Pages

Monday, July 9, 2012

Upatikanaji wa maji tatizo ni ongezeko la watu-Prof Magembe


Waziri wa maji Profesa Jumanne Magembe amesema kuwa moja ya mambo yaliyochangia kutokupatikana kwa maji ni ongezeko kubwa la idadi ya  watu. Mh waziri alisema sababu hiyo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara ya maji kwa mwaka 2012/2013 leo hii asubuhi.

Alisema kuwa utoaji wa huduma ya maji unakabiliwa na changamoto yakuongezeka kwa idadi ya watu kusikoendana na uwekezaji. Hali hiyo ni dhahiri katika maeneo yote ya vijijini na mijini. Kiwango cha ongezeko la watu kwa mwaka kitaifa ni asilimia 2.3 vijijini, asilimia 4.5 mijini, na asilimia 6 katika Jiji la Dar es Salaam.

Ongezeko lingine ni kukua kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la viwanda na kupanuka kwa ujenzi wa makazi.

Mkali.
0719466466

No comments:

Post a Comment