Pages

Monday, July 2, 2012

Mheshimiwa Machali amtaka waziri wa Utumishi aseme ongezeko la Mshahara.

Nimefuatilia kwa karibu sana Mjadala wa bunge jioni 02 july 2012. Mheshimiwa Moses Machali, mbunge kupitia chama cha NCCR mageuzi amemtaka wazi Waziri wa Utumishi aseme viwango mishahara vimeongezeka kwa viwango gani na si kusema kiujumla. Wakati akiendelea kuchangia mara umeme ukakatika bungeni hivyo kumfanya ashindwe kuchangia. Ameongea mambo mbalimbali ikiwamo maslahi ya walimu, mikataba mibovu hususani kwenye sekta ya madini. Ameshauri kuwa utawala bora utakuwa mzuri tu endapo mianya ya kukwepa kodi itapungua. Mheshimiwa Machali ameitaka serikali kubadilika kiutendaji ili kuongeza tija kwa wafanyakazi wa serikali.

No comments:

Post a Comment