Pages

Thursday, July 5, 2012

BBC; Dr. Olimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine


:Source BBC: na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini
Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.
Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.
Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii
""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

No comments:

Post a Comment