Pages

Saturday, July 14, 2012

Msome huyu jamaa akimshauri Dr Slaa; Je ana Hoja?

                                                                   Dr Slaa.

Nianze kwa kusema kuwa nakukubali Dr slaa kwa kazi nzuri ulioifanya bungeni kipindi cha 2005 - 2010 kabla hujagombea urais. Nilikuelewa kama mtu ulie makini, mzalendo uso yumbishwa na porojo za kisiasa! siyo siri hicho kipindi ulilitumikia taifa kama mzalendo halisi. Hongera kwa hili! lakini baada ya kugombea urais Dr umekua ukibadilikabadilika kimsimamo na umekua hueleweki na wafuasi wako. Elewa kuwa katika uchaguzi wa 2010, uliungwa mkono na watanzania wakikutaka wewe kuwa rais wao. Hawakujali itikadi za vyama vyao. walikuona kama mkombozi wao. mambo yafuatayo, nionavyo mimi, yanakutoa kwenye msitari uliyokujengea umaarufu.

KAULI ZAKO TATA
wewe ni Dokta, una Phd (hata kama ni ya mambo ya kidini lakin ni Phd). Upeo wako wa kuchambua mambo lazima uwe wa hadhi ya Phd. kauli hizi zinanitia wasiwasi kuhusu uwezo wako wa kiuchambuzi na kifalsafa!
"Leo asubuhi Ofisa wa Makao Makuu ya Polisi amenipigia simu kuomba appointment ya kukutanana na polisi kwa mahojiano". "nasema sina muda". "sisi hatuendi polisi kwa sababu walishatudanganya mara nyingi tu. kama wanataka waje watukamate lkn sisi hatuendi polisi". la kushangaza, jana majira ya saa 4 na dakika 45 asubuhi, Dr slaa na lema walikwenda wenyewe makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano! walihojiwa kwa saa 2 kisha wakaruhusiwa kuondoka. alipohojiwa na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya polisi, slaa alisema "tumehojiwa lakini hatukukubali maelezo yaandikwe. hakuna sehemu ambayo tumetia sahihi maelelezo ya mahojiano".

NAMUULIZA Dr YAFUATAYO
 
1- ulisema piga, ua, garagaza hutokwenda polisi labda waje kukukamata. la kushangaza ulikwenda mwenyewe!
2- mahojiano siyo lazima yaandikwe. mahojiano ya kuandikwa kwa teknolojia ya leo hayana mashiko sana. mahojiano mazuri ni yale ya sauti inayosikika. una uhakika hujarekodiwa!? natilia mashaka Phd yako kutokana na kauli hiyo. eti nimekataa mahojiano yasiandikwe.

Hivi majigambo, ubeberu na ukaidi kwa jeshi la polisi uliouonesha jumatatu ulipoongea na waandishi wa habari vimeishia wapi? hukupima na kuelewa kuwa jeshi la polisi lina nguvu sana!? hukuelewa kuwa wafuasi wako watakushangaa wakiona unakwenda polisi mwenyewe? Dr wangu pima kauli zako. nina mifano mingi ya kauli zako tata lakini nazihifadhi hadi siku nyingine.


Kadhia ya rose kamili na josephine mshumbusi (sp)
suala hili limekukalia vibaya dr. kwanza ulimhonga rose ubunge ili akae kimya lakini inaelekea hajaridhika na ofa ya ubunge! ulitaka ufunge ndoa mwezi huu na josephine. umewekewa pingamizi. nakushauri ujitahidi kumalizana na mama rose nje ya mahakama. la sivyo suala hili litakugharimu sana na hadhi yako itaendelea kushuka sana. sasa hivi jua kwamba ww siyo slaa aliegombea urais 2010. kosa ulofanya kuzaa ukiwa padri. kosa ulofanya kumtorosha na kujimilikisha mke wa mtu mama josephine, hayatokuacha salama! umeteleza kijamii na kisiasa lakini jitahidi kumalizana na mama rose. mpe hizo 50 m ili mambo yaishe. tunamtaka slaa mwenye uono wa kimantiki kama ule wa 2005-2010 bungeni.


USHAURI WA BURE KWA CHADEMA
chadema ya akina slaa na zitto bungeni ya 2005 - 2010 ilikua chadema yenye mikakati maridhawa. walikua wachache lakini walitegemea kitu kimoja. KUJENGA HOJA. hiyo ndiyo silaha ilioipa chadema umaarufu. chadema ya 2010 hadi sasa bungeni imekua chadema ya "fungeni milango tupigane" "mwongozo wa spika", "mh spika taarifa", "pigeni wanaonunua viwanja kawe hata kuwaua sawa. nitajibu kama mbunge wenu", "nchemba ulishiriki katika EPA", "majaji ni wazee na hawana elimu. wanabebwatu" "Rais ni dhaifu" nk........... chadema yenye constructive points and ideologies iko wapi? ccm wamekupandisheni hasira ili kukuyumbisheni kwenye mijadala ya bunge na nyinyi mkaingia mkenge! bado fursa ya kubadilika ipo

Dr slaa wewe ni jembe. nimeandika haya ili kukushauri kama shabiki wako wa 2005- 2010. sasa hivi nimesimamisha ushabiki kwako hadi nione umebadilika! ni hayo tu!

Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo!)

www.jamiiforum.com







 

No comments:

Post a Comment