Nimefika Singida
kuitikia mwito wa Polisi kutoa maelezo kuhusu mkutano nilioalikwa Iramba kwa
nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.
Nimekutana na RPC,
amesema kwamba nisubiri mpaka saa 10:30 alasiri ndiyo nikutane nao kwa kuwa kwa
sasa kuna kikosi cha upelelezi toka Dar Es Salaam kimekwenda eneo la tukio.
Nimemuuliza RPC maswali mawili;
1. Wameniita kutoa
maelezo kama mtuhumiwa au shahidi?
Amenijibu kuwa ni
mahojiano ya kawaida.
2. Kwanini mpaka sasa
watuhumiwa 12 waliofunguliwa jalada NDG/RB/190/2012 kwa kurusha mawe kwenye
mwanzo wa mkutano wakati Bwana Waitara akitoa hotuba ya utangulizi huku polisi
wakiachia hali hiyo. Baada ya kufungua jalada na polisi wa juu kupigiwa simu
kuwa kuna njama kati ya Polisi na CCM
hali ilitulia, Waitara akamaliza hotuba yake, Dkt Kitila akasalimia name
nikahutubia kwa amani na kwenda kwenye mkutano mwingine. Mauaji yalitokea baadae
mbali na
tulipohutubia.
John John MNYIKA,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
18 Julai, 2012
No comments:
Post a Comment