Pages

Saturday, December 29, 2012

Thursday, December 27, 2012

Taswira Maandamano na mkutano mkoani Mtwara kuhusu Gesi kutokusafirishwa

Kuna mkutano Mkubwa unaendelea hivi sasa katika uwanja wa Mashujaa. Wananchi wanakutana kujadili rasilimali ya Gesi, ambayo hawataki isafirishwe kwenda kuzalisha umeme eneo jingine la Nchi hii. Viongozi wa dini, wanachama wa vyama mbali mbali pia wapo hapa katika uwanja huu kujadili suala hilo.....na kuna kauli mbiu nzito inayosema "GESI KWANZA VYAMA BAADAE

Ujumbe katika bango
Moja ya jumbe ilisomeka hivi
Umati wa watu katika uwanja wa mashujaa
haya tena
maandamano

 

Sunday, December 23, 2012

Taswira siku ya Mazishi ya Marehemu Mary Chunga

Gari lililobeba mwili wa marehemu likiwasili nyumbani kwa marehemu
Sanduku lililobeba mwili likiingizwa nyumbani kwa marehemu
Mwili ukipelekwa ili uweze kuombewa ...padri akijiandaa
Sanduku lililobeba mwili wa marehemu
Padri akihubiri sambamba na kuuombea mwili wa marehemu....
Baadhi ya watoto wa marehemu.....
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
Msafara ukielekea mazishini
Mwili wa marehemu ukihifadhiwa kwenye nyumba ya milele....
Ndugu wa marehemu wakiweka mashada kwenye kaburi la marehemu
Mishumaa pamoja na mashada juu ya kaburi
"Bwana alitoa.....na bwana ametwaa...jina lake lihimidiwe"

AMEEEEEEEEEEN
 

Tuesday, December 18, 2012

lulu kama Ukiwaona Ditopile Mzuzuri...akwepa kunyongwa

 
 
Hatimaye Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Eliezer Feleshi amembadilishia shtaka Msanii Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu kutoka kuua kwa kukusudia hadi kuua bila ya kukusudia. Lulu anashtakiwa kwa kumuua Msanii mwenzake Marehemu Stephen Kanumba.

Jambo kama hilo lilifanywa pia katika kesi ya Marehemu Kapteni Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyeshtakiwa kwa kumuua dereva wa daladala kwa kumpiga risasi.

Hii ndio kusema,sasa mlango wa dhamana kwa Lulu uko wazi kwakuwa kosa analoshtakiwa  si kati ya yale yasiyo na dhamana. Sinema hii ndio inaelekea patamu, kumbuka kuwa Marehemu Ditopile aliachiwa Huru.

Monday, December 17, 2012

Lissu amtega JK

 
Julius Magodi, Dodoma
SUALA la kuwapo kwa majaji wasiokuwa na sifa nchini limeingia katika sura mpya baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete kama atashindwa kuwaondoa kazini ifikapo Kikao cha Bunge lijalo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.

Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao wasiokuwa na sifa.

Lissu alisema atawasilisha hoja yake hiyo kwa kutumia Kanuni ya Bunge sehemu ya 11, Ibara ya 121, 122, 123, 124, 125 na 126 na pia kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 146 A.

Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumwondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Lissu alisema atakusanya saini za wabunge kuunga mkono hoja yake ambayo ni asilimia 20 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Wabunge wote kikatiba ni 357.

Julai 13, mwaka huu wakati akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Katiba na Sheria bungeni, Lissu alisema uteuzi wa majaji umegubikwa na ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Alisema baadhi ya majaji walioteuliwa hawana sifa, uwezo na kwamba hawakufaa kufanya kazi hiyo.
Kauli hiyo ilisababisha Bunge kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi kumhoji ili athibitishe kauli yake.

Alisema wakati akihojiwa na kamati hiyo, pamoja na nyaraka nyingine, aliwasilisha nakala ya ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa mwaka 2008 na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuchunguza uteuzi wa majaji nchini.

Alisema ripoti ya kikosi kazi hicho kilibaini kuwapo majaji ambao hawana sifa ya kufanya kazi hiyo, lakini Rais Kikwete ameshindwa kuwaondoa kazini.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alisema hali ya mahakama ni mbaya, kwani kuna majaji wawili ambao waliwahi kukamatwa kwa rushwa wakiwa mawakili, lakini wakateuliwa kufanya kazi hiyo.

Alisema baadhi ya majaji hawana uwezo hata wa kuandika hukumu kutokana na kutojua vyema lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo inayotumika katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.

Mbunge huyo alimtaja Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ambaye ameteuliwa akisema hana hata shahada ya kwanza ya sheria kinyume cha taratibu.

“Kwa mfano, yupo Jaji wa Mahakama ya Rufani (jina tunalo), ambaye hana hata shahada ya sheria anaweza vipi kuwa jaji?,” alihoji Lissu.

Alisema jaji huyo hivi sasa anasoma shahada ya sheria katika chuo kikuu kimoja hapa nchini.
Lissu alisema ili mtu aweze kuchaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu lazima awe na elimu ya shahada ya kwanza ya sheria, awe ametumikia miaka 10 mahakamani na anayechaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani lazima awe ametumikia miaka 15 mahakamani.

Mbali ya kueleza hayo, Lissu alisema kwamba alitoa pia katika kamati hiyo, ushahidi unaoonyesha kuwa kuna jaji mmoja wa Mahakama Kuu ambaye hawezi hata kuandika sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka... “Kama jaji hawezi kuandika hata sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka, tunaweza vipi kuwa na mahakama inayotenda haki?”

Alisema kuna jaji mwingine ambaye ameongezewa mkataba wa kufanya kazi mara ya tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Alisema kwa mujibu wa Tume ya Mahakama, hakuna jaji ambaye anaweza kufanya kazi kwa mkataba kwa vipindi vitatu.

Mbunge huyo alisema mbali ya madudu hayo katika sekta ya mahakama, hivi sasa kuna jaji maarufu ambaye ameghushi umri wa kuzaliwa ili aweze kuendelea kufanya kazi hiyo.

Alisema jaji huyo amezaliwa Septemba 4, 1949 lakini amebadilisha umri wake kuwa amezaliwa Septemba 4, 1952 ili aweze kufanya kazi hiyo hadi mwaka 2017.

Mbunge huyo alisema kazi hiyo ya kughushi umri wa jaji huyo imefanywa kwa kunyofoa nyaraka za kumbukumbu zake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alimtaka jaji huyo kuzirejesha mara moja nyaraka hizo vinginevyo katika Bunge lijalo atamtaja kwa jina hadharani.

Alipotakiwa kueleza kwa nini asimtaje sasa alisema akifanya hivyo anaweza kutingisha nchi.
Kama Lissu atachukua hatua hiyo, itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kumwajibisha kiongozi wa juu serikalini.

Mara ya kwanza alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe katika Bunge lililopita alipokusanya saini za wabunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitaka awajibishe baadhi ya mawaziri waliokuwa wametajwa kuhusika katika matumizi mabaya ya madaraka katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Hata hivyo, Rais Kikwete alifanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri hivyo kuzima hoja hiyo ya Zitto.

source: mwananchi 17.12.12 via Jamii forum

Wednesday, December 12, 2012

Mike Tyson Sasa ni Michelle! Abadili Jinsia

 
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mike "Iron" Tyson amesema anaendelea kujisikia vizuri baada ya operesheni ya kubadili jinsia yake kufanyika kwa mafanikio katika clinic ya Beverley Hills.
 
Bondia huyo mzaliwa wa Brooklyn, aliwahi kujulikana kama "mtu mbaya zaidi duniani" amewaambia waandishi wa habari kuwa amepata hedhi kwa mara ya kwanza na kwamba jambo hilo limetimiza ndoto yake, na sasa anapenda ajulikane kama Michelle Tyson.
 
"Baadhi ya watu wanaona ajabu kwa  mimi kuwa mwanamke" alisema Tyson ambaye aliwahi kuhukumiwa kwa kesi ya ubakaji. " katika kipindi chote cha upiganaji nilijulikana kama mpiganaji bora, na nilikuwa na ndoto ipo siku nitakuwa na matiti pamoja na uke" alibainisha Tyson.

Monday, December 10, 2012

Majambazi waipora Maiti ya mwanafunzi wa SUA

 
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mkoa Singida, akirekebisha mapambo ya jeneza lililokiwa na mwili wa marehemu Munchari Lyoba, mwanafunzi wa SUA , jeneza lililovunjwa na majambazi na maiti kupekuliwa yakitafuta fedha zaidi baada ya kupora wasindikizaji. (Picha na Gasper Andrew)

WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka mjini Morogoro kwenda mkoani Mara kisha kupora takriban Sh19.8 milioni walizokuwa nazo waombolezaji.
Katika tukio hilo la kusikitisha lililotokea juzi mkoani Singida, majambazi hao walivunja vioo vyote vya gari pamoja na jeneza lililokuwa na mwili wa Munchari Lyoba aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) cha Morogoro na kumpekua marehemu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida, mkuu wa msafara uliokuwa ukisafirisha maiti, Makaranga alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 7:30 usiku katika gari aina ya Land Cruiser mali ya SUA.
Akisimulia tukio hilo, Makaranga alisema kuwa lilitokea katika Barabara Kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya Mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans kuelekea mkoani Mara.
Alisema kuwa gari hilo pamoja na jeneza, lililobeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne lilipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa barabarani na kuwalazimisha kusimama ndipo wakavamiwa na kundi kubwa la vijana, ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.
“Walipofika walipiga kioo cha gari letu kwa mbele na kumparaza kwa panga usoni dereva wetu. Baada ya hapo walivunja vioo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu tulichokuwa nacho,” alisema Makaranga.
Makaranga alisema kuwa katika tukio hilo, aliporwa Sh2 milioni alizokabidhiwa azihifadhi kwa ajili ya kugharimia msafara huo, Sh8.8 milioni zilizochangwa na wanafunzi kama rambirambi kwa mwenzao na jumla ya Sh9 milioni ambazo wasindikizaji walikuwa nazo mifukoni mwao.
“Pia tuliporwa simu zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu,” alisema.
Makaranga aliyeeleza kuwa anafanya kazi za kiutawala SUA, aliwataja walioumizwa na majambazi hao kuwa ni pamoja na yeye, dereva wao na kiongozi wa wanafunzi, Idd Idd ambao walitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na kuruhusiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa amewasiliana na uongozi wa SUA ili watume gari lingine na kukarabati jeneza lililoharibiwa na majambazi hao.
Mlozi aliongeza kuwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Kamati ya Ulinzi na Usalama, watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa haraka iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
“Nimesikitishwa sana na tukio hili, inaelekea sasa binadamu tunaanza kutoka kwenye utu na kuhamia kwenye vitendo ambavyo binadamu wa Mwenyezi Mungu hawezi kuthubutu kuvifanya. Watu wanafikia hata kufungua jeneza na kuanza kulisachi,” alisema Mlozi akionyesha masikitiko.

Soma zaidi: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Thursday, December 6, 2012

Walimu wakimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi

 
WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.

Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
 
Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.
Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.
 
“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.

Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.
Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.

Mwalimu huyo alidai kuwa walimu.......Endelea (: http://www.mwananchi.co.tz/)

Saturday, December 1, 2012

"Serikali imezidi kudhihirisha udhaifu"-Mnyika

 
Na: Elias Msuya
MBUNGE wa Ubungo (Chadema), John Mnyika amesema ukiukwaji wa sheria wa matumizi ya Sh96 bilioni katika ununuzi wa mafuta mazito ya uendeshaji wa mitambo ya kufua umeme wa dharura ni matokeo ya Serikali kuwa dhaifu.

Amesema udhaifu huo unatokana na Serikali kushindwa kuzingatia utawala wa sheria, huku akilishukia Bunge kwamba nalo limefanya uzembe katika kusimamia utekelezwaji wa maazimio yake.

Kauli hiyo ya Mnyika ambaye ni Waziri kivuli wa Nishati na Madini imekuja siku chache tangu gazeti la East African kutoa taarifa kwamba jumla ya Dola54milioni zimegundulika kuibwa, watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco kupitia manunuzi ya mafuta ya kuendeshea mtambo wa umeme wa IPTL.
 
Gazeti hilo lilinukuu taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ikieleza kuwa kuna kikundi ambacho kazi yake ni kujinufaisha na mpango huo.
 
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mnyika alimtaka Rais Jakaya Kikwete aagize ripoti ya CAG iwekwe wazi, kuchukuliwa hatua kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo, William Ngeleja.

“Spika wa Bunge anatakiwa kuifuatilia wizara hii pamoja na ile ya Fedha kuhusu ufisadi huu,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza;

“Rais Kikwete atumie mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ibara za 33, 34, 35, 36 na 143 (4), aagize kuwekwa hadharani kwa ripoti ya ukaguzi maalum (Special Audit) uliofanyika mwaka 2011 kuhusu tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa sheria katika ununuzi wa mafuta mazito ya kufua umeme wa dharura katika mitambo ya IPTL.”

Katika taarifa hiyo Mnyika amemtaka Rais Kikwete azielekeze mamlaka na vyombo husika kumchunguza Ngeleja kwa kuwa tuhuma hizo zilitokea wakati akiwa waziri.

“Ripoti ya ukaguzi maalumu (special audit) ya mwaka 2012, ile ya uchunguzi wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhusu suala hilo ziwekwe wazi” ilieleza taarifa hiyo.

Mbunge huyo alimtaka Spika Makinda naye anatakiwa kuitisha haraka kikao cha kamati mojawapo ya kudumu ya Bunge ili kuepusha udhaifu na uzembe unaoendelea kwa sasa kwa kuwa moja ya mamlaka ya Bunge ni kuisimamia Serikali.“Juhudi hizi zinatakiwa kufanyika kwa haraka ili wizara husika itueleze kinachoendelea” ilieleza taarifa hiyo.
Mbunge huyo aliwahi kumuandikia barua Spika wa Bunge mwezi mmoja uliopita akimtaka atumie madaraka yake kukabidhi usimamizi na utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme katika moja ya Kamati za kudumu za bunge.
 
Inaeleza kuwa sasa anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Spika kuhusu tuhuma za baadhi ya wabunge na na umuhimu wa hoja ya kutaka Bunge liazimie kuunda kamati Teule kuchunguza masuala yote ya ukiukwaji wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ufisadi.
 
Taarifa hiyo inaeleza kuwa uchunguzi huo umhusishe Mkaguzi mkuu ili kuchunguza malipo yaliyofanywa kampuni za BP (Sasa PUMA Energy), Oryx na Camel Oil ili kubaini kama kuna vigogo zaidi wa Serikali waliojinufaisha kwa kisingizio cha dharura ya umeme.
 
Source:Mjengwa blog