“Naomba hili liwe wazi kwa Watanzania,
Ridhiwan Jakaya Kikwete, chini ya kampuni ambayo wanaharakati tutaleta ushahidi
wake kwa wananchi wanaotaka ukombozi, wiki hii alikuwepo Jijini Arusha na
tayari ana mkataba wa umiliki wa zaidi ya hisa asilimia 45 za kampuni ya
Tanzanite One. Hii ni biashara ya Rais wa nchi. Ametumia madaraka yake kwa siri
kupisha umiliki huu kupitia mtoto wake. Linaweza kukanushwa na kupingwa lakini
muda unafika ambapo umma wa Watanzania utaamua. Hata wakishinda kesi za
mahakamani, hawataushinda uamuzi wa umma. CCM inakufa, iko hatua za mwishokabisa.”-Lema.
(Source: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/285378-lema-amvaa-ridhiwani-kikwete.html)
No comments:
Post a Comment