Nimekuwa nikifatilia matamasha
makubwa ya burudani hapa nchini yanayohucsha wasanii wa Hip Pop nakugundua kuwa
msanii Roma Mkatoliki hugeuza jukwaa la burudani kuwa jukwa la siasa kwa kutoa
mistari inayoamsha hasira za mashabiki dhidi ya serikali.
Leo( Jana) nikiwa ktk viwanja vya
fukwe za coco beach ktk tamasha la Tigo msanii huyo alihamasisha maelfu ya
mashabiki waliojitokeza kuonesha ishara ya vidole viwili na tamasha kugeuka
kuwa kama mkutano wa chadema, hakika hali ilinichukiza sana kwani audience yote
ililipuka kwa mayowe baada ya kutolewa mistari iliyochochea chuki dhidi ya
serikali na vyombo vya dola kama police. Picha za tukio hilo nitazitupia badae.
Mytake serikali sasa inayowajibu wa kutunga
sheria kali ili kuwadhibiti wasanii kama Roma mkatoliki ambao wanageuza
majukwaa ya burudani kuwa majukwaa ya siasa kwani hali hiyo inaweza leta
uvunjifu wa amani kwani ktk matamasha ya burudani wanahudhuria mashabiki wenye
itikadi mbalimbali ya vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment