Serikali imeamua kuagiza
madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao
wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita. Habari kutoka katika moja ya
vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika
kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti
wa Rais Jakaya Kikwete. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais
Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi
zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao. Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha
sh bilioni 200 kimetengwa.....( source: www.mjengwa.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment