Udhaifu wa kutokutekeleza mipango ya uzalishaji wa gesi na makaa ya mawe kwa
wakati umesababisha utegemezi mkubwa kwenye matumizi ya mafuta katika mitambo ya
kuzalisha umeme wa dharura. Takribani nusu ya umeme unaozalishwa nchini hivi
sasa unazalishwa kwa kutumia dizeli, mafuta ya ndege na mafuta mazito hali
ambayo imeongeza mahitaji makubwa ya uagizaji wa mafuta toka nje ya nchi.
Hii
imesababisha mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza
mafuta na hivyo kuchangia katika kuporomoka kwa thamani ya shilingi. Aidha,
ongezeko kubwa la uagizaji toka nje limeathiri urari wa biashara na hivyo
kuchangia katika mfumuko wa bei. Hivyo, Watanzania hivi sasa wanabeba mzigo wa
kupanda kwa bei za bidhaa na gharama za maisha kwa ujumla kutokana na ufisadi
kwenye mikataba, ubadhirifu katika matumizi, uzembe katika uongozi na upungufu
katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali kwenye sekta ya nishati.
Mzigo huu
usingekuwa mkubwa iwapo Serikali ingetekeleza katika mwaka wa fedha 2011/2012
maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya kuhakikisha nyongeza ya fedha kwenye bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini kwa upande wa sekta ndogo ya Gesi kwa ajili ya
mitambo ya umeme na kuharakisha kuwekeza katika Bomba la Gesi pamoja na ujenzi
wa mtambo wa kutengeneza Gesi (LPG extraction Plant).
www.mnyika.blogspot.com
No comments:
Post a Comment