hours using a single liter of urine as fuel.
The generator was unveiled at last week's Maker Faire in Lagos, Nigeria, by the four teens Duro-Aina Adebola, Akindele Abiola, and Faleke Oluwatoyin, all age 14, and Bello Eniola, 15.
So how exactly does the urine-powered generator work?
  • Urine is put into an electrolytic cell, which separates out the hydrogen.
  • The hydrogen goes into a water filter for purification, which then gets pushed into the gas cylinder.
  • The gas cylinder pushes hydrogen into a cylinder of liquid borax, which is used to remove the moisture from the hydrogen gas.
  • This purified hydrogen gas is pushed into the generator.

And as for delivering the fuel itself? Well, we'll leave that up to the consumer.
The Maker Faire is a popular event across the African continent, drawing thousands of participants who travel to Lagos to show their inventions and other practical creations.
The Maker Faire is intended to highlight creations "that solve immediate challenges and problems, and then works to support and propagate them. Put another way, this isn't just a bunch of rich people talking about how their apps are going to change the world."
Source: Jamii Forum

Matokeo ya Nec yateka Dodoma; WASSIRA ATAJWA UKATIBU MKUU

 
WASSIRA ATAJWA UKATIBU MKUU, WALIOSHINDA WATAMBIANA, WALIOSHINDWA WATOWEKA
WAKATI matokeo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), yakiwa yamevuja baadhi ya wapambe wa wagombea walioshinda wameanza kusherehekea, huku wengine wakitambiana.

Hata hivyo, matokeo hayo yamekuwa machungu kwa baadhi ya vigogo walioanguka wakiwamo mawaziri, wabunge na watu maarufu.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuunda sekretarieti mpya baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar utakaofanyika leo.

Kwa upande wa Zanzibar, matokeo hayo yanaonyesha kuwa walioshinda ni pamoja na Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto.

Watu maarufu walioangukia pua katika uchaguzi huo ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdallah Juma Sadallah, mtoto wa Rais Mstaafu, Abdallah Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa Salehe na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalaam Issa Khatib.
Walioshinda BaraMajina ya wajumbe wa Nec walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (1,967), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824).

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mukangara (984).

Wakati walioshinda Bara na wapambe wao wakitambiana, majina makubwa yaliyoanguka katika uchaguzi huo ni pamoja ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama, Richard Hiza Tambwe na Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri.

Wassira atajwa kumrithi Mkama
Habari zilizopatikana jana mjini hapa zinaeleza kuwa Wassira, anatajwa kuwa anaweza kuikwaa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho.

Wengine wanaotajwa kuwa wanaweza kupata nafasi hiyo ya Katibu Mkuu ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na Waziri Lukuvi.

Makundi yatambiana
Tambo na kejeli za wapambe, jana zilitawala katika viwanja vya Ukumbi wa Kizota unakofanyika Mkutano Mkuu wa CCM, baada ya baadhi ya wajumbe kuanza kusherehekea kutokana na kupata matokeo.

Nje ya ukumbi huo, tangu asubuhi wapambe wa wagombea hao walionekana wakiwa wamekaa katika makundi huku wakinunuliana vinywaji.

Ingawa matokeo yalitarajiwa kutangazwa leo, lakini takriban wajumbe wote wa mkutano huo walionekana kuyapata hali ambayo iliwafanya walioshinda kupongezwa wakati wakiingia katika ukumbi wa mikutano.

Mwananchi lilimshuhudia, Waziri Mathayo akipongezwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo nje ya ukumbi wa mkutano asubuhi.

Pamoja na kupongezwa na wajumbe wa mkutano huo hata washindi wa uchaguzi huo nao walipokutana walipongezana.

Mwananchi lilimshuhudia, Shigela akimpongeza Waziri Wassira na baadaye walikumbatiana na kupongezana na Nchemba. Baadaye baadhi ya wajumbe walimbeba Shigela juu juu wakimpa pongezi.

Wakati Shigela akibebwa, baadhi ya wajumbe walimfuata Wassira na kumpongeza kwa kumshika mikono na wengine kumkumbatia huku yeye wenyewe akitamba kuwa ni mwarobani wa Chadema.

Waziri Membe akiwa ndani ya ukumbi wa mkutano, baadhi ya wajumbe wanaomuunga mkono walimfuata na kumzunguka huku wengine wakimkumbatia.
Walioanguka watowekaWakati walioshinda wakionekana kufurahi na kupongezwa, hali ilikuwa tofauti kwa wagombea walioshindwa, kwani baada ya kupata matokeo hayo wengi walitoweka katika eneo la ukumbi huo.
Kamati ya Uchaguzi yalala ukumbini

Kamati iliyokuwa ikisimamia uchaguzi huo jana ililala katika ukumbi wa kuhesabia kura kutokana na kazi hiyo kumalizika usiku wa manane, huku baadhi ya watu waliokuwa wakifanya kazi hiyo kunyang’anywa simu zao ili matokeo yasivuje.

Watu hao waliondoka katika ukumbi wa kuhesabia kura uliopo katika Ukumbi wa Kizota saa 12:00 asubuhi.

Source: Jamii Forum

Monday, November 12, 2012

Mnyika: Spika amefunika kombe


AKATA RUFAA, ADAI ADHABU ZILIZOTOLEWA NDOGO
 
MBUNGE wa Ubungo na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, ameamua kulivalia njuga suala la tuhuma za wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa, akisema kuwa uamuzi wa Spika Anne Makinda umeacha makando kando mengi, ikiwemo ukiukwaji wa katiba ya nchi, hivyo anajipanga kuukatia rufaa.

Alisema kuwa uamuzi wa Spika Makinda uliotangazwa juzi bungeni, umefanyika kwa namna ya ‘funika kombe’, hivyo rufaa yake inalenga kutaka taarifa kamili ya Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iwasilishwe kwa ukamilifu wake kwenye kamati husika ya kudumu ya Bunge na kujadiliwa bungeni ili ‘mbivu na mbovu’ katika usimamizi na uendeshaji wa sekta ya nishati zijulikane, kisha uchunguzi wa kina ukihusisha vyombo vingine nje ya Bunge, ufanyike.

Alifafanua kwa kurejea hotuba yake aliyosoma bungeni kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni wakati wa Bunge la bajeti lililopita, akisema kuwa alitoa angalizo tangu awali kuwa ili ukweli ujulikane ilipaswa kuundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza masuala yote ya ukiukwaji wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ufisadi katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta kwa ajili ya mitambo ya umeme.

Alisema ni muhimu kufanyika kwa uchunguzi wa namna hiyo, ukihusisha pia Mkaguzi Mkuu kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi kwa malipo yaliyofanywa na makampuni ya BP (Sasa Puma Energy), Oryx na Camel Oil ili kubaini iwapo kuna vigogo zaidi wa serikali waliojinufaisha kwa kisingizio cha dharura ya umeme, kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 27(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, siku moja tu baada ya Spika Makinda kutoa uamuzi wake bungeni juu ya tuhuma za wabunge kujihusisha na rushwa, Mnyika alisema kuwa atakata rufaa kwa kuwa kiwango cha ‘adhabu’ kilichotolewa na Spika hakilingani na ‘makosa’ ambayo yameelezwa kuwa na uzito wenye kuathiri “kwa kiasi kikubwa hadhi ya Bunge kama taasisi na heshima ya wabunge waliohusishwa”.

Akitolea mfano, Mnyika alisema kuwa ikiwa ni kweli Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kuwa amefanya makosa ya kuvunja haki za Bunge kwa kuzusha tuhuma za uongo ili kujihami dhidi ya wabunge waliokuwa wanahoji utendaji wake, basi adhabu aliyopewa hailingani na ukubwa wa makosa anayodaiwa kufanya.

“Kwa kosa hilo ikiwa maelezo ya Spika kuhusu matokeo ya uchunguzi wa kamati ni sahihi, anapaswa kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge na kupewa adhabu ya zaidi ya onyo ikiwemo hata faini au kifungo au walau kutakiwa kuwajibika.

“Kadhalika Spika ameeleza kuwa mbinu aliyotumia (Maswi) ni pamoja na kutaka kuwalipa fedha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini shilingi milioni mbili kwa kila mjumbe, madai haya ni ya jaribio la kufanya ufisadi wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyokuwa kwenye kashfa ya Katibu Mkuu aliyemtangulia, David Jairo, hivyo Spika alipaswa kupendekeza kwa mamlaka ya uteuzi wake kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria.

“Baada ya uamuzi wa Spika kuhusu tuhuma kwamba baadhi wa wabunge na wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini walijihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza kazi zao za kibunge, nimeulizwa na baadhi ya wanahabari na wananchi kwa simu na kwenye mitandao ya kijamii sababu za kusimama bungeni tarehe 9 Novemba 2012 mara baada ya Spika kutoa uamuzi huo na kutaka kuomba muongozo.

“Nakusudia kukata rufaa kwa sababu uamuzi wake una maudhui kadhaa yasiyozingatia katiba ya nchi, sheria mbalimbali za nchi, kanuni za kudumu za Bunge, maamuzi ya awali ya maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa bunge letu,” alisema Mnyika na kuongeza;

“Kwa kuzingatia kuwa rufaa huchukua muda kusikilizwa, nilitaka niombe muongozo wake kwa kuwa katika uamuzi wake hakueleza hatma ya Kamati ya Nishati na Madini, hivyo Spika anapaswa kuueleza umma iwapo kamati hiyo inarejeshwa au inaundwa kamati nyingine au kuelekeza kamati nyingine ya kudumu ya Bunge inayopaswa kuisimamia serikali wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na matatizo mengi kwenye sekta za nishati na madini yenye athari kwa maisha ya wananchi.”

Aliongeza kusema kuwa, kwa kuwa katika uamuzi wake Spika Makinda alieleza kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake Maswi wametoa maelezo yasiyokuwa kweli kwa nyakati mbalimbali, uwepo wa Kamati ya Bunge kwa ajili ya kuisimamia wizara hiyo kwa niaba ya Bunge ni suala linalohitaji uamuzi wa haraka kutokana na hali ya nchi juu ya sekta ya nishati kuwa tete bila usimamizi wa kibunge.

Aidha, katika taarifa yake hiyo, Mnyika ameonekana kushangazwa na kitendo cha Spika Makinda kutoa onyo kali kwa Katibu Mkuu na wabunge kadhaa, lakini hakutoa onyo kwa Waziri wa Nishati na Madini wala hakueleza chochote iwapo alipokea ushauri kutoka kwa Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu ukiukwaji wa kanuni uliofanywa bungeni wakati wa kadhia nzima.

Akikumbushia hadidu rejea moja tu iliyopewa Kamati Ndogo iliyofanya uchunguzi ya “Kuchunguza na kumshauri Spika iwapo tuhuma kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli au hapana”, hivyo, kwa mujibu wake, baada ya uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake Spika alipaswa kuanzisha mchakato wa adhabu, kama kulibainika kuwepo kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni.

Alisema kuwa uamuzi wa Spika ‘kufunika kombe’ hauna tofauti na maamuzi yaliyotangulia ambayo yamesababisha mpaka sasa serikali haijawasilisha bungeni ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya sakata la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Jairo, kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge.

Aliongeza kuwa, leo ataeleza masuala ya ziada atakayoyakatia rufaa na kauli yake kuhusu maelezo na uamuzi wa Spika juu ya Waziri na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini.

Chanzo: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=42379

Thursday, November 8, 2012

Watu 4 wafariki, 48 majeruhi katika ajali mkoani Lindi.


 Picha na Habari na Abdulaziz video,LindiABIRIA wapatao wanne wamekufa papo hapo na wengine 48 wamekimbizwa katika hospitali ya Kinyonga,wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,kufuatia basi walilokuwa wakisafiria kutoka jiji Dar es salaam kwenda wilaya yaLiwale,kuacha njia na kupinduka.

Habari kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa,Joseph Mfungara, zinaeleza ajali hiyo imetokeakatika mteremko mkali wa Nangurukuru wilayani Kilwa

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa basi hilo aina ya Mitsubishi lenye namba za usajili T981 AFL lililokuwa likiendeshwa na Shabani Kiparapara wa Jijini Dar es salaam lilipata ajali hiyo eneo la mlima uitwao Kipokonyo.

“Hili basi lilipofika eneo hilo la mlima,lilionekana likienda mwendo kasi na hatimaye kuacha barabara na kuelekea Porini na kupinduka”Walisema mashuhuda hao waliojitambulisha Issa Abdallah na Juma Selemani.

Walisema wananchi waliojitokeza kutoa msaada kwa abiria hao, waliweza kushuhudia watu wanne wakipoteza maisha papo hapo,huku wengine hali zao zikiwa katika hali mbaya.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Joseph Mfungamara amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza basi hilo lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda wilaya ya Liwale.

Mfungamara amewataja marehemu hao kuwa ni,Flora Francis Lamumba (32) mwalimu wa Shule ya msingi,Dorah Francis (35) muhudumu wa Bar,Halima Manicha (60) wote ni wakazi wilaya ya Liwale na Christina Samweli Kika,muhudumu wa Idara ya Afya mkoani Arusha.

Amesema katika ajali hiyo abiria wapatao 48 wamelazwa Hospitali ya wilaya ya Kilwa, Kinyonga,kutokana na kuumia maeneo mbalimbali ya miili yao.

Kaimu kamanda huyo wa Polisi mkoani Lindi, amesema bado chanzo cha ajali hiyo,haijaweza kufahamika mara moja,na kuongeza dereva wa basi hilo Shabani Kiparapara ametoroka mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo,na kwamba anatafutwa ili afikishwe mahakamani kwa hatua zingine za kisheria.
 
Source: Francis Godwin Blog

Tuesday, November 6, 2012

Polisi wanasa ‘Radio call’ ya Barlow katika shimo la majitaka


Sheilla Sezzy, Mwanza

POLISI mkoani hapa wamefanikiwa kuipata simu ya upepo ‘radio call’ iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow ambayo ilichukuliwa baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi usiku wa manane eneo la Minazi Mitatu Kitangiri.

Mbali na simu hiyo, jeshi hilo pia limefanikiwa kupata ufunguo wa gari la marehemu Barlow ambaye aliuawa wakati akimsindikiza mwanamke mmoja aliyeitwa Doroth Moses walipokuwa wakitoka kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lili Matola, alisema jana kwamba vitu hivyo vilipatikana vikiwa vimefichwa katika shimo la majitaka katika nyumba moja iliyopo maeneo ya Nyashanya.

Pia jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine wawili wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo na Kamanda Matola alisema wataunganishwa kizimbani na wengine watano Novemba 15, mwaka huu.

Alisema watuhumiwa hao wawili (majina tunayahifadhi kwa sasa), mmoja wao akiwa ni ndugu wa mtuhumiwa namba moja katika mauaji hayo, ndio waliotaja sehemu vilikokuwa vimefichwa vitu hivyo baada ya kuhojiwa.

“Baada ya kuonyesha vilipokuwa vimefichwa, ilibidi kumtaarifu mwenye nyumba ambaye alitoa idhini ya kubomolewa kwa shimo hilo la majitaka na mmoja wa watuhumiwa aliingia na kutoa ‘radio call’ pamoja na funguo za gari la marehemu,” alisema Kamanda Matola.

Alisema kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa namba moja alitoa maelekezo ya wapi pa kuficha vifaa hivyo. Kabla ya kuficha simu hiyo, waliitenganisha na betri yake.

Kamanda Matola alisema katika msako waliofanya nyumbani kwa watuhumiwa hao, pia walikuta sare za moja ya kampuni ya ulinzi pamoja na magwanda ya mgambo.

Alisema kuwa vitu vingine vilivyokamatwa ni kofia mbili, moja ikiwa ya polisi na nyingine ya kampuni ya ulinzi pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia uhalifu.

Alisema mmoja wa watuhumiwa aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, alichokitumikia kuanzia mwaka 2006 baada ya kukutwa na makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha. Hata hivyo, alisema aliachiwa huru mwaka 2010 baada ya kukata rufani Mahakama Kuu na kuachiwa huru.

Alisema katika mahojiano na polisi, mtuhumiwa huyo alisema alishawishiwa na kaka yake kufanya kazi hiyo ya ujambazi.

Mbali na watu hao, Matola alisema polisi pia inamshikilia mtu mmoja (jina tunalihifadhi) mkazi wa Nyakabungo akituhumiwa kufadhili kundi hilo la majambazi.
 
Source: Mwananchi

Monday, November 5, 2012

GMO ni sumu.....itaongeza umaskini: Mdee


Mbunge wa jimbo la kawe Mh Halima Mdee amesema Genetic Modification ni sumu na haina tija kwa wakulima wa Tanzania, zaidi itaongeza umaskini. Mh Mdee ameyasema hayo wakati akichangia muswada wa sheria ya kulinda haki ya ugunduzi wa aina mpya ya mbegu leo hii jioni bungeni mjini Dodoma.

Mh Mdee amesema sheria itakayoundwa kwa kiasi kikubwa haitawatambua wakulima wa hapa nchini kama wazalishaji wa mbegu za asili za mazao mbali mbali. Akitolea mfano zao la pamba, amesema kuwa serikali imeingia mkataba na kampuni ya kigeni kutoka Zimbabwe inayofanya kazi ya kuzalisha mbegu mpya za pamba.

" Kinachofanyika kampuni hiyo hununua mbegu hizo kwa wakulima wetu wa hapa nchini kwa bei ya chini, na kuzifanyia mabadiliko kidogo na kuja kuziuza tena kwa wakulima kwa bei ya juu" alisema Mh Mdee. Kwa kitendo hicho ni kwamba kampuni hiyo inapata hakimiliki kama wazalishaji wa mbegu mpya ilhali zimenunuliwa kwa wakulima wa hapa hapa.

Mh Mdee aliendelea kuihoji serikali kuhusu kuwa na ushirika na kampuni ya MONSATO ambayo inatajwa kuwa imefunguliwa kesi nyingi na baadhi ya nchi kwa utendaji wake mbovu wa kazi. Kampuni ya MONSATO inatajwa kuwa ni mdau namba moja katika kuisadia serikali katika kutekeleza programu ya kilimo kwanza

Sunday, November 4, 2012

Familia ya Mwangosi kuishtaki Serikali

Itika Mwangosi-mjane
Familia ya aliyekuwa Mwandishi wa kituo cha televisheni cha chaneli ten, Marehemu Daudi Mwangosi, imepanga kuishtaki Serikali na jeshi la polisi kufuatia mauaji hayo ya kinyama. Mauaji hayo ya mwandishi huyo wa habari yameweka rekodi ya mwandishi kuuliwa mbele ya polisi katika taifa hili la Tanzania.
 
Familia inatumai kwamba hatua za kisheria zitaisaidia kutoa ukweli wa wazi kabisa na hivyo kumfikisha muuaji katika haki. Mjane wa Daudi Mwangosi, Ms Itika Mwangosi amesikitishwa na taarifa ya tume ya kuchunguza mauaji ya mume wake iliyoundwa na Waziri wa mambo ya Ndani Dr. Emannuel Nchimbi. Itika mwangosi amesema srekali haina nia ya thabiti ya kuelezea kile kilichotokea na hana imani na jinsi kesi iliyoko mahakamani jinsi inavyoendeshwa.
 
Itika Mwangosi ameshangazwa na hatua ya tume hiyo ya kutotaja muuaji wa mume wake na kuona ni kama vile imepoteza fedha za walipa kodi katika kuchunguza tukio hilo. "Tunajua kuna baadhi ya watu wanataka kuficha ukweli juu ya suala hili na sisi tutaipeleka serikali mahakamani ili haki itendeke" alisema Mjane wa Mwangosi. Hakuna kitu kitakachonipa faraja kama muuaji wa mume wangu kuhukumiwa kwa kile alichotenda" alimalizia Ms Itika Mwangosi.....
 
Kwa taarifa zaidi fuatilia link hii....The Citzens
 
 

Friday, November 2, 2012

Wabunge vinara wa rushwa hatarini;BUNGE LAJIANDAA KUWACHUKULIA HATUA KALI

 
Julius Magodi, Dodoma
BUNGE limeandaa kanuni za maadili ili kuwadhibiti wabunge ambao wanatumia mianya ya kanuni zilizopo kufanya makosa mbalimbali ikiwamo kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Habari zilizopatikana mjini Dodoma na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel zinaeleza kuwa hatua hiyo ya Bunge inatokana na kuongezeka kwa wabunge kutuhumiwa kwa makosa mbalimbali wanayoyafanya wakiwa nje na ndani ya Bunge.

Joel alisema masharti hayo mpaka sasa yapo katika hatua ya kuchapwa na kwamba muda siyo mrefu maadili hayo ya kanuni yatatoka.

“Tupo katika hatua ya kuichapa code of conduct (Kanuni za maadili) hiyo na kwamba muda si mrefu itatoka na kuanza kutumika.”

Alisema wamegundua kuwa baadhi ya wabunge wanatumia kanuni za Bunge zilizopo kuzikwepa na kufanya mambo yasiyofaa ambayo yanashusha hadhi ya Bunge, hivyo masharti hayo mapya yatawabana zaidi.

Kauli hiyo ya Joel inakuja siku mbili baada ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi uliomalizika jana mjini hapa.

Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, alikamatwa na makada wengine wa chama hicho saa 4:30 usiku katika kituo cha mafuta akidaiwa kujaribu kutoa rushwa ya Sh100,000 kwa wajumbe wa mkutano huo wa wazazi.

Hata hivyo, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Eunice Mmari juzi alikaririwa akisema vijana wake walimtia nguvuni Zungu katika Hoteli ya Golden Crown akiwa na wapambe wake wakiendelea kugawa fedha kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wazazi.

Mbunge mwingine ambaye ana kesi mahakamani kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa ni Omar Badwel wa Bahi.

Badwel anatuhumiwa kuomba rushwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani, Zipora Liana.

Hatima ya Zungu, Badwel
Kuhusu kukamatwa kwa Zungu, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Shughuli za Bunge, alisema kuwa Bunge halitamchukulia hatua yoyote na badala yake linaviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake.

Joel alisema suala la Zungu bado ni tuhuma hivyo, ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala hadi hapo kama itathibitika kuwa ametenda kosa mahakamani.

Alisema suala lake ni sawa na la Mbunge Badwel ambaye ana kesi mahakamani ya kutuhumiwa kujihusisha na rushwa, lakini bado anaendelea kuwa mbunge.

Hatua hii ya Bunge pia inakuja wakati bado ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na rushwa wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu, ikisubiriwa kusomwa bungeni.

Agosti 2, mwaka huu Spika Makinda aliunda kamati ndogo ya kuchunguza tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya wabunge ambao walidaiwa kwamba walihongwa ili kuikwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kuundwa kwa kamati hiyo, kulitanguliwa na tukio la kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Julai 28, mwaka huu pia kutokana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, kujihusisha na rushwa na wengine kutumia nafasi zao kujinufaisha kwa kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo lipo chini ya kamati hiyo.

Mabilioni ya Uswisi
Katika hatua nyingine, Serikali imeanza kufanya uchunguzi wa kina ili kujua ukweli na kuwachukulia hatua watu wote walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi.

Waziri Mkuu alisema bungeni jana kuwa, mara baada ya uchunguzi huo kukamilika Serikali itatoa taarifa kuhusu uchunguzi huo.

Pinda alikuwa akijibu swali aliloulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu jana asubuhi.

“Jambo hili kwa uzito wake, tumeanza kulifanyia uchunguzi ili kujua ukweli wake na hatua stahiki za kuchukua, tukimaliza tutatoa kauli kama ilivyo kawaida yetu, “ alisema.

Mbowe katika swali lake alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kuhusu taarifa za kuwapo kwa mabilioni ya fedha katika akaunti za benki mbalimbali nchini Uswisi ambazo zimewekwa na baadhi ya vigogo serikalini na viongozi wastaafu.

Katika Bunge la Bajeti lililopita, Kambi ya Upinzani ililiibua suala hilo wakati wa hotuba yao ya Bajeti wakieleza kuwa kuna jumla ya Sh360 bilioni zilizofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa baadhi ya fedha hizo
zimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni za mafuta na gesi zilizopo nchini.

Jumanne wiki hii, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alipokuwa akichangia azimio la kuridhia marekebisho ya pili ya Mkataba wa Ushirikiano kati ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP), alisema Serikali iutumie ushirikiano huo kurejeshwa mabilioni yaliyofichwa nchini Uswisi.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara Rombo, mkoani Kilimanjaro Oktoba 26 mwaka huu, alimlipua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akidai kuwa bosi huyo ameandika barua Uswisi, akieleza kwamba Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki za nchini hiyo.

Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha akisema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.


Source: Jamii forum